Thursday, November 24, 2011

Picha bora za mwaka 2011

Photo: Tree in a cornfield
Shamba la mahindi huko Sao Paulo,Brazil

Photo: Mountain peak at night
Dente del Gigante,Italy

Photo: Green sea turtle swimming underwater
Kasa wa kijani  picha hii ilipigwa huko Hawaii.

Photo: Birds in a tree
Ndege mtini huko Pantanal,Brazil

Photo: A veiled woman walking by a mosaic wall
Msikiti wa Hazrat uliopo Afghanistan

Photo: Aerial view of a bazaar
Hema sokoni nchini Uturuki

Photo: Climber dangling from red rock
Mwamba maeneo ya Sedona,Arizona

Photo: Surfer riding a large wave
Jamaa aki-surf huko Hawaii

Photo: Aerial view of a colorful terraced rice field
Shamba la mpunga,picha ilipigwa huko China

Photo: Brightly dressed people at celebration
Sherehe ya harusi ya kabila la Samburu,picha ilipigwa nchini Kenya

Photo: Women holding candles in front of a lit palace
Sherehe za Diwali huko India

Photo: Muslims praying in a temple
Msikiti wa Istiklal uliopo Indonesia

Photo: Boat sailing along coast of Hong Kong at night
Cityscape Hongkong,China

Mafuriko Thailand, Viwanda vya magari Honda na Toyota vyajaa maji

Car pool: An aerial view of submerged cars at the Honda Motor factory in Ayutthaya province, Thailand, which has been caught up in the country's flooding
Magari yakiwa yamezama ndani ya maji kutokana na mafuriko yaliyovamia kiwanda hicho katika kitongoji cha Ayutthaya,Thailand

High and dry: Aerial view shows cars standing on bridge surrounded by floodwaters at the Honda Motor factory in Ayutthaya province, Thailand
Magari yakiwa yameegeshwa kwenye daraja katika kiwanda cha Honda huko Ayutthaya,Thailand.

Life buoy: Thai flood victim in a small bath tub shaped bucket paddling with flip-flop sandals past a flooded Toyota dealership in Bangkok
Dogo akijaribu kukatiza mitaani kwa kutumia karai kama mtumbwi wa kukatiza katika maji ya mafuriko

Waterway: Thai flood victims pass Toyota cars at the flooded Toyota Bangkok branch in Don Mueang district of Bangkok, Thailand
Waathirika wa mafuriko wakipita karibu na tawi la kiwanda cha magari cha Toyota kilichopo Don Mueang wilaya ya Bangkok huko Thailand. 

Row your boat: Thai flood victims passing the flooded Toyota car showroom in Bangkok, Thailand
Show room ya Toyota katika dimbwi la maji.

Driven out: An aerial view of Honda Motor factory buildings submerged by floodwaters at Rojana Industrial Estate in Ayutthaya province, Thailand
Kiwanda cha magari ya Honda kikiwa kimefurika maji katika eneo la viwanda la Rojana. Thailand.

Shot bora zaidi kuwahi kutokea kwenye mchezo wa Tennis.

Ntombenhle

Arsenal Barca mwendo mdundo ligi ya mabingwa

Van Persie
Van Persie ana magoli 18 katika mechi 18 msimu huu

Arsenal imeingia katika ngazi ya makundi ya ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa kuichapa Burrusia Dortmund kwa mabao 2-1.

Robin Van Persie alipachika mabao hayo mawili na kuhakikisha Arsenal inaingia kwa mara nyingine tena katika ngazi ya timu 16.
Arsenal inakuwa timu ya kwanza ya England kusonga mbele na pia kumaliza juu katika kundi lao.

Chelsea nayo ilishindwa kutamba mbele ya Bayer Leverkusen baada ya kuzabwa 2-1.

Ili kusonga mbele Chelsea itahitaji sare au kushinda mchezo wake wa mwisho dhidi ya Valencia.

Barcelona nayo iliishinda AC Milan kwa 3-2.

Katika michezo mingine BATE Borisov ilichapwa 1-0 Plzen, Marseille kufungwa 1-0 na Olympiakos, Shaktar Donetsk kuzabwa 2-0 na FC Porto, Valencia kuiachia kisago 7-0 Genk huku Zenit St Petersburg ikitoka sare ya 0-0 na Apoel Nicosia.

Wednesday, November 23, 2011

Tsvangirai aoa mfanyabiashara,Mahari zaidi ya milioni 60 za kitanzania (USD 36,000) na Ng'ombe 10


Tsvangirai na mkewe mtarajiwa Bi Tembo

Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai amevunja mwiko kwa kufunga ndoa mwezi Novemba.
Kitamaduni inahofiwa kuwa kufunga ndoa mwezi Novemba kutaletea wanandoa bahati mbaya.

Lakini waziri huyo mkuu amefanya harusi na Locadia Tembo katika sherehe za kikabila siku ya Jumatatu, baada ya kutoa mahari ya dola elfu 36 na ng'ombe 10.

Mke wake wa kwanza, Susan, alifariki katika ajali ya gari muda mfupi baada ya Bw Tsvangirai kuingia katika serikali ya umoja wa kitaifa na Rais Robert Mugabe mwaka 2009.

Viongozi hao wawili walitia saini makubaliano ya kuunda serikali ya pamoja, kufuatia uchaguzi wenye utata ulioghubikwa na ghasia.

Dalili za mwanzo kuwa Bw Tsvangirai anafikiria kufunga ndoa zilikuja wakati wa mkutano wa hadhara wa chama chake cha MDC mwishoni mwa wiki, katika eneo la Chitugwiza, nje kidogo ya jiji la Harare.

Kiongozi huyo wa MDC,59, alifanya mzaha kwa watu waliokusanyika kwa kusema waandishi wa habari wamekuwa wakiandika kuhusu yeye kuwa na marafiki wa kike. "Lakini kwani kapera anakatazwa kufanya hivyo?" alioluza mashabiki wake na kujibiwa kwa kicheko na kupigiwa kofi.

Bi Tembo, 39, ni mfanyabiashara wa bidhaa za rejareja na pia ni dada wa mbunge aliye katika chama cha Mugabe cha Zanu-PF - jambo ambalo limeleta utata kwa baadhi ya wafuasi wa MDC.

Lakini wafuasi wa MDC wanaonekana kufurahishwa na hatua ya kiongozi wao, wakisema kuwa uchaguzi ukiwa umekaribia mwakani, mgombea urais atanufaika kwa kupata msaada kutoka kwa mke wake na mshauri katika kampeni.

Katika mitaa ya Harare kulikuwa na maoni tofauti, hata hivyo wengine wakiwa na wasiwasi kuhusu harusi hiyo ya mwezi Novemba.

"Kama mzee anatakiwa kuongoza kwa mfano - wao ndio wanatuambia tusioe mwezi Novemba," mtu mmoja aliiambia BBC.

Baada ya kutoa mahari, maarufu kama lobola, kwa ndugu wa Bi Tembo katika sherehe ya kitamaduni huko Criston Bank, takriba kilomita 25 kaskazini mwa Harare, Bw Tsvangirai imeripotiwa alitaka ifanyike harusi 'nyeupe' katia kufuata utamaduni.

Ni katika sherehe hizi zinazoegemea zaidi katika utamaduni wa Kizimbabwe, zinatoa dalili kuwa zitafanyika wakati wa mapumziko ya Krismasi.

Jameson Timba, waziri wa nchi katika ofisi ya waziri mkuu, ameiambia BBC kuwa Bw Tsvangirai "atatoa tangazo rasmi kuhusu mipango ya harusi yake wakati utakapowadia".

Ligi ya Mabingwa Man C yachapwa, Man U yatoa sare

Balotelli

Manchester City ilishindwa kutamba mbele ya Napoli baada ya kuzabwa 2-1. Napoli ndio walianza kupachika bao la kwanza kupitia Edison Cavani.

Mario Balotelli alisawazisha bao hilo, lakini Cavani alizamisha meli ya City kwa kuandika bao la pili. City sasa watalazimika kusibiri matokeo ya mchezo kati ya Napoli na Villareal ili kufahamu hatma yao ya kuingia raundi ya makundi hata kama watashinda mchezo wao dhidi ya Bayern Munich.

 Manchester United nayo ililazimishwa sare ya 2-2 na Benfica kwenye uwanja wa Old Trafford. Man United walijifunga katika dakika ya 4 kupitia beki wake Phil Jones. Dimitar Berbatov alisawazisha bao hilo. Darren Fletcher aliandika bao la pili la United dakika ya 59, lakini kabla hata kabla mashabiki hawajamaliza kushangilia Benfica walisawazisha bao hilo katika dakika ya 60.
Benfica sasa wamefuzu. United wanahitaji pointi moja kuzonga mbele.

Real Madrid nayo iliendeleza wimbi lake la ushindi kwa kuikandika Dinamo zagreb 6-2.

Bayern Munich ikaichapa Villareal 3-1, CSKA Moscow ikicheza nyumbani ilifungwa 2-1 na Lille.

Lyon na Ajax zilitoka sare ya 0-0, Otelul Galati nayo ikafungwa na FC Basel 3-2.

Trabzonspor ikatoka sare ya 1-1 na Inter Milan.