Friday, February 21, 2014

MATOKEO KIDATO CHA NNE (CSSE 2013)

Tuesday, February 18, 2014

VIDEO YA LEO-NAY WA MITEGO (NAKULA UJANA)

 
Ney Wa Mitego-Nakula ujana

LIGI YA MABINGWA MAN CITY DOMONI MWA BARCELONA



Timu ya Manchester City itakutana na timu ya Barcelona siku ya leo, Tarehe 18/02/2014 katika kombe la klabu bingwa ulaya katika uwanja wa Etihad Stadium, mtanange huo utakawakutanisha wababe hao wa soka utakua katika sura mpya kwenye historia ya soka la dunia kwani itakuwa ni mara ya kwanza kwa timu hizo kukutana.

Manchester City itamkosa mshambuliaji wake mahiri Sergio Aguero ambaye yupo majeruhi;hivyo kocha Manuel Pellegrini bado ana washambuliaji wakutosha kama Dzeko, Negredo na Jovetic wakati huo huo Barcelona itawakilishwa na nyota wake kama Lionel Messi na Neymar Jr katika mtanange huo wa kugombania kombe la mabingwa ulaya katika hatua ya 16 bora siku ya leo.
city_new_45457.jpg
RATIBA | UEFA Champions League

Leo - Jumanne 18 February 2014
22:45 Manchester City vs Barcelona
22:45 Bayer Leverkusen vs PSG


Kesho - Jumatano 19 February 2014
22:45 Arsenal vs Bayern München
22:45 Milan vs Atlético Madrid

Wednesday, February 12, 2014

NI ARSENAL Vs MAN UNITED...HATUMWI MTOTO SIGARA

 

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, anatarajiwa kuwa nyota wake aliyesajiliwa kwa kitita cha pauni milioni 42, atarejea katika hali yake ya kawaida na kuonyesha mchezo mzuri, baada ya matokeo mabaya wikendi iliyopita.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, kutoka Ujerumani,Metsut Ozil hajatupia kambani katika mechi nane zilizopita huku akiwa amechangia kupatikana kwa magoli mawili pekee katika mechi hizo.
 
Metsut Ozil

 
Lucas Podolski
 
Ozil, ambaye alijiunga na Arsenal, kutoka kwa klabu ya Real Madrid Septemba mwaka uliopita, alianza vyema kwa kufunga magoli manne na kuchangia magoli sita katika mechi zake kwanza kumi na mbili za ligi kuu.
Lakini mcheza kiungo huyo, alishutumiwa vikali kufuatia mchezo aliouonesha wakati Arsenal ilipovurugwa magoli 5-1 na Liverpool, hali iliyomlazimu Wenger kumuondoa kunako dakika ya sitini na moja.
Akiongea kabla ya mechi yao katika Uwanja wa Emirates siku ya Jumatano usiku, Wenger alisema kuwa anadhani David Moyes anaweza kufanikiwa kama kocha wa United ikiwa atapewa muda.
 
Van Persie

Wayne Rooney

Julai mwaka uliopita, Moyes aliteuliwa kuchukua mahala na Sir Alex Ferguson ambaye alistaafu kama kocha wa Manchester United baada ya kushinda ligi kuu ya Premier mara 13 katika kipindi cha miaka 27, lakini amekuwa na kibarua kigumu kufuata nyayo za Ferguson.
Manchester United inashikilia nafasi ya saba kwenye msururu wa ligi kuu na alama 41 na hata ikishinda mechi yake dhidi ya Arsenal, Vijana hao wa Moyes watasalia katika nafasi hiyo hiyo.

Tuesday, February 4, 2014

HUU NDIO MSIMAMO LIGI KUU UINGEREZA BAADA YA MECHI YA JANA

CHELSEA YAITULIZA MASHETANI MAN CITY

 
 
Ivanovic akitupia kambani bao la pekee.
  
Muuaji Ivanovic akishangilia goli la pekee dhidi ya Man City

Manchester City imevutwa shati na Chelsea kwa kucharazwa bao 1-0 katika uwanja wao wa nyumbani. kabla ya mechi hiyo Man City ilikuwa imeshinda mechi zote 11 ilizokuwa imecheza katika dimba la nyumbani Ettihad Stadium kabla ya kukutana na Chelsea.
Mtanange huo umeweka historia mpya kwa mara ya kwanza kwa Manchester City kushindwa kufunga bao katika mechi za nyumbani tangu mwaka 2010.
Bao la Chelsea lilifungwa na Branislav Ivanovic katika kipindi cha kwanza .
Kutokana na matokeo hayo Manchester City na Chelsea zinalingana pointi lakini Man City imetupia kambani mabao mengi.
Liverpool iko katika nafasi ya nne, Everton ni ya tano ilhali Tottenham ni ya sita huku Manchester United ikishikilia nafasi ya saba.
 
Kwangu mimi huyu dogo,Hazard ndio alikuwa "Man of the Match"


Hali tete Wachezaji wa Man City ''wameshavurugwa"


Hii ndio hali ilivyokuwa baada ya kukosakosa magoli


Hii ni hali na vituko vya Mourinho pale alipohisi mwamuzi hatendi haki

 
TAZAMA VIDEO YA MPAMBANO HUO