Wednesday, June 8, 2011

WANYAMA NI RAFIKI WAZURI KWA BINADAMU.

Hapa duniani kiumbe ambaye amepewa akili ya kuweza kuufahamu ulimwengu na kuutawala ni Binaadamu, Pamoja na hilo maisha ya Binaadamu yanategemea viumbe wengine waliomzunguka kwa asilimia kubwa,mfano binaadamu wanategemea wanyama kwa kupata chakula mfano,Ng'ombe,mbuzi,nguruwe,kondoo na wengineo wengi. Binaadamu anategemea wanyama wengine kwa kazi za kila siku mfano,Punda kubeba mizigo, Ng'ombe kulimia na hata ubebaji wa mizigo. vilevile Binaadamu anategemea wanyama kwa ulinzi kwa mfano Mbwa.
Lakini baadhi ya wanyama wametokea kuwa adui wakubwa kwa Binaadamu kwa mfano Simba,Chui,Nyoka,na wengineo wengi. Lakini nimegundua kuwa Binaadamu na wanyama wanaogopana kwasababu hawajajuana, lakini pindi Mnyama anapokuwa karibu na akawa na mazoea na Binaadamu basi huwa rafiki mzuri sana wa Binaadamu kwa mfano Simba,Chui,Mbwa,Dubu ,Nyoka na wengineo wengi.angalia picha zifuatazo kwa ushahidi zaidi.
Samaki aina ya DOLPHIN wakicheza na watoto.


Chui wakijiachia kitandani na mlezi wao.

Pamoja na kuwa na urafiki na Binaadamu hata wao kwa wao ni marafiki.

Tuesday, June 7, 2011

PICHA YA LEO

Ni kama huyu mtoto anasema " Aaah mzee...unanipa pipi? shuka uone home tulivyo majalala..hapa nilipo sina hata sare za shule, home hatujala tokea jana mchana".

WAJUE 10 WANAOWANIWA NA ARSENE WENGER.

Meneja wa timu ya Arsenal ya uingereza Arsene Wenger amnahusishwa na nia ya kuhitaji wachezaji ambao atawatumia kujenga kikosi cha timu ya Arsenal ambacho kimemaliza ligi na hali mbaya japokuwa kilikuwa kikiwania ubingwa kwa karibu zaidi, wachezaji ambao wapo kichwani mwa Wenger ni hawa wafuatao. 
1-Gervinho, mshambuliaji wa Lille ya ufaransa raia wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 24 ambaye anauzwa kwa dau la paundi za uingereza milioni 12-15.


2-Borjan Kric,Mshambuliaji wa Barcelona na raia wa uhispania mwenye umri wa miaka 20 dau lake ni paundi za uingereza milioni 16-18. 

3-Mamadou Sakho,mlinzi wa kati wa PSG na raia wa ufaransa mwenye umri wa miaka 21 dau lake ni paundi za uingereza milioni 12-18.

4-Jan Vertonghen,Mlinzi wa kati wa Ajax na raia wa ubelgiji, umri miaka 24,dau lake ni paundi za uingereza milioni 12-15.
5-Gary Cahill, Mlinzi wa kati wa Bolton na raia wa uingereza, umri miaka 25,dau lake ni paundi za uingereza milioni 15-20.

6-Phil Jones, Mlinzi wa kati wa Blackburn na raia wa uingereza, umri miaka 19, dau lake ni paundi za uingereza milioni 15-18.

7-Karim Benzema, Mshambuliaji wa Real Madrid na raia wa Ufaransa,umri miaka 23, dau lake ni paundi za uingereza milioni 20-26.

8-Christopher Samba, Mlinzi wa kati wa Blackburn na raia wa Congo, umri miaka 27, dau lake ni paundi za uingereza Milioni 8-12.

9-Radamel Falcao,Mshambuliaji wa Porto na raia wa Colombia, umri miaka 25, dau lake ni paundi za uingereza milioni 26.


10-Ricardo Alvarez, mshambuliaji wa pembeni wa Velez Sasfield na raia wa Argentina, umri miaka 23, dau lake paundi za uingereza milioni 6-12.

ARSENE WENGER
wakati huo huo wenger anatafuta mrithi wa Niclas Bendtner mbali na hao kumi katika kumrithi Bendtner wengine ni Jeremy Menez wa Roma ya italy, Hugo Rodallega waWigan Athletic,Hulk wa Porto F.C, Gonzalo Higuian wa Real Madrid na Eden Hazard wa Lille.

BURRESS AMALIZA KIFUNGO CHA MIAKA MIWILI.

Hatimaye mchezaji mashuhuri wa NEW YORK GIANTS siku ya jumatatu tarehe 6 mida ya saa tatu asubuhi aliachiliwa huru kutoka gerezani ikiwa ni miezi mitatu kabla ya kifungo chake kukamilika kutokana na kuonesha tabia njema akiwa gerezani na kurudi nyumbani kwake Florida baada ya kutumikia kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kukutwa na silaha, ambapo siku ya tukio novemba 2008 akiwa katika klabu ya usiku jijini  New York kwa bahati mbaya risasi aliyoiweka kiunoni ilifyatuka na kumpiga katika mguu na kusababisha kukamatwa kwake na silaha kinyume na sheria.

                        Plaxico Burress akitoka Gerezani.

Plaxico Burress akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka gerezani.

Plaxico Burress akiwa amembeba mwanae Elijah Burress baada ya kutoka gerezani.

        Plaxico Burress uwanjani kabla ya kukamatwa kwake.


Akiwa amevalia mavazi meusi,sweater jeusi,t-shirt nyeupe na pale chini ametupia sneakers nyeusi akiwa peke yake kutoka gerezani na kuangaza huku na huko na kumuona meneja wake Drew Rosenhaus na kumrukia kwa furaha."Napenda kumshukuru mungu kwa kunipa moja ya mitihani maishani mwangu" alisema burress, "Napenda niwashukuru wote kwa maombi na maneno ya kunitia nguvu nikiwa gerezani" aliongeza Burress. Burress ambaye mwezi wa nane anatimiza miaka 34 alijitupia ndani ya Range Rover na kuungana na mkewe tayari kwenda nyumbani kufungua ukurasa mpya wa maisha baada ya kifungo.
Burress alitoka gerezani akiwa amevalia kofia ya Philadelphia Phillies na inasemekana kuna uwezekano mkubwa akarudi kuichezea tena na wakati huohuo kuna uwezekano wa timu ya New York Jets wakamchukua ili kuziba pengo la Braylon Edwards aliyestaafu.

Monday, June 6, 2011

TANZANIA UMASIKINI UNATOKA WAPI?

Watanzania kadri siku zinavyozidi hali ya maisha inazidi kuwa tete,wakati hilo linatokea wanasiasa wanatuhubiria kuwa uchumi wa nchi unakua, nashindwa kuelewa uchumi unakua hali ya maisha inazidi kuwa ngumu kivipi?

     Mgodi wa Ashanti uliopo katika migodi ya Geita.

             Moja ya machimbo ya madini nchini Tanzania.




Hivi karibuni katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini alitoa hotuba ambayo iliniacha mdomo wazi, katibu mkuu huyo alisema kuwa Tanzania imewekeza katika miradi mikubwa sita katika gesi,mafuta na madini, katika miradi hiyo ya madini ni mitatu ambayo uzalishaji inasemekana umeanza miaka 12 iliyopita ambapo miradi imekuwa ikiendelea vizuri sana, uzalishaji wa madini kutoka tani moja mwaka 1998 mpaka tani 50 hivi sasa unavyosoma habari hii. swali la kujiuliza kwa uzalishaji huu wa madini bado tunaendelea "kufulia" kila siku?
Wakati huo huo unaambiwa kuwa visima vya gesi vya songosongo na Mnazi bay vinatoa gesi kama upepo na huku bado kuna uwezekano mkurunga nako gesi ya kumwaga itaanza kupatikana. achilia Bahari ya Hindi na Mafia ambapo utafiti bado unaendelea. Katika hili "wadanganyika" wenzangu hatupaswi kusema kuwa Tanzania ni nchi masikini,si masikini hata kidogo labda vichwa vyetu ndio masikini. Hapo bado hatujazungumzia sekta ya utalii na rasilimali lukuki zilizotuzunguka ambazo kungekuwa na 'efficient utilization of resources' Tanzania ingeongoza kwa uchumi East Africa.

Thursday, June 2, 2011

PICHA YA LEO

Kula bila mpangilio ni hatari kwa afya yako.

KATIKA UPANGAJI MIJI SISI TULIKUWA WAPI?

Mipango miji ni suala ambalo ni la muhimu kuliko chochote katika kuendeleza miji, kutokana na kutokuwa na umakini kwa waliotangulia na waliohusika na suala zima la usimamizi wa  upangaji miji ndio leo hii tunapata adha ya msongamano wa watu mijini iwe ni kuingia au kutoka mjini, foleni za magari tatizo hili limekuwa sugu hapa kwetu Tanzania na kutokana na jinsi ambavyo tayari mji ulivyo sidhani kama tatizo hili linaweza kutatuliwa ama kupunguzwa kwasasa na hata miaka ijayo
Ingawa tumekuwa na mapungufu katika upangaji miji tangu awali, mamlaka zinazohusika nadhani huu ulikuwa wakati wa japo kujaribu kusawazisha angalau kidogo kwa kuandaa taratibu za kutanua mji walau baadhi ya ofisi iwe ni makampuni,taasisi za serikali na zisizo za kiserikali na mashirika walau zitengewe maeneo nje ya mji ili kuondoa msongamano katikati ya jiji jambo ambalo linawapa wananchi mawazo kila inapofika asubuhi kwenda makazini na kwenye shughuli mbalimbali na pia wakati wa jioni wakiwa wanarudi.
Huwa nasikia faraja na wivu ninapoona nchi ambazo zimejipanga vyema tokea zamani ambapo hivi sasa zina mtiririko mzuri wa miji.

Pichani ni jiji la Johannesburg nchini Afrika ya kusini kama linavyoonekana katika picha hii iliyopigwa kutoka katika jengo refu kuliko yote Afrika la Carlton Tower.

Pichani ni moja ya miji ambayo ni mfano kwa jinsi ilivyopangiliwa, hili ni jiji la Barcelona nchini Uhispania.

                                       Harare,Zimbabwe.