Monday, June 6, 2011

TANZANIA UMASIKINI UNATOKA WAPI?

Watanzania kadri siku zinavyozidi hali ya maisha inazidi kuwa tete,wakati hilo linatokea wanasiasa wanatuhubiria kuwa uchumi wa nchi unakua, nashindwa kuelewa uchumi unakua hali ya maisha inazidi kuwa ngumu kivipi?

     Mgodi wa Ashanti uliopo katika migodi ya Geita.

             Moja ya machimbo ya madini nchini Tanzania.




Hivi karibuni katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini alitoa hotuba ambayo iliniacha mdomo wazi, katibu mkuu huyo alisema kuwa Tanzania imewekeza katika miradi mikubwa sita katika gesi,mafuta na madini, katika miradi hiyo ya madini ni mitatu ambayo uzalishaji inasemekana umeanza miaka 12 iliyopita ambapo miradi imekuwa ikiendelea vizuri sana, uzalishaji wa madini kutoka tani moja mwaka 1998 mpaka tani 50 hivi sasa unavyosoma habari hii. swali la kujiuliza kwa uzalishaji huu wa madini bado tunaendelea "kufulia" kila siku?
Wakati huo huo unaambiwa kuwa visima vya gesi vya songosongo na Mnazi bay vinatoa gesi kama upepo na huku bado kuna uwezekano mkurunga nako gesi ya kumwaga itaanza kupatikana. achilia Bahari ya Hindi na Mafia ambapo utafiti bado unaendelea. Katika hili "wadanganyika" wenzangu hatupaswi kusema kuwa Tanzania ni nchi masikini,si masikini hata kidogo labda vichwa vyetu ndio masikini. Hapo bado hatujazungumzia sekta ya utalii na rasilimali lukuki zilizotuzunguka ambazo kungekuwa na 'efficient utilization of resources' Tanzania ingeongoza kwa uchumi East Africa.

Thursday, June 2, 2011

PICHA YA LEO

Kula bila mpangilio ni hatari kwa afya yako.

KATIKA UPANGAJI MIJI SISI TULIKUWA WAPI?

Mipango miji ni suala ambalo ni la muhimu kuliko chochote katika kuendeleza miji, kutokana na kutokuwa na umakini kwa waliotangulia na waliohusika na suala zima la usimamizi wa  upangaji miji ndio leo hii tunapata adha ya msongamano wa watu mijini iwe ni kuingia au kutoka mjini, foleni za magari tatizo hili limekuwa sugu hapa kwetu Tanzania na kutokana na jinsi ambavyo tayari mji ulivyo sidhani kama tatizo hili linaweza kutatuliwa ama kupunguzwa kwasasa na hata miaka ijayo
Ingawa tumekuwa na mapungufu katika upangaji miji tangu awali, mamlaka zinazohusika nadhani huu ulikuwa wakati wa japo kujaribu kusawazisha angalau kidogo kwa kuandaa taratibu za kutanua mji walau baadhi ya ofisi iwe ni makampuni,taasisi za serikali na zisizo za kiserikali na mashirika walau zitengewe maeneo nje ya mji ili kuondoa msongamano katikati ya jiji jambo ambalo linawapa wananchi mawazo kila inapofika asubuhi kwenda makazini na kwenye shughuli mbalimbali na pia wakati wa jioni wakiwa wanarudi.
Huwa nasikia faraja na wivu ninapoona nchi ambazo zimejipanga vyema tokea zamani ambapo hivi sasa zina mtiririko mzuri wa miji.

Pichani ni jiji la Johannesburg nchini Afrika ya kusini kama linavyoonekana katika picha hii iliyopigwa kutoka katika jengo refu kuliko yote Afrika la Carlton Tower.

Pichani ni moja ya miji ambayo ni mfano kwa jinsi ilivyopangiliwa, hili ni jiji la Barcelona nchini Uhispania.

                                       Harare,Zimbabwe.

Wednesday, June 1, 2011

PICHA YA LEO

Maisha ndivyo yalivyo wakati mtu anatafuta gari la kutembelea anakosa wengine wanakula bata kama unavyoona pichani gari likiwa na bwawa la kupumzikia.

PILIPILI KICHAA NJIA NYINGINE YA KUPUNGUZA UZITO.

Maisha ya kila siku ya binaadamu kwa asilimia kubwa yametawaliwa na suala la kupata msosi ili kuweka sawa miili tayari kwa kuweza kuendelea kuishi na kufanya kazi za kila siku katika maisha ya mwanadamu, kuna suala la kufahamu ni vyakula gani vya kula na kwa wakati gani japokuwa hili lipo tofauti kwa watu yaani inategemeana na mwili wa mtu ambapo kuna miili ya watu hukubaliana na vyakula vya aina fulani na kukataa vyakula vya aina fulani japokuwa kuna watu wengine hali hii ni tofauti kwa maana ya kwamba wao hakuna kinachodunda miilini mwao kila kitu pwani
Ulaji wa vyakula vya mbalimbali bila kuucontrol ulaji husababisha baadhi ya watu kuwa na uzito kupita kiasi hali ambayo huwaweka katika hatari ya kupata magonjwa mbalimbali leo napenda niwashauri wale ambao wana uzito ambao haulingani na miili yao kuwa pilipili kichaa inaweza kukusaidia kupunguza uzito. Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na wanasayansi na zimeandikwa katika makala ya pscology & behaviour, wataalamu wa mambo wanasema nusu kijicho cha chai chenye pilipili kichaa katika mlo wako humeng'enya kalori 10 zaidi ya kiwango cha kawaida katika milo 25.

Tuesday, May 31, 2011

TUBADILIKE KATIKA HILI.

Imekuwa ni kama desturi watu kupuuza kanuni na taratibu zinazowekwa sehemu mbalimbali nchini aidha kwa makusudi au kwa kutokujua na bado wahusika wakafumbia macho uvunjwaji wa kanuni na taratibu hizo. Utathibitisha haya utakapopita mitaani na kukuta maeneo yamejaa takataka ili hali pameandikwa usitupe taka hapa lakini ndio panakuwa dampo la kimataifa hali hii ninaweza kusema imechangia kwa kiasi kikubwa miji mingi Tanzania kuwa michafu kupita kiasi. Sielewi ni kwa faida au hasara ya nani mtu anapoamua kutupa takataka sehemu ambayo hairuhusiwi maana inaonekana kila mtu anapuuza na hata wanaohusika katika kusimamia mazingira inawezekana mtu anaacha kama vile anasema kwani ni nyumbani kwangu hapo aaah acha pawe pachafu,jamani kumbukeni hayati baba wa taifa Mwl J.K. Nyerere aliwahi kusema kuwa mwenye kujenga ama kubomoa nchi ni mwananchi mwenyewe sasa katika hili kwanini tunataka mpaka mtu atumie nguvu?
Siku hizi kumezuka mtindo watu wanakusanya uchafu majumbani mwao wanajaza kwenye mifuko ya plastic au kwenye viroba halafu wanasubiri usiku au gizagiza na kwenda kuvitelekeza katika maeneo ya wazi yaani kana kwamba ameambiwa pale ndio jalalani.

wafanyabiashara wakifanya biashara eneo lisilo rasmi.

Hali hii ya kukaidi kanuni na taratibu ndio leo hii inaleta mgogoro kati ya halmashauri ya jiji na wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga,kuna maeneo yametengwa kwa biashara lakini wao wanataka tubanane humuhumu mijini jamani kwa staili hii hatutofika hakuna kitu nkizuri kama kufuata sheria,kanuni na taratibu zinazowekwa kwa manufaa ya wote. Pichani wafanyabiashara wakiendeleza biashara sehemu isiyo rasmi tena huku kukiwa na tangazo kubwa tu ambapo hata asie na macho anaweza kuliona.naomba nisichonge sana alieelewa kaelewa na ambaye anajifanya hajaelewa mimi najua kaelewa.

Monday, May 30, 2011

TANGAZA KUPITIA BLOG HII

BONYEZA: mobile +255 712 184 598, au +255 689 184 598
                     E-mail,   jiffjeff@yahoo.com