Monday, March 26, 2012
MAAMUZI YA TFF KUPENDELEA VILABU VIKUBWA YANAUA SOKA LETU(kusimamisha adhabu za wachezaji wa Yanga)
TFF kupitia kamati ya Usuluhishi na Nidhamu(kamati ya Tibaigana) imesimamisha adhabu walizopewa wachezaji mabondia wa Yanga, kwa madai kuwa kamati ya ligi ya TFF haina mamlaka ya kutoa maamuzi yaliyotolewa. maswali yanakuja;
1-nani alipeleka mashitaka kwenye kamati hiyo?
2-walikuwa wapi muda wote huo kusema kuwa kamati ile haina mamlaka?
3-Kamati ile ilitumia vielelezo vipi kutoa adhabu kwa wachezaji mpaka kamati ya usuluhishi na nidhamu iseme Tff hawajapeleka vielelezo?
4-Wamesimamisha adhabu zilizotolewa na kamati ya ligi na adhabu alizotoa refa zinaendelea,sasa mchezaji Mwasika aliyempa refa ngumi ya uso hakupewa hata kadi ya njano inakuwaje?
5-Kuna wachezaji kama Cannavaro wameshatumikia adhabu ya kadi aliyopewa je maamuzi mengine yatakayotolewa na kamati ya usuluhishi na nidhamu hayatamuathiri?
5-Kamati ya ligi imetoa adhabu ngapi na Hazikupingwa na kamati ya nidhamu na usuluhishi(kamati ya Tibaigana)?
Ninaamini kamati ya Ligi ya TFF ina watu makini na ni viongozi makini na hata aliyepeleka mashitaka kwenye kamati hiyo aliamini inaweza kufanya maamuzi na ndio maana kamati ikafanya kazi yake sasa hii kamati ya Tibaigana iliyotengua maamuzi hayo ninaamini walikuwa na taarifa ya maaamuzi ya kamati ya Ligi iweje wakakaa kimya mpaka sasa wakati wachezaji wameshatumikia adhabu waseme kamati haina hadhi ya kutoa maamuzi?
Naomba niwe muwazi katika hili sidhani kama adhabu hizo wangekuwa wamepewa wachezaji wa Oljoro au Coastal Union kamati ya Tibaigana ingehangaika kuzisimamisha na kutumia muda kukaa vikao vingine, ikumbukwe hapo gharama zimetumika kuita waandishi wa habari pale habari maelezo watu wakaacha kazi zao wakakaa kusikiliza maamuzi ya kamati ya Ligi na watu wakalipana posho na waandishi wakatumia gharama kuandika habari ya adhabu za wachezaji hao na wananchi wakatumia pesa zao kununua magazeti kupata habari hizo halafu mwisho wa siku pamoja na usumbufu na gharama zote hizo anatokea mtu na kusema maamuzi yametolewa na kamati isiyokuwa na mamlaka,najiuliza mlikuwa wapi muda wote huo kama sio hii kamati ya Tibaigana kufanya kazi kwa maslahi ya timu fulani?
Hakika soka letu kwa utendaji wa kubabaisha kama huu litaendelea kudidimia wadau tujiandae kupinga adhabu itakayotolewa na kamati ya usuluhishi na nidhamu ambayo kwa hili hatuna imani nayo.

SIMBA YAFANZA KWELI YAWARUDISHA ES SETIF ALGERIA VICHWA CHINI
Wachezaji wakisalimiana kabla ya mpambano huo kuanza
Timu ya soka ya Simba ya jijini Dar es salaam imefanya kweli katika kombe la shirikisho kwa kuifunga timu ngumu ya ES Setif kutoka algeria katika mechi ya awali iliyopigwa katika dimba kuu la Taifa jijini Dar es salaam kwa kuibuka na ushindi mnono wa bao 2-0.
Katika mchezo huo uliokuwa na upinzani mkali Waarabu walionekana kucheza mchezo wa kujihami huku wakifanya mashambulizi ya kushtukiza lakini ngome ya Simba iliyoongozwa na Kelvin Yondan sambamba na Nyosso wakisaidiwa vyema zaidi na beki za kushoto na kulia smbso ni Shomari Kapombe na Maftah na pale katika milingoti miwili alikuwepo Tanzania one Juma K Juma.
Katika mpambano huo uliohudhuriwa na mashabiki 41,000 na zaidi Mpaka mapumziko hakukuwa na timu iliyoweza kuliona lango la mwenzake.
Kosakosa langoni mwa Setif
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi zaidi hasa kwa timu ya Simba kana kwamba kocha alishawasoma Setif mchezo wao wa kutegea na kufanya mashambulizi ya kushtukiza kwa kucheza pasi fupifupi katika nusu yao na wanapofika nusu ya pili kuelekea langoni mwa Simba walikuwa wakipiga pasi ndefu.Simba kipindi hiki walikuja na kasi na kufanya mashambulizi mengi katika lango la Setif na tabu ililetwa langoni mwa Setif kwa juhudi kubwa za viungo waliocheza kwa ushirikiano mzuri kati ya Kazimoto,Machaku na Haruna Moshi"Boban" ambapo kwa kiasi kikubwa Simba wana kila sababu kujivunia beki ya kulia na kushoto yaani Maftah na Kapombe waliofanya kazi kubwa kupandisha mashambulizi mbele na hii ilileta nafuu kwa washambuliaji Okwi,Sunzu na Boban.
Felix Sunzu alitumika vizuri kuwaweka mabeki wa Setif katika wasiwasi na kujikuta wakimkaba kwa jihadi na kutoa mianya kwa Okwi na Boban kuleta mashambulizi langoni mwao.
Baada ya dakika 75 za ukame wa magoli ndipo jitihada za wachezaji wa Simba zilipozaa matunda wakati Mshambuliaji wa Kimataifa toka Uganda Emmanuel Okwi alipotupia kambani bao la kwanza na kuamsha shamrashamra kwa wapenzi wa Simba na hata wale wasio na mapenzi na Simba waliohudhuria katika dimba kuu la Taifa.

Mashabiki wa Yanga waliokuwa wakiibeza Simba lakini mwisho wa siku walitoka uwanjani na chupi yao mkononi na aibu tele
Goli la Okwi liliamsha morari kwa wachezaji wa Simba na Setif walioonekana kama wamezinduka toka usingizini na kuanza kusaka bao la kusawazisha lakini jitihada zao ziligonga mwamba pale Mshambuliaji mwingine wa Simba toka Zambia Felix Sunzu alipotupia kambani goli la pili katika dakika ya 80 baada ya kipa wa Setif kutema kombora la Machaku.
TIMU YA SOKA YA NOVA2010 YAFUNGWA 58-0
Timu ya Wheel Power F.C iliyoichapa Nova2010 58-0
Wakuu na wachezaji wa timu moja inayocheza soka ya mitaa au bustani, wanajitahidi kutathmini kilichotokea na kusababisha kinachoaminika kua kipigo kikubwa kuwahi kutokea katika mpira wa miguu katika historia ya Uingereza.
Klabu ijulikanayo kama Nova 2010 FC iliadhibiwa kwa kuchapwa 58-0 dhidi ya watani wa mji ule ule Wheel Power FC katika Ligi ya Torbay Sunday League huko Devon.Mambo yalianza mapema kwa Nova na kuendelea kuwa hivyo hata kufikia mapumziko ikiwa Nova imeisha bugia 20-0 kabla ya kipindi cha pili kushuhudia mengine 38.
Inaaminika kua ushindi wa Wheel power ndiyo mkubwa kuwahi kuandikwa, baada ya ushindi wa awali wa Timu ijulikanayo kama Illogan wa mabao 55-0 dhidi ya Madron FC mwezi novemba mwaka 2010
Mchezaji mmoja ka jina Lewis Parker, akiwa na umri wa miaka 60-anayeichezea Nova 2010, alisema kua wachezaji wengi hawakujitokeza kwa hio tulitarajia matokeo mabovu ingawa si kiasi hiki.
Nova ilipofika uwanjani bila wachezaji wake wa kawaida ndipo ikakusanya watu wengine watano na kutumia jumla ya wachezaji tisa pekee dhidi ya Timu inayoongoza Ligi hio ya Torbay.
Ndugu wawili Robbie mwenye umri wa miaka 27 na Bowker mwenye umri wa miaka 21 walifunga jumla ya mabao 28 ambapo Robbie alifunga 18 na Bowker kufunga 10.
Friday, March 23, 2012
SIMBA YAAHIDI KUWAANGAMIZA WAARABU
Timu ya soka ya Simba imewatoa hofu Watanzania kwa kuahidi kuvunja mwiko wa kufungwa na Waarabu kwa lengo la kulinda heshima ya soka la Tanzania hapo Jumapili watakapocheza dhidi ya ES Setif katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Wito huo umetolewa na washambuliaji Emmanuel Okwi, Uhuru Selemani na nahodha Juma Kaseja jana kabla ya kuelekea kwenye mazoezi yao ya jioni jana walipozungumzia malengo yao katika mchezo huo, huku wakidai kuwa timu za Waarabu zimekuwa zikiwasumbua mara kwa mara.
Wachezaji hao walisema Watanzania wanatakiwa kuwaamini kwa kuwa wako kikamilifu na wamejipanga kuweka historia ya kweli katika pambano hilo linalosubiriwa na mashabiki kwa hamu.
"Tunahitaji ushindi wa mabao zaidi ya moja hapa ili kujiwekea mazingira mazuri katika mchezo wa marudiano tutakapokuwa ugenini."
"Utakuwa mchezo mgumu, kwani mara nyingi tunapokutana na hizi timu za Waarabu wamekuwa wakitufunga, lakini sasa tunataka kuvunja mwiko huo wa kufungwa kila mara na kuhakikisha tunashinda kwa magoli mengi,"alisema Uhuru.
Naye kinara wa ufungaji wa Simba, mshambuliaji Okwi aliwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi na kuwashangilia kwa nguvu.
"Unajua kila mmoja anategemea ushindi na amejipanga kwa namna yake, tunawataka Watanzania watuombee ili tushinde na hatimaye tuiwakilishe nchi katika hatua nyingine ya mashindano haya," alisema Okwi kwa kujiamini.
Nahodha wa Simba, Kaseja alisema ushindi wa mapema ni muhimu kwao na watahakikisha wanatumia vyema kila nafasi wanayopata huku akiwataka wachezaji wote kuwa na ushirikiano wa kutosha miongoni mwao ambao utaongeza ari ya ushindi.
Naye mshambuliaji wa zamani wa Simba, Zamoyoni Mogella 'Golden Boy' aliwataka wachezaji wa Simba kufuata maelekezo yote watakayoambiwa na kocha wao Cirkovic Milovan.
"Wakifuata maelekezo ya kocha watacheza kwa kujiamini na kutumia vizuri nafasi watakazopata, kwani hili ndio tatizo kubwa ninaloliona kwa wachezaji wa Tanzania hivi sasa,"alisema Mogella.
Katika mazoezi ya jana jioni kocha Milovan alitumia muda wake mwingi kuwafundisha mabeki wake namna ya kuokoa mipira ya kona, krosi na mipira ya juu.
Heshima ya soka ya Algeria
Vinara wa ligi ya Algeria, Setif wenyewe wamejipanga kwa ajili ya kujenga heshima ya soka ya nchi yao.
Kocha Alain Geiger wakati wote Setif inapocheza lengo lake la kwanza ni ushindi sio kitu kingine, ni kitu kilichoeleweka kwa wachezaji wake wote na hivyo wajibu wa wachezaji wake ni kuthibitisha ubora wao uwanjani.
Setif hawategemei kuingia uwanjani na kukaa nyuma kujilinda kwa kusubiri mashambulizi ya wapinzani wao kwa sababu silaha kubwa ya soka ya Algeria ni kushambulia kwa haraka.
Geiger anapendelea timu kujilinda kwa kukaa na mpira iwe kwa kushambulia kwa kasi au pasi fupi fupi na kwenda mbele kwa lengo ya kuichanganya ngome ya timu pinzani na kupata ushindi bila ya kuruhusu goli la kufungwa.
Mashabiki watulivu
Nyota wa Setif, Delhoum amesifia tabia ya ukarimu wa mashabiki wa Tanzania, kitu kinachotoa faraja kwao katika mchezo huo.
"Mashabiki wa Tanzania hawana matendo mabaya kwa timu za kigeni wanajulikana kwa utulivu wao na tabia yao nzuri ya uanamichezo," alisema Delhoum aliyecheza katika mechi kati ya Algeria dhidi Taifa Stars mwaka jana.

Thursday, March 22, 2012
ARSENAL YAICHAPA EVERTON,VERMAELEN NI NOUMER!
Arteta na Van Pesie wakishangilia goli lililofungwa na Vermaelen(5)
Theo Walcott akipunguzwa makali na Leighton Baines wa Everton
Timu ya soka ya Arsenal jana tarehe 21 machi 2012 waliutumia vizuri uwanja wake wa Emirates uliopo jijini London kwa kuichabanga Everton bao moja kwa ubuyu(1-0).
Katika meshi hiyo ndani ya dimba la Emirates ilihudhuriwa na watu 30,330 na mchezo huo ulichezeshwa na Mason.
Arsenal ambao wanaonekana kuwa fit kwa kila mechi kipindi hiki walicheza soka la kuvutia kama kawaida yao na sio mwingine aliepeleka msiba Everton bali ni Beki anaeongoza kwa kutupia kambani Thomas Vermaelen aliposukumiza mpira wa kichwa wavuni katika dakika ya 7 ya mchezo.
Mpaka mapumziko Arsenal walitoka kifua mbele kwa goli moja la kuongoza,Kipindi cha pili kilianza kwa soka la kuvutia huku Gunners wakijaribu kuongeza bao na Everton nao wakifanya jitihada kutafuta bao japo la kufutia machozi bila mafanikio.
Japo washambuliaji wa Arsenal kama Ramsey,Rosicky na Van Persie walijaribu kuchafua hali ya hewa golini mwa Everton lakini ngome ya Everton iliyoongozwa na Baines akisaidiana na Heitinga na Distin ilikaa vyema na mpaka dakika 90 zinakamilika Arsenal ndiyo iliyoibuka mshindi.
Timu:
ARSENAL; Szczesny, Sagna, Vermaelen, Koscielny, Gibbs, Walcott, Arteta, Song, Ramsey, Rosicky, van Persie
EVERTON; Howard, Hibbert, Heitinga, Distin, Baines, Pienaar, Fellaini, Osman, Drenthe, Cahill, Jelavic.
MANCHESTER CITY YAIBOFOA CHELSEA 2-1
Golikipa wa Man City Joe Hart akichumpa bila mafanikio kuokoa mpira uliopigwa na Garry Cahill ukielekea kambani.
Aguero akitupia kambani kwa mkwaju wa penati na kuisawazishia Man City
Nasri akitupia kambani na kuandika bao la pili na la ushindi kwa Man City,Cech hoooooi
Manchester City imeendeleza kampeni zake za kuusaka ubingwa wa Ligi kuu ya Uingereza pale ilipoichabanga timu ngumu ya Chelsea kwa kamba 2-1 mchezo uliopigwa katika dimba la Etihad jijini Manchester.Mchezo ulipigwa jana tarehe 21 march 2012 ukichezeshwa na refa mahiri Dean.
MAN C 2-1 CHELSEA
Katika kipute hiko iliwachukua takriban dakika 60 mashabiki waliohudhuria mtanange huo kushangilia bao na bao hilo likitiwa kambani na Garry Cahill na kuifanya Chelsea kuongoza mchezo huo uliokuwa wa kawaida tofauti na ulivyotegemewa na wengi.Mbwembwe za mashabiki na wachezaji wa Chelsea za kuongoza zilikomeshwa katika dakika ya 78 pale refa Dean alipoizawadia mkwaju wa penati Man City na bila ajizi wala kokoro mkwaju huo ulitiwa kambani na Sergio Aguero na kubadilisha taswira ya mchezo na kusomeka 1-1.
Zikiwa zimesalia dakika 5 ili kila mshabiki alielipia mechi hiyo kuhesabu maumivu kwa kuona mchezo wa sare Vijana wa Manchini walikaza na kufanikiwa kuwanyanyua vitini mashabiki wa Man City huku wakiwaonesha milango ya kuondokea wale wa Chelsea, kwa goli kali na la kuvutia lililotupiwa kambani na Mshambuliaji mzuri wa sura na uchezaji Samir Nasri katika dakika ya 85.
Bao hilo la Nasri lilionekana kuwachanganya Chelsea hasa kocha wao wa kuunga unga De Matteo na kushindwa kukaa kwenye benchi akiwahimiza kina Drogba kufanya mambo bila mafanikio yeyote na mpaka dakika 90 zinakwisha ni Man City ndio walioibuka kidedea na kuwaacha Chelsea walikwa wamelowa ndembendembe kama laki si pesa.
Vikosi vilikuwa hivi;
MAN CITY; Hart, Zabaleta, Richards, Toure, Clichy, Silva, Toure Yaya, De Jong, Nasri, Aguero, Balotelli
CHELSEA; Cech, Ivanovic, Luiz, Cahill, Cole, Mikel, Meireles, Ramires, Lampard, Mata, Torres
Subscribe to:
Posts (Atom)