Wednesday, April 17, 2013
Friday, April 12, 2013
RATIBA NUSU FAINALI UEFA 2013
SF 1
v
SF 2
v
Wednesday, April 3, 2013
BALAA LA KHANGA MOKO HILI HAPA
Balaa linaanza mtu anamwagiwa Kinywaji kwenye makalio ooo maaamaaa
Sasa ni ndembendembe

Balaa hilo mie simoooo
Twende kazi..asie na mwana aeleke jiwe
PSG YAIKOMALIA BARCELONA, BAYERN YAITUNGUA JUVENTUS
Messi akitupia kambani goli la kwanza Katika dakika ya 37 kabla Zlatan Ibrahimovic hajaisawazishia PSG katika dk 78. Na Barcelona waliongeza bao la pili likitupiwa kambani na Xavi kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 88 lakini PSG walikomaa na kusawazisha katika dakika ya 90 bao la nduki kali ya Matuidi. Mpambano huo ulihudhuriwa na mashabiki wapatao 45,000.
Ibrahimovic akishangilia goli la kwanza la kusawazisha
Iniesta chini ya ulinzi mkali
Goli la pili na la kusawazisha la PSG likitinga wavuni
Mfungaji wa goli la kusawazisha la PSG Matuidi akishangilia
Messi na Beckham shughuli pevu
Messi baada ya kuumia akijiandaa kutoka nje
PSG 2-2 BARCELONA
Katika robo fainali nyingine ya kwanza timu ngumu ya Ujerumani Bayern Munich waliiadabisha Bibi kizee wa Turin,Juventus kwa bao 2-0. Goli la kwanza likifungwa na Alaba dakika ya 0, Na sio mwingine alietupia msumari wa pili bali ni Thomas Muller katika dakika ya 62.
Nimetupiaaa..Alba akishangilia baada ya kufunga goli la mapema mno katika dakika ya 0.
Robben chini ya ulinzi
BAYERN 2-0 JUVENTUS
Tuesday, April 2, 2013
CHELSEA YAIPIGA MAN UNITED CHA NGURUWE KOMBE LA FA
Timu ya soka ya Chelsea imeisambaratisha timu ngumu ya Man united katika kombe la chama cha soka cha Uingereza FA kwa bao moja kwa nunge katika dimba la Stamford Bridge, ukiwa ni mchezo wa marudiano baada ya mchezo wa kwanza uliopigwa katika dimba la Old Trafford kuisha kwa matokeo ya sare ya 2-2.

Demba BA akifunga goli pekee
Katika mchezo huo uliohudhuriwa na watazamaji wapatao 40,704 walishuhudia mtanange wa kukata na shoka. Wenyeji walionja tamu ya mtanange huo pale Mshambuliaji raia wa Senegal Demba BA alipofunga goli maridadi baada ya kutanguliziwa pande murua na Juan Mata katika dakika ya 48 ya mtanange huo. Goli hilo lilidumu mpaka mtanange unamalizika na hivyo Man United kuondoshwa katika michuano hiyo ya FA na kuiacha Chelsea kusonga mbele.

Wachezaji wa Chelsea wakimpongeza Demba BA baada ya kuitengeneza Man United

Danny Welbeck akijaribu kumtoka Oscar
Demba BA akifunga goli pekee
Katika mchezo huo uliohudhuriwa na watazamaji wapatao 40,704 walishuhudia mtanange wa kukata na shoka. Wenyeji walionja tamu ya mtanange huo pale Mshambuliaji raia wa Senegal Demba BA alipofunga goli maridadi baada ya kutanguliziwa pande murua na Juan Mata katika dakika ya 48 ya mtanange huo. Goli hilo lilidumu mpaka mtanange unamalizika na hivyo Man United kuondoshwa katika michuano hiyo ya FA na kuiacha Chelsea kusonga mbele.
Wachezaji wa Chelsea wakimpongeza Demba BA baada ya kuitengeneza Man United
Danny Welbeck akijaribu kumtoka Oscar
Chelsea 1-0 Man United
Thursday, March 28, 2013
UEFA WAMFUTIA ADHABU IBRAHIMOVIC KUIVAA BARCELONA
Zlatan Ibrahimovic
Kamati ya nidhamu ya UEFA imemfutia adhabu mshambuliaji mahiri wa Paris Saint German Zlatan Ibrahimovic huku akiwa tayari ametuikia kwa kukosa mechi moja dhidi ya Valencia.
Kutokana na kufutiwa adhabu hiyo sasa atakuwemo kwenye kikosi cha PSG kitakachoivaa Barcelona katika mchezo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya wiki ijayo.
MANDELA HALI TETE ARUDISHWA HOSPITALI
Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amelazwa tena hospitalini baada ya kuugua ugonjwa wa mapafu kwa mara nyingine.
Taarifa kutoka kwa serikali ya nchi hiyo,
ilisema kuwa Mandela mwenye umri wa miaka 94 alilazwa hospitalini muda
mfupi kabla ya saa sita usiku.Nelson Mandela
Mandela alilazwa siku kumi na nane hospitalini mwezi Disemba mwaka jana kupokea matibabu ya ugonjwa wa mapafu na kibofu.
Anasifika sana kama baba wa taifa hilo kwa kuongoza vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi.
Kadhalika Mandela alihudumu kama rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini tangu mwaka 1994 hadi mwaka 1999, ingawa hali yake ya kiafya imezua wasiwasi kwa muda sasa.
Rais Jacob Zuma alimtumia taarifa ya kumpa pole na kumtakia kupona Mandela
"tunawataka watu wa Afrika Kusini pamoja na duniani kote kuwa watulivu na kumuombea Madiba na familia yake. Tuna imani kuwa kikosi cha madaktari wanaomtibu Mandela watafanya kila hali kuhakikisha anapona,'' alisema Zuma katika taarifa yake.
Mapema mwezi huu bwana Mandela alilazwa hospitalini mjini Pretoria baada ya kufanyiwa ukaguzi wa kiafya.
Subscribe to:
Posts (Atom)