Wednesday, October 12, 2011

PICHA AMBAZO HUJAWAHI KUZIONA POPOTE





Bruce Lee na Chuck Norris

Cheguevara na Fidel Castro

Copacabanna Beach,Rio De Jeneiro.BRAZIL

Meli ya Titanic ikiwa chini ya Bahari

Familia ya OSAMA,Osama amezungushiwa kiduara chekundu

Tuesday, October 11, 2011

VAN PERSIE AWEKA "MJENGO" SOKONI

Van Persie says he believes in Arsenal, puts house up for sale
Nyumba ya Van Persie ambayo ameiweka sokoni inauzwa paundi za Uingereza milioni 1,395,000.

Van Persie says he believes in Arsenal, puts house up for sale
Sehemu hii ni  dhahiri kuwa nyumba hii inamilikiwa na mwanamichezo kutokana na mpangilio wa upambaji wake.

Thursday, September 29, 2011

Yanga yafanya maangamizi yaisambaratisha Coastal Union 5-0














Davis Mwape akichanja mbuga

Kenneth Asamoah alitia kambani mabao mawili na kuiongoza Yanga kuwasambaratisha wagosi wa kaya ambao ni vibonde wa ligi Coastal Union kwa mabao 5-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mabingwa hao waliopoteza mvuto kwa mashabiki wao kutokana na kuanza ligi kwa kusuasua jana walionekana tofauti kabisa kwani katika dakika ya nne mshambuliaji wao wa kimataifa wa Ghana, Asamoah alifunga bao la kwanza kabla ya Shamte Ally, Davies Mwape, Nurdin Bakari na Mghana huyo kufunga kalamu hiyo ya kishindo.

Kiungo Idrisa Rajabu alitoa mchango mkubwa kwenye mauaji hayo kwa kutengeneza mabao matatu kati ya matano ikiwa ni mechi yake ya tatu kuanza kuitumikia Yanga.

Umakini huo wa safu ya ushambuliaji ya Yanga unamfanya kocha Sam Timbe kutomfikiria kabisa mshambuliaji wake Jerryson Tegete aliyefunguliwa na uongozi wake hivi karibuni.

Timbe aliwapumzisha Mwape, Shamte na Asamoah na kuwaingiza Rashid Gumbo, Julius Mrope na Hamis Kiiza.

Mabingwa hao sasa wamefikisha pointi 12, huku Coastal wakibaki mkiani na pointi zao nne katika ligi hiyo inayoongozwa na Simba yenye pointi 18.

Mshambuliaji Davies Mwape alijaribu kufunga bao la mapema katika dakika ya 2, lakini mpira wake wa kichwa ulidakwa na kipa wa Coastal Union, Omar Hamis na dakika mbili baadaye Asamoah alifungia Yanga bao la kuongoza akimalizia kwa kichwa krosi nzuri ya Idrisa Rajabu.

Mshambuliaji wa kimataifa wa zamani wa Kenya, Ben Mwalala alikaribia kuipatia timu yake bao katika dakika 11 baada ya kuunganisha vizuri krosi kutoka upande wa kulia iliyopigwa na Daniel Lianga, lakini kipa wa Yanga, Yaw Berko aliupangua mpira huo.

Winga Shamte Ally aliipatia Yanga bao la pili katika dakika ya 21 akiunganisha kwa umakini krosi ya Asamoah kutoka upande wa kushoto, wakati Wagosi hao wakishaanga uwanja wa Taifa, Mwape aliendeleza kalamu ya mabao kwa kufunga bao la tatu kwa Yanga katika dakika ya 30 kwa kuunganisha kwa shuti kali pasi ya Rashid kutoka winga ya kushoto.

Mshambuliaji Mwalala alijaribu kuwaongoza vijana wake bila ya mafanikio kwa sababu katika dakika ya 35 alipiga shuti kali lililopanguliwa na Berko na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

Nurdin Bakari aliipatia Yanga bao la nne katika dakika ya 41, akimalizia pasi nzuri ya Asamoah.

Yanga ambayo safu yake ya ushambuliaji ilikuwa ikilaumiwa kwa ubutu ilionekana kuwa bora mbele ya mabeki dhaifu wa Coastal Union ambao wameruhusu timu hiyo kufungwa mechi sita kati ya nane ilizocheza msimu huu.

Coastal mabingwa wa mwaka 1988 wanaofundishwa na Hafidh Bardu walishindwa kucheza kabisa na kumtegemea Mwalala wakati wapinzani wao Yanga wakitawala asilimia 80 ya ya mchezo huo katika nafasi ya kiungo na ushambuliaji.

Asamoah alipachika bao la tano katika dakika ya 46 akipokea krosi ya Rajabu na kuifanya Yanga kushinda kwa mabao 5-0. Asamoah amefunga mabao manne tangu msimu huu wa Ligi Kuu uanze.

Kocha wa Coastal Union, Badru alimpumzisha kipa wake Hamis aliyeruhusu mabao manne na kumwingiza Godson Mmasa, pia Coastal ilimtoa Mwinyi Abdulrahman na kumuingiza Said Swed

Arsenal,Barcelona zafanya kweli ligi ya mabingwa ulaya

Arsenal 2-1 Olympiakos


Bate borisov 0-5 Barcelona


Valencia 1-1 Chelsea


AC Milan 2-0 Victoria Pulzen

Wednesday, September 28, 2011

MATOKEO MECHI ZA LIGI YA MABINGWA ULAYA

CSKA MOSCOW 2-3 INTER MILAN

REAL MADRID 3-0 AJAX

   BAYERN MUNICH 2-0 MAN CITY


               TRABZONSPOR 1-1 LILLE

 MAN UNITED 3-3 BASEL

Arsenal,Chelsea kibaruani leo ligi ya mabingwa ulaya

WINGA wa Chelsea, Juan Mata atakutana na rafiki zake wakati atakaporudi kucheza mechi Ligi ya Mabingwa dhidi ya Valencia leo ikiwa ni miezi mwezi moja tangu alipoondoka.

Kocha Andre Villas-Boas alitumia karibu dola 40.4 milioni kumsajili nyota huyo mwenye miaka 23 na tayari ameonyesha uwezo wake kwa kufunga kwenye mchezo wa kwanza wa Kundi E walioshinda 2-0 dhidi ya Bayer Leverkusen.“Nipo tayari kucheza dhidi yake na wote tunamsubili,” alisema winga Valencia, Pablo Hernandez aliyekuwa wakilala chumba kimoja na Mata.

“Itakuwa ni siku yake nzuri kurudi nyumbani, lakini hatutakuwa na urafiki uwanjani. Tutafanya kila kitu kuhakikisha tunawafunga pamoja na Juan, baada ya hapo tutamtakia mfanikio mema.”

Chelsea wapo ipo kwenye kiwango cha juu baada ya kushinda 4-1 dhidi ya Swansea City pale Jumamosi na kuwafanya wapande hadi nafasi ya tatu katika Ligi Kuu, nyuma kwa pointi tatu kwa vinara Manchester United na Manchester City.Mshambuliaji wa Hispania, Fernando Torres alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika 39 pale Jumamosi, lakini anaonekana kurudi kwenye kiwango chake akiwa ameshafunga mabao mawili katika mechi mbili mfululizo.

Safu ya ushambuliaji wa Chelsea imeimarika na kurejea kwa nyota wa Ivory Coast, Didier Drogba aliyeingia kuingia akitokea benchi na kufunga baada ya wiki nne za kuwa nje kwa sababu ya kuumia.

LONDON, Robin van Persie ameanza kuthibisha kwamba anaweza kuiongoza Arsenal anategemewa kuibeba klabu hiyo leo kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Olympiakos.Van Persie alichukua unahodha huo baada ya Cesc Fabregas kutimikia Barcelona, Robin alifunga mabao mawili waliposhinda 3-0 dhidi ya Bolton Wanderers Jumamosi.

Olympiakos wenyewe wamepoteza mechi tisa walizocheza dhidi ya timu za England kwenye mashindano ya Ulaya, wakiwa wamefungwa mabao 29 na wao kufunga moja tu.

Van Persie, 28, ameshafunga mabao matano msimu huu na Wenger anaamini Mdachi huyo aliyeripotiwa na vyombo vya habari vya England, Jumatatu hataki kuharakisha kuongeza mkataba wake wake unamalizika 2013, kuwa kwa sasa amekuwa na anaweza kuongoza kwenye ufungaji na kuwatia moyo wenzake.

“Robin amekuwa kutoka mvulana anayesumbuliwa na presha za jamii wakati anakuja hapa na leo ni mtu mzima,” Wenger aliimbia tovuti ya Arsenal.Hilo alitakuwa vumbi pekee kutimka wiki hii Ulaya mashariki wakati BATE Borisov watakapowakaribisha mabingwa wa Ulaya, Barcelona katika mchezo wa Kundi H hapo leo.

BATE walitoka sare1-1 na Belshina Bobruisk pale Ijumaa, Barca walituma salamu kwa kuisambaratisha Atletico Madrid 5-0 Jumamosi huku mchezaji bora wa Dunia, Lionel Messi alifunga mabao matatu peke yake.

KIKOSI KITAKACHOKABILIANA NA MORROCCO HIKI HAPA


Tanzania imetangaza kikosi kitakachopambana na Morrocco katika michuano ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani.
Taarifa iliyotolewa na chama cha soka cha Tanzania TFF imesema Taifa Stars ambayo inafundishwa na kocha Jan Poulsen itaondoka Oktoba 6 kwenda Morrocco, na kujitupa uwanjani Oktoba 9 mjini Marrakech kupambana na timu ya taifa ya Morrocco.

Kikosi hicho cha wachezaji 23 ni:

Makipa:


Shabani Dihile  (JKT Ruvu Stars)
Juma Kaseja  (Simba)
Shabani Kado   (Yanga)


Mabeki:


Shadrack Nsajigwa (Yanga)
Erasto Nyoni (Azam)
Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya)
Amir Maftah (Simba)
Aggrey Morris (Azam)
Juma Nyoso (Simba)
Victor Costa (Simba)


Viungo:


Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway)
Nurdin Bakari (Yanga)
Shabani Nditi (Mtibwa Sugar)
Jabir Aziz (Azam)
Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada)
Mrisho Ngassa (Azam)
Ramadhan Chombo (Azam)


Washambuliaji:


Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam
Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC)
Dan Mrwanda (DT Long An, Vietnam)
Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden)
John Bocco (Azam)
Hussein Javu (Mtibwa Sugar)


Tanzania iko kundi D, pamoja na Algeria, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Morrocco.

Tanzania ina pointi 5 baada ya michezo mitano na kushinda mmoja, sawa na Algeria. Morrocco na Jamhuri ya Afrika ya Kati zinaongoza kundi hilo zikiwa na pointi 8.