|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Wednesday, May 2, 2012
Tuesday, May 1, 2012
Vicent Company akitupia goli la pekee na la ushindi lililoisambaza Man United
Nimeuaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Tuliaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Weweeeeeee pumbafuuuuuuu
Man City imeichakaza man united bao moja kwa nunge na kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza, goli la pekee lilifungwa na Vicent Company dakika ya fulani.
AZAM YAILAMBA TOTO
Patashika nguo kuchanika katika mpambano huo
AZAM imeendeleza wimbi lake la kusaka ubingwa msimu huu baada ya kuichakaza Toto African kwa mabao 3-1 kwenye uwanja Azam Complex Chamazi.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Kipre Tchetche alifunga mabao mawili na kumtegeneza la tatu kwa John Boko kabla ya Enyinna Darlington kuifungia Toto bao la kufutia machozi dakika 88.
Kwa ushindi huo Azam sasa imefikisha pointi 56 ikiwa nyuma ya Simba kwa pointi 3 kabla ya mechi ya mwisho zitakazoamua bingwa kwa tofauti ya mabao kama vinara Simba watafungwa na Yanga na Azam watainyuka Kagera Sugar kwa mabao zaidi ya matatu.
Azam waliingia kwenye mchezo huo na kasi na kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 10 kupitia kwa Kipre Tchetche akiunganisha kwa kichwa krosi ya Ibrahim Mwaipopo.
Tchetche alifunga bao la pili dakika tisa baadaye akimalizia mpira ulioshindwa kuokolewa na mabeki wa Toto African wakati wakizuia shuti la John Boko.
Kinara wa ufungaji katika ligi msimu huu Boko alipachika bao la tatu akimalizia kazi nzuri ya Tchetche dakika ya 37.
Mabao hayo ya haraka yaliwavunja nguvu mashabiki wanadhaniwa wa Simba waliokodi Daladala na kujitokeza kwa wingi uwanjani hapo kwa lengo la kuishangilia Toto.
Baada ya bao la tatu kocha wa Toto msaidizi Salemain Kigi aliyechukua nafasi ya kocha mkuu Athuman Bilali, alimpumzisha kipa Mustapha Mabrouk na kumwingiza Sunga Ramadhani.
Kocha Bilali anatumikia adhabu ya kadi nyekundu alionyeshwa wakati wa mechi yao dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko Toto walikuwa wamefika golini kwa Azam mara moja tu kwenye mchezo huo uliokuwa wa upande moja.
Mwamuzi wa mchezo huo alitoa kadi za njano kwa Mrisho Ngasa wa Azam na Ladisraus Mbogo, Emmanuel Swita kwa Toto African.
Uwanja ulifungwa vipaza sauti kila kona na kufunguliwa muziki mkubwa aina ya mchiriki uliokuwa ukiimbwa na kuchezwa na mashabiki wa Azam muda wote wa mchezo.
Kipindi cha pili Toto ilimpumzisha Swita na kuingiaPhabian James huku Azam wakimtoa Mwaipopo na kuingia Abdi Kassim.
Mabadiliko hayo yalikuwa na faida kwa Toto walirudi mchezoni na kufanya mashambulizi mengi langoni kwa Azam walionyesha kulidhika na mabao yao matatu.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria, Enyinna Darlington alifungia Toto bao la kufutia machozi dakika ya 88 kwa shuti la umbali wa mita 30, lililokwenda moja kwa moja wavuni.
Mwisho wa mchezo huo kocha wa Toto, Bilali aliangua kilio kudai kujumiwa na kusababisha kufungwa kwao.
Huku wachezaji wa Toto wakitaka kuwapiga viongozi wao pamoja na kipa Mustapha Mabrouk wakiwashutumu kuhusika na kipigo hicho
Monday, April 30, 2012
SIMBA S.C.....WE ACHA 2!! YAIBANJUA AL AHLY SHANDY 3-0
Timu ya Simba maarufu kama watoto wa Msimbazi ya jijini Dar es Salaam wameendeleza kipigo dhidi ya timu za kigeni safari hii timu ya Al Ahly Shandy ya Sudan imepata kichapo kingine kwa kubanjuliwa mabao 3-0 katika mpambano mkali wa kuvutia uliojaza wapenzi wa soka uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam kwenye mechi ya kuwania ubingwa wa kombe la shirikisho la klabu za Afrika.
Emmanuel Okwi akijaribu kuipenya ngome ya Al Ahly Shandy ya Sudan
Umati wa mashabiki wa soka waliohudhuria walilipuka kwa shangwe pale mshambiliaji Haruna Moshi"Boban" alipotupia kambani balo la kwanza baada ya kazi nzuri iliyofanywa na mshambuliaji mwenzake Uhuru selamani.
Bao la pili lilifungwa na mshambuliaji Patrick Mafisango"Mutesa" ambaye alikosesha timu yake bao kwa njia ya penati baada ya kupiga mpira penati mbofumbofu iliyodakwa na Mlinda Mlango wa Al Ahly Shandy.
Wachezaji wa Simba wakishangilia bao la pili lililofungwa na Mafisango
Bao safi lililofungwa na Mshambulaiji kutoka Uganda, Emmanuel Okwi liliwainua watazamaji wote uwanjani kwani bao hilo lilikuwa la kifundi sana na kuifanya timu ya Simba kuibuka kifua mbele kwa mabao 3-0 dhidi ya Al Ahly Shandy ya Sudan.
Mabao yote yalifungwa katika kipindi pili cha mchezo huo ambao ulijaa shauku kubwa kutoka kwa wanachama wa timu ya simba ambayo imeingia 16 bora katika kombe la shirikisho la klabu za Afrika.
Kocha wa Simba Milovan akishangilia pamoja na wachezaji wake
Umati wa Mashabiki wa Simba wakishangilia kwa mbwembwe
Simba na Al Ahly Shandy ya Sudan zitachauana tena Mei 11 mwaka huu katika mchezo wa marudiano wa michuano ya kombe la shirikisho la klabu za Afrika.
Friday, April 27, 2012
GUARDIOLA KUBWAGA MANYANGA BARCELONA
Pep Guardiola kocha anayetazamiwa kubwaga mikoba ya kuinoa Barcelona
Kocha wa mabingwa wa Ulaya Barcelona ambao hivi karibuni walitupwa nje katika kinyang'anyiro cha kutetea ubingwa wa klabu bingwa ya Ulaya na Chelsea, Pep Guardiola atabwaga manyanga mwishoni mwa msimu huu baada ya kufikia uamuzi wa kutoongeza mkataba wake na Klabu hiyo ya Barcelona katika ligi kuu ya Uhispania.
Rais wa Barcelona Sandro Rosell aliliambia shirika moja la Habari kuwa msimu huu ndio wa mwisho Guardiola kukinoa kikosi cha Barcelona baada ya kukataa kuongeza mkataba wake ambao unamalizika mwishoni mwa msimu huu.
Rais huyo alimshukuru Guardiola kwa kusema"Thank you for your work and your love,"
akimaanisha akhsante kwa kazi yako na upendo wako.
Subscribe to:
Posts (Atom)