Friday, July 29, 2011

MAN CITY YAKAMILISHA USAJILI WA SERGIO AGUERO

Sergio Aguero anasema ameshajiunga na timu ambayo " Itajitahidi kila mwaka kushinda mataji makubwa". baada ya kukamilisha kuhama kwake kutoka Atletico Madrid hadi Manchester City.

Sergio Aguero
Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Argentina aliwasili England siku ya Jumatano kukamilisha mipango ya kuhama kwa kiasi kinachosemekana kuwa pauni za Uingereza milioni £38m.

Siku ya Alhamisi jioni timu hiyo ilitangaza kuwa Aguero ametia saini kandarasi ya miaka mitano.

Man City wanasema mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23, anatarajiwa kuwa miongoni mwa kikosi kitachocheza mechi ya kombe la Dublin mwishoni mwa juma.

Aguero, atakayevaa nambari 16, amesema katika mtandao rasmi wa Man City: " Nafkiri sisi ni timu ambayo katika siku zijazo tutakuwa tukijitahidi kushinda mataji makubwa kila mwaka.

" Wakati tukifanya mazungumzo niliwaambia mawakala wangu wafanye kila wawezalo kwa sababu hii ni timu nzuri na nilitaka sana kucheza kwenye ligi kuu ya soka ya England. Nimeridhishwa kwa hilo.

Nafkiri sitokuwa na tatizo kwenye timu hii. Nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu kufanya kile meneja anachotaka nifanye na kujaribu kuwajibika vile yeye anavyotaka mimi niwajibike."

Alipoulizwa kuhusu kuzowea maisha ya England, aliongeza: " Kwanza sipendi hali ya hewa ya joto kwa hiyo hapa nitakuwa sawa. Nina hakika nitafurahi hapa na nitakuwa sawa."

Mapema siku ya Alhamisi, Aguero aliandika kwenye mtandao wa Tweeter: " Mimi tayari ni mchezaji wa City. Nimefurahi kuwa kwenye timu hii na pia mji huu wa Manchester."

Thursday, July 28, 2011

TOLEO JIPYA LA TRENI JAPAN

Hakika Japan wapo mbali katika teknolojia, wakati sisi huku bado tunapanda "vyuma chakavu" wenzetu Japan wanakula bata..hakika toleo hili ni zaidi ya ndege.



sehemu ya abiria

maeneo ya kuelekea chooni



Abiria wakijiandaa kukwea mchuma

Treni ikikatiza mitaa

Treni ikiingia stesheni

sehemu ya dereva wa treni

WANIGERIA WAZICHAPA NDANI YA JUMBA LA BIG BROTHER AFRICA

Asubuhi ya leo Karen alimshambulia Vina kwa maneno akimshutumu na kumpasha kwa kujipendekeza kwa Lomwe wakati hamtaki hali iliyozua tafaruku kati ya mabinti hao ndani ya jumba la Big Brother africa, Karen na Vina wote wanatoka Nigeria.

Karen (kushoto) na Vina (kulia)
Awali mabinti hao walishutumiana katika vitu fulanifulani na kuanza kushikana nguo hali iliyomfanya Hanni aingilie kati ili kunusuru amani baina ya mabinti hao wawili, "mmoja akiwa moto, lazima mmoja awe maji" alisikika Hanni akiwasihi mabinti hao waache ugomvi, Kitendo cha Hanni kumsihi Vina aachane na Karen na amzoee kwani ndivyo alivyo kilionekana kumjaza ghadhabu zaidi Karen, ambapo ugomvi huo ulianza 26 julai, siku ambayo ilikuwa ni birthday ya Vina, siku hiyo Vina alibainisha kuwa Karen utani wake umezidi mipaka na sasa sio utani tena bali ni kusambaza uongo. Zikiwa zimebaki siku mbili.je wanigeria hao wataweza kushinda?

SHEREHE ZA MWAKA MMOJA KUELEKEA OLIMPIKI 2012

Sherehe zinafanyika jijini London kuadhimisha mwaka mmoja kamili kabla ya kuanza michezo ya Olimpiki ya mwaka 2012.

Uwanja utakaotumika kwa olimpiki UK 2012
Kituo cha kuogelea katika Olympic Park , Stratford kitazinduliwa na anaetarajiwa kushinda medali ya Olimpiki Tom Daley akiwa mchezaji wa kwanza kupiga mbizi.
Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olympiki (IOC) Jacques Rogge atakua katika uwanja wa Trafalgar Square ambako mifano ya medali zitakazokua zikitolewa katika michezo hiyo zitazinduliwa.
Mwenyekiti wa Kamarti ya matayarisho ya Olimpiki 2012 Lord Coe amesema mipango yote imekwenda kama ilivyopangwa.
Amesema hii ni siku kubwa kwa kamati ya matayarisho akiongeza kuwa wamepokea maombi millioni 23 ya tiketi kutoka watu milioni mbili na kwamba watu laki mbili na elfu 50 wamejitolea kutumika wakati wa michezo hii.
Katika sherehe za Trafalgar Square, usiku Bwana Rogge na Meya wa jiji la London, Boris Johnson wataialika dunia kuja London kusherehekea michezo hii majira ya kiangazi mwakani.
Bendi ya muziki wa Pop, The Feeling, kwaya za nyimbo za dini na na DJ wa Radio 1 DJ Kissey Sell Out ni miongoni mwa watakaotumbuiza.

DVD YA UMEME OUT SASA SAMAKI WENYE SUMU SIJUI IPI ITAFUATA

SERIKALI HII KIBOKO..KABLA HATUJAMALIZA KUANGALIA DVD YA UMEME TAYARI WAMEIKATISHA NA HATUJAJUA MWISHO WAKE NI NINI..STERLING NGELEJE ATAKUFA AU? HAYA WAMETUWEKEA DVD YA SAMAKI WA SUMU KUTOKA JAPAN..LAKINI PICHA HII NAYO INAONEKANA NI KALI SANA INGAWAJE WASIWASI WANGU ULEULE KUWA PICHA LIKINOGA NA WAKATI WATU TUMESHAAGIZA POP CORN NA TUMEKAA ZETU SAWA SAWA KATIKA SOFA ILI TUICHEKI KWA UZURI WATATUBADILISHIA NYINGINE, SIPENDI MCHEZO WA KUTOKUMALIZIA MOVIE ILA SINA JINSI NA SISI WENYEWE TUNAYATAKA INATAKIWA TUKOMAE MPAKA MOVIE MOJA IKIISHA WATUWEKEE NYINGINE LAKINI TUNAWAACHIA MOVIE ZIKIKOLEA WAO NDIO WANATOA.


ILA NIWAPONGEZE HIZI DVD WANAPOZIPATA MAANA KILA INAYOKUJA NI KALI KUPITA ILIYOTOLEWA,KWA HILI VIONGOZI WA TANZANIA NAWAPA 100% WAMEFUZU MAFUNZO YA KUSIMAMIA MABANDA YA VIDEO.
LAKINI HUWA NAJIULIZA UTAALAMU HUU LAZIMA KUNA MTU NYUMA YA PAZIA ANAEWAWEZESHA KUWA MAHODARI KIASI HIKI,JE NI NANI?..BILA SHAKA HAKUNA ASIEMJUA NI YULE Dk WETU..NAE NAMSIFU SANA WAKATI SISI TUNAKETI KUCHEKI MOVIE TULIYOWEKEWA YEYE HUISHIA KUTABASAMU TU BILA KUJALI HIYO MOVIE TULIYOWEKEWA KUWA INA MADHARA.

MADHARA HAYO NI PAMOJA NA KUTUUMIZA MACHO, INATUFANYA TUSHINDWE HATA KUONA VIZURI HALI INAYOPELEKEA TUNASHINDWA KUFAHAMU MAMBO TUNABAKI KUWA MAMBUMBUMBU TU TUKIACHA VITU VYA HOVYOHOVYO VIKIFANYIKA KATIKA ARDHI YETU.

PILI, HIZI MOVIE ZINAFANYA TUNATUMIA MUDA MWINGI KUZIANGALIA MPAKA TUNASHINDWA KUFANYA KAZI NA KUJIPATIA KIPATO NA KWA HALI HUU TUNADUMISHA UMASKINI KWETU NA KWA TAIFA KWA UJUMLA.

VILEVILE HIZI MOVIE ZINATUKOMAZA NA MATATIZO NA MBAYA ZAIDI SASA ZINAELEKEA KUTUFUMBUA MACHO KWA KUONA KILE KINACHOFANYIKA KATIKA MOVIE HIZI SI SAHIHI.

HAPA SASA MIMI NDIPO NINAPOOGOPA NA NINAKUOMBA Dk,sijui ni Dk wa NINI MSINIULIZE HATA MIFUGO SI NI Dk? WA KIENYEJI NAE SI NI Dk?..tafadhali TUNAELEKEA PABAYA NA HIZI MOVIE, KWA HIVI SASA TAYARI WALE WATAZAMAJI WAMESHAANZA KUZICHAMBUA NA KUJUA KILICHOMO KATIKA HILI BANDA LA VIDEO, MBAYA ZAIDI WAMESHAGUNDUA KWANINI MOVIE HAZIMALIZIWI, WAMEGUNDUA HAZIMALIZIWI KWASABABU MOVIE ZOTE HIZI WALE MA-STERLING WANATAKIWA WAFE NA KWA KUWA ZINATOLEWA MAPEMA NAKUWEKWA ZINGINE NDIO MAANA HAWAFI WANAPETA TU WAKATI WAMESHAFANYA UHALIFU MKUBWA KATIKA TAIFA.
USHAURI WANGU KWAKO Dk..TAFADHALI WAAMURU WALE WABADILISHAJI MIKANDA(DVD) PINDI DVD INAPOWEKWA HALAHALA MPAKA TUONE MWISHO WA PICHA NA TUHAKIKISHE STERLING AMEKUFA NDIO TUANGALIE MOVIE NYINGINE,NA KAMA HAJAFA BASI AWE SHUPAVU SANA KUWAPIGA MAADUI WOTE NA ABAKI PEKE YAKE.
PILI, HAKIKISHA MOVIE HAZIRUDIWI NA KABLA SIJAENDELEA KUKUPA USHAURI NINA SWALI..HIVI UNAFIKIRI HAWA MA-STERLING WAKIFA NA KAMA HAWAJAFA UKIWAUA UTAKOSA WENGINE?...UTAKAPO NIJIBU NDIO NITAENDELEA KUKUPA USHAURI ZAIDI NA HII NI KWA FAID YA TAIFA...SALAMU ZANGU KWAKO Dk.

Wednesday, July 27, 2011

BATISTA ATIMULIWA ARGENTINA

Sergio Batista amekubali kuacha ukocha wa timu ya taifa ya Argentina baada ya nchi hiyo kutolewa hatua ya robo fainali ya kuwania kombe la Copa America.

Sergio Batista
Wenyeji Argentina walitolewa na mabingwa Uruguay kwa mikwaju ya penalti.
Batista, mwenye umri wa miaka 48, amekuwa akiifundisha Argentina kwa mwaka mmoja sasa, awali akiwa kocha wa muda, baada ya Diego Maradona kutimuliwa kufuatia kutolewa katika Kombe la Dunia mwaka 2010.
Msemaji wa Chama cha Soka cha Argentina (AFA) amesema Batista hajatimuliwa, lakini imeamuliwa "kutengua" mkataba wake.
Argentina, ambayo mara ya mwisho kunyakua kombe muhimu ilikuwa mwaka 1993 waliposhinda mashindano ya Copa America, wamefuta mechi ya kirafiki dhidhi ya Romania mjini Bucharest iliyopangwa kuchezwa tarehe 10 mwezi wa Agosti.
"Makocha wa Argentina kwa viwango vyote wanafanyiwa tathmini na tume ta makocha wa taifa," aliongeza Bialo.
"Hakuna muda maalum uliowekwa, hakuna sababu ya kuharakisha kumchagua kocha mpya, kwa hiyo kuna mchakato wa kuwasoma na kuwafikiria makocha."

BECKHAM AMTETEA BALOTELLI

David Beckham amemtetea Mario Balotelli kutokana na utata uliojitokea wakati akiwa karibu na lango alipoupiga mpira kwa kisigino badala ya kufunga, hali iliyomsabababishia atolewa nje na meneja wake wakati Manchester City ilipopambana na LA Galaxy.

Balotelli

Meneja wa Manchester City Roberto Mancini alihoji umahiri wa mchezaji huyo baada ya makusudi kukataa kufunga bao la wazi.
"Niliangalia tena, kutokana na tabia yake, naamini alidhani alikuwa ameotea," alisema Beckham, huku akimshauri Balotelli aendelee kufunga katika mechi zijazo.
"Mario amekuwa mchezaji hodari kwa miaka michache iliyopita na bado ni kijana mdogo sana."
Nahodha huyo wa zamani wa England, ambaye aliwahi kuichezea Manchester United ambao ni mahasimu wakubwa wa Manchester City, ameongeza: "Ataendelea kurjirekebisha, nina hakika.
"Lakini iwapo unadhani umeotea au la, hiyo haina maana. Kuna vijana wengi wadogo wanaziangalia hizi timu na wachezaji nyota waliokuja hapa.. Ni lazima uoneshe umahiri wako an ufunge bao."
Mancini, ambaye alizozana na Balotelli wakati akitoka uwanjani baada ya dakika 31, amesisitiza mshambuliaji huyo alipokuwa Inter Milan na yeye akiwa meneja wake alijua hakuwa ameotea.
"Katika soka kila wakati unatakiwa kuonesha umahiri, kila wakati unakuwa makini na kwa wakati ule hakuwa makini na hakuonesha umahiri wake," alisema.