Thursday, November 6, 2014
Friday, October 31, 2014
RAIS WA BURKINA FASO APIGWA CHINI
Rais alieenguliwa madarakani nchini Burkina Faso, Campaore
Msemaji wa jeshi amewaambia waandishi wa habari mjini Ouagadougou kuwa bwana Compaore hayuko mamlakani tena.
Rais Compaore alikuwa ametangaza kuwa atajiuzulu baada ya kipindi cha serikali ya mpwito ya mwaka mmoja .
Lakini wanasiasa wa upinzani wakakataa kata kat kuendelea kwa utawala wake na wakamtaka ajiuzulu maramoja.
Rais Compaore alikuwa ameongoza kwa zaidi ya miaka 27 tayari.
Kumeripotiwa maandamano mapya nchini Burkina Faso ya kutaka kujiuzulu mara moja kwa rais wa nchi hiyo Blaise Compaore.
Viongozi wa upinzani wanakutana kwenye mkji mkuu Ouagadougou kukubaliana kwa pamoja hatua watakazochukua.
Siku ya Alhamisi waandanamaji walikarisishwa na jitihada za rais za kuongeza kipindi chake chake miaka 27 madarakani na wakateketeza bunge na kusaka kituo cha runinga cha serikali.
Bwana Compaore alitupilia mbali jitihada za kubadilisha katiba ambayo ingemruhusu kuwania tena muhula mwingine kama rais lakini akasema kuwa atabaki madarakani kwa mwaka moja zaidi .
<span >Viongozi wa Upinzani Nchini Burkina Faso wamewaomba waandamanaji kutolegeza kamba bali kuendelea na maandamano huku wakimtaka Rais Blaise Campaore ang'atuke mamlakani mara moja.
Licha ya Rais Compaore wa Burkina Faso kuhutubia taifa siku moja baada ya vurugu kubwa na kutangaza kuvunja serikali waandamanaji hawataki kusikia kwamba apewe muda wa mwaka mmoja ndipo aondoke madarakani.
Jana jioni kiongozi wa Jeshi Jeneral Honore Traore alitangaza kuundwa kwa serikali ya mpito itakayodumu kwa kipindi cha mwaka mmoja japo hakusema itaongozwa na nani.
Wananchi wa Burkina Faso wakiwa katika maandamano
Monday, October 27, 2014
NAHODHA WA BAFANABAFANA AUAWA KWA RISASI
Senzo Meyiwa enzi za uhai wake
Nahodha ambaye pia ni golikipa wa
timu ya soka ya taifa la Afrika kusini Senzo Meyiwa amefariki dunia
baada ya kupigwa risasi. Jeshi la polisi la nchi hiyo limesema.
Tukio hilo limeripotiwa kutokea katika nyumba ya mpenzi wake iliyopo katika mji wa Vosloorus kusini mwa Johannesburg.Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aliichezea klabu ya Orlando Pirates na alicheza mechi nne zilizopita za timu yake ya taifa katika mechi za kufuzu za fainali ya mataifa ya Afrika.
Jumamosi alikuwepo katika tukio la timu yake pindi waliposonga mbele katika nusu fainali ya ligi ya Afrika kusini.
Katika maelezo yake Jeshi la polisi la afrika kusini limesema kwamba Meyiwa ameripotiwa kufariki wakati akiwasili hospitalini.
Senzo enzi za uhai wake akifanya vitu uwanjani
Marehemu Senzo akinyaka mpira Bafanabafana ilipoumana na Nigeria
MAN UTD YAIVIMBIA CHELSEA ZATOKA SARE
Haikuchukua muda mwingi punde tu baada ya kuanza kwa kipute hicho, mchezaji mkongwe Didier Drogba akawainua mashabiki wa Chelsea baad ya kufunga goli zuri la kichwa.
Goli hili liliweza kudumu hadi dakika za nyongeza za mchezo huo na kuwapa matumaini mashabiki wa timu hiyo kuamini kuwa wangekusanya point zote tatu kutoka kwa Man U.
Dakika ya 93 ya mchezo Mholanzi Robin van Persie akawainua mashabiki wa timu yake pamoja na kocha wake Louis van Gaal baada ya kuisawazishia timu yake kwa shuti kali la guu la kushoto na kufanya matokeo kuwa ni sare ya 1-1 mpaka kipyenga cha mwisho.
Baada ya kupata goli la dakika za lala salama Kocha Louis Van Gaal hajafurahishwa na timu yake ya Manchester United japokuwa vijana hao wa Old Trafford wameweza kuondoka na point moja muhimu katika mchezo dhidi ya Chelsea uliochezwa katika dimba la Old Trafford. '' hatujatumia faida ya kuwa nyumbani na tungeweza kushinda mchezo huu'' alisema Mholanzi huyo.
Goli la kichwa la Didier Drogba liliisaidia Chelsea kushika usukani katika mchezo huo kabla ya Robin van Persie kusawazisha na kuwasaidia vijana
Didier Drogba akitupia kambani kwa kichwa goli la kuongoza
Drogba akishangilia
Niacheni jamaniii hapa kazi tuuu
Di Maria akimhadaa Willian
Van Persie akitupia goli la kusawazisha
Wachezaji wa Man Utd wakishangilia goli ka kusawazisha dhidi ya Chelsea
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho akisalimiana na kocha wa Man Utd Van Gaal
MAN UTD 1-1 CHELSEA
Thursday, October 23, 2014
KLABU BINGWA ULAYA ARSENAL, REAL MADRID ZAKANYAGAKANYAGA
Anderlecht akitupia goli la kwanza
Podolski akishangilia goli la ushindi
Katika ligi ya mabingwa barani Ulaya
Liverpool imechabangwa nyumbani Anfield kwa mabao 3-0 kutoka kwa Real
Madrid huku Mario Balotelli akiingia lawamani
Meneja wa mchezaji
huyo mtukutu, Brendan Rodgers amemlaumu mshambuliaji huyo kwa kitendo
chake cha kubadilishana Jezi na Pepe mara tu baada ya dakika 45 za
kwanza.Baadhi ya mashabiki wa jijini Dar es Salaam,Tanzania wamemtupia lawama mchezaji huyo ambaye pamoja na kununuliwa kwa pauni milioni 16 ameifungia Liverpool goli moja tu msimu huu.
Wakati huo huo Arsenal wamepata ushindi wa dakika za mwisho wa 2-1 baada ya Anderletch kuwakimbiza mchakamchaka kwa muda mrefu.
Mara baada ya mchezo huo nimezungumza na shabiki wa Arsenal ambaye anasema pamoja na ushindi walioupata lakini kuna haja ya Arsene Wenger kubadillika
Matokeo mengine ni Atletico Madrid wameifumua Malmo 5-0 na Olimpiakos imeichapa Juventus bao 1-0
Kwa upande wa michuano ya Uropa Ligi, leo Tottenham inakipiga na Asteras Tripolis, Inter Millan inakutana na St Etienne, Lille itamenyana na Evaton, wakati ambapo Viareale watacheza na FC Zurich
C.Ronaldo akishangilia baada ya kutupia goli la kwanza
Wachezaji wa Madrid wakimpongeza Benzema bada ya kutupia kambani bao la pili
Chukua hiyooooooooooo
ANDERLECHT 1-2 ARSENAL
LIVERPOOL 0-3 REAL MADRID
Monday, October 6, 2014
CHELSEA YAWAADABISHA WATOTO WA WENGER, MOURINHO NA WENGER WAKUNJANA
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger
Katika ligi kuu ya England jana
mamilioni ya wapenda soka duniani waliokuwa wakishuhudia mtanange kati
ya Chelsea na Arsenal walishuhudia Chelsea wakiibuka kidedea kwa jumla
ya mabao 2-0 yakifungwa na Eden Hazard katika dakika ya 27 kwa njia ya
penalti na dakika ya 78 likifungwa na Diego Costa mwenye magoli tisa
katika mechi saba alizocheza katika ligi kuu hiyo ya primier.
Pamoja
na mchuano uwanjani hapo lakini nao makocha wa timu hizo Jose Mourinho
wa Chelsea na Arsene Wenger wa Arsenal walitifuana baada ya Wenger
kulalamikia mchezo mbaya wa Cahil dhidi ya Sanchez.Chelsea imejiimarisha kileleni kwa pointi tano juu ya Mancity inayofuatia ikiwa na pointi 14, huku Southampton akishikilia nafasi ya tatu baada ya timu zote za ligi kuu ya England kucheza mechi saba kila moja.
Kipigo cha jana cha Arsenal ni cha 12 kutoka kwa Chelsea ikiwa chini ya Mourinho dhidi ya Arsene Wenger. Mechi nyingine zilikuwa kati ya Manchester United dhidi ya Everton, ambapo Man-U imejipatia ushindi wa magoli 2-1. Tottenham imeicharaza Southampton kwa goli 1-0. Nayo Manchester City imetakata kwa kuichapa Aston Villa mabao 2-0. Msimamo wa ligi hiyo katika michezo saba, Chelsea inaongoza ikiwa na pointi 19, ikifuatiwa na Manchester City yenye pointi 14, Southmpton ni ya tatu na pointi 13, Manchester United nafasi ya 4 sawa na Swansea zikitofautiana idadi ya magoli ya kufunga. QPR, Burnely na Newcastle ndizo tatu za mwisho zikiwa na pointi 4 kila moja.
Diego Costa akishangilia baada ya kuidungua Arsenal
Welbeck Vs Fabregas
Diego Costa akitupia kambani goli la pili
Ozil Vs Fabregas
Wenger na Moueinho nusura wazichape kavukavuu
Tazama magoli yote hapa
WENGER AFUNGUKA DIEGO COSTA NI SHEEEEEDAAA!
DIEGO COSTA
ARSENE WENGER
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger
amesema kuwa Diego Costa ni mshambuliaji hatari na kwamba mshambuliaji
huyo wa Chelsea ni tishio kubwa kwa kikosi chake katika mechi ya Leo
itakayochezwa katika uga wa stamford Bridge.
Kilabu zote mbili hazijafungwa tangu msimu huu wa ligi uanze,lakini Chelsea iko juu ya Arsenal kwa pointi sita.Costa aliyenunuliwa kwa kitita cha pauni millioni 32 kutoka kilabu ya Uhispania ya Atletico Madrid,amefunga mabao 8 katika mechi 6 za ligi ya Uingereza alizoshiriki.
''Costa ana kila kitu cha mshambuliaji,anajitolea na yuko tayari kufunga bao'',alisema Wenger.
Wenger anahisi matumaini kwamba huenda Arsenal ikaishangaza Chelsea ilio katika kilele cha jedwali la ligi ya Uingereza ikiwa na pointi 16 kati ya 18.
Msimu uliopita Arsenal ilipata kichapo cha mabao 6 kwa 0 katika mechi iliochezwa katika uga wa Stanford Bridge huku Wenger akiweka rekodi ya kuisimamia kilabu hiyo kwa mechi yake ya1000.
Kwa upande wake Mourinho anatarajia ushindani mkali kutoka kwa Arsenal na amejitayarisha vilivyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)