Tuesday, July 26, 2011

MAGOLI YA FAINALI COPA AMERICA URUGUAY ILIPOINYANYASA PARAGUAY

Suarez, Forlan waonesha viwango.

MANCINI ANA MATUMAINI YA KUMNASA SERGIO AGUERO

Meneja wa Man City Roberto Mancini amefunguka na kusema kuwa ana matumaini makubwa ya kumnasa Sergio Aguero kutoka Atletico Madrid mwishoni mwa wiki hii. Man C inafungua milango ya maongezi na Atletico Madrid kwa kuwa Srgio amekuwa ni mmoja kati ya wachezaji anaowahitaji katika kikosi chake.
Sergio Aguero
Pamoja na upinzani uliopo kutoka kwa Real Madrid na Juventus ambao nao wanatajwa kumuwania Sergio lakini Mancini ana matumaini ya kushinda kinyang'anyiro hicho mwishoni mwa mwezi huu."Sielewi kwa sasa lakini ninachojua Atletico walikuwa na maongezi na Sergio kabla ya mwisho wa wiki" alisema Mancini.
"Nafikiri kati ya siku nne au tano kabla ya mechi inayofuata,na inaweza kuwa wiki hii tukamaliza mazungumzo"Alioneza Mancini.
"Aguero amecheza Copa America, kama tukikubalina nataka nizungumze nae mwenyewe kwasababu nataka nijue maoni yake(kuhusu kucheza Manchester City)" Alifunguka zaidi kocha huyo wa Manchester City.

ASTON VILLA YAKUBALI KUTOA DAU KUMNYAKA N'ZOGBIA TOKA WIGAN

Charles N'zogbia
Aston Villa imefungua milango ya maongezi na Wigan Athletic juu ya kumsajili Charles N'zogbia mwenye umri wa miaka 25 na imekubali kulipa ada ya uhamisho ya paundi za uingereza 9.5 milioni. Meneja wa Villa Alex Mc Leish ameridhishwa na kiwango cha N'zogbia na timu yake imeamua kufanya mazungumzo rasmi na Wigan ili kumsajili mchezaji huyo. Habari kutoka ndani ya klabu ya Villa zinasema pesa ipo ya usajili baada ya kumuuza Ashley Young kwenda Man United na Stewart Downing kwenda Liverpool zote za uingereza, kabla ya kusaini mkataba mrefu ndani ya Villa N'zogbia anatarajiwa kwanza kufanyiwa vipimo vya afya.

FERGUSON ASEMA AMERIDHIKA NA WACHEZAJI KWA SASA

Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson anasema hatomsajili mchezaji yoyote hadi pale watakapokabiliana na majirani zao Manchester City katika uwanja wa Wembley.

Sir Alex Ferguson
Tayari ameshamsajili Ashley Young, Phil Jones na mlinda mlango David de Gea.
Kiungo wa Inter Milan Wesley Sneijder amehusishwa na Manchester United.
Lakini Ferguson anasema: "kwa wakati huu,sioni ya kuongeza mchezaji mwengine. Mchezaji ambaye tunamuhitaji hatujamuona kwa sasa."
Aliongeza kuwa: " Tumepoteza wachezaji watano mwaka huu kutokana na wao kuwa na umri wa miaka zaidi ya thelathini".
"Hilo limetusaidia kupata pesa za kuwasajili wachezaji watatu vijana niliowaleta kwenye timu.
"Nimeridhika na wachezaji nilionao kwa sasa."
Kutokana na kustaafu kwa kiungo Paul Scholes,majina kadhaa yametajwa kama yanayofikiriwa kujumuishwa kwenye kikosi cha Manchester United kama vile Sneijder, Samir Nasri wa Arsenal na Luka Modric wa Tottenham.
Hata hivyo Ferguson amekanusha kama anafikiria kumsajili Sneijder, akisema kwamba "hana nia ya kumsajili".

Monday, July 25, 2011

BALLOTELI AFANYA MZAHA ATOLEWA AMBWATUKIA MANCHINI

AMY WINEHOUSE AFARIKI DUNIA

Mwimbaji maarufu mwanamke wa Uingereza, Amy Winehouse, amekutwa amekufa katika fleti yake mjini London.


Amy amefariki akiwa na umri wa mika 27 tu.
Amy Winehouse alishinda tuzo kadha kwa albamu yake ya pili, Back to Black, ambayo ilitolewa mwaka 2006.

Sababu ya kifo chake haijajulikana.

Lakini mwimbaji huyo amekuwa akipambana na uraibu wa ulevi na mihadarati kwa muda.

Mara nyingi alitokeza kwenye tamasha akiwa amelewa.

BALLOTELI ATOLEWA UWANJANI BAADA YA KUFANYA MZAHA KWA TIMU PINZANI

Mchezaji wa Manchester City Mario Balotelli alitolewa nje katika kipindi cha kwanza katika mechi yao dhidi ya LA Galaxy kwa kutoonyesha heshima kwa wapinzani wake.
Mancini na Balotelli
Mshambuliaji huyo wa Italia mwenye umri wa miaka 20 alikuwa karibu kufunga goli,lakini hakufunga na badala yake akapiga mpira kwa kisigino na kukosa goli.

Kocha wa Manchester City Roberto Mancini alimpumzisha Balotelli kutokana na tukio hilo lakini wakati akitoka nje ya uwanja alionekana kujibizana na kocha wake.

Awali Balotelli alifunga bao kupitia mkwaju wa penalti katika mechi hio ya kirafiki iliomalizika kwa sare ya 1-1.

Man City Imepata ushindi wake wa tatu katika mechi zake za kujiandaa kwa msimu wa ligi kuu ya England.Katika uwanja huo mashabiki wa LA Galaxy walimzomea Balotteli kwa kitendo chake hicho.

Hii si mara ya kwanza kwa mchezaji huyo wa zamani wa Inter kujikuta katika matatizo na Kocha Mancini, ambaye pia alikuwa kocha wake nchini Italia.