Bousquets akifunga goli la kwanza la Barca
Klabu ya soka ya Chelsea ya Uingereza imefanikiwa kutinga fainali
ya klabu bingwa barani Ulaya, licha ya nahodha John Terry kulimwa kadi
nyekundu.
Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya 2-2, lakini Chelsea ikapata ushindi
wa jumla ya magoli 3-2.
Andre Iniesta akitupia kambani goli la pili kwa Barca
Timu ya The Blues (Chelsea) ilionekana kuelemewa baada ya Sergio Busquets na
Andres Iniesta kuiwezesha Barca kuongoza katika mchezo huo.
Lakini Ramires kwa umakridadi alifanikiwa kuichomoka ngome ya Barca na kutupia kambani bao safi la
Chelsea kwa staili ya ku-chop katika mechi hiyo.
Ramires na golikipa Valdes wakishuhudia mpira uliopigwa na Ramires ukitinga wavuni
Barca walipata penalty, lakini Lionel Messi, licha ya maarifa yake na sifa
nyingi katika ufundi wa penalty, lakini mkwaju huo ukagonga mwamba.
Messi akipiga penati iliyogonga mwamba
Muda wa majeruhi wa dakika tatu za nyongeza, Fernando Torres
alionyesha utulivu wa hali ya juu sio tu kwa kushambulia ngome ya Barca ambayo
kwa muda mrefu ilikuwa haiguswi, lakini vile vile kwa kumchenga hata kipa Valdes
na kuukwamisha mpira wavuni kwa makini.
Mapema wiki hii, Torres alikuwa amenukuliwa akisema “sio siku zote timu bora
hupata ushindi”, matamshi ambayo ni ndoto iliyotimia.
Torreeeeeees akimlamba chenga Valdes na kutupia kamba ya pili kwa Chelsea
Sasa vijana wa Chelsea wa Roberto di Matteo wanasubiri kufahamu kama
watacheza na timu ya kocha wao wa zamani, Jose Mourinho, akiwa mkufunzi wa Real
Madrid, au pengine watakutana na Bayern Munich, ambao uwanja wao ndio
utakaotumiwa kuandaa fainali ya ligi ya klabu bingwa.
Nahodha John Terry akilimwa kadi nyekundu baada ya kumpiga teke Alexis Sanchez
Wachezaji wa Chelsea wakishangilia ushindi wa kutinga fainali baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa.
Drogba akimpoza machungu Leonel Messi
Real Madrid na Bayern zinapambana Leo, tarehe 25 Aprili 2012.
Tatizo la Chelsea ni kwamba katika fainali ya Jumamosi tarehe 19 Mei, sasa
watazikosa huduma za nahodha John Terry, Ramires, Branislav Ivanovic na Raul
Meireles mjini Munich, kutokana na kuadhibiwa kwa kucheza mchezo wa kuumizana
katika nusu fainali.