Thursday, August 11, 2011

JE WAJUA?

Msitu wa Amazoni unazalisha 20% ya Oxygen ipatikanayo duniani.

Mto wa Amazon unatiririsha maji mengi kuingia Bahari ya Atlantic, na zaidi ya maili 100 za bahari zinaingia katika mdomo wa mto ambapo hutoa maji safi kuelekea baharini.
Ujazo wa maji ya mto wa Amazon ni mkubwa ukilinganisha na jumla ya ujazo wa mito saba mikuu duniani kwa ujumla na mto Amazon unatambaa mara tatu zaidi ya mito yote ya U.S.

SONG OF THE DAY

Ipo poa sana....utaipenda

SIGARA INA MADHARA ZAIDI KWA WANAWAKE KULIKO WANAUME

Utafiti mpya umeonyesha kwamba wanawake walio na uraibu wa kuvuta sigara wako katika hatari ya kupata maradhi ya moyo zaidi kuliko wanaume walio na uraibu huo.
Utafiti ulioendeshwa miongoni mwa zaidi ya watu milioni mbili umepata wanawake wako kwenye hatari ya maradhi ya moyo kwa asili mia 25 wakati wanapotumia tumbako.

Sababu za matokeo haya hazijatolowa japo watafiti kutoka Marekani wamesema wanawake wako kwenye hatari kubwa ya kuvuta kemikali zenye simu kutoka kwa sigara ikilinganishwa na wanaume.

Hali hiyo wameongeza imejitokeza katika idadi ya wanawake wanaopata saratani ya mapafu ikilinganishwa na wanaume wanaovuta sigara.

Wednesday, August 10, 2011

LIGI YA UINGEREZA KUAHIRISHWA KUTOKANA YA MACHAFUKO NCHINI HUMO

Waandaaji wa Ligi Kuu ya soka ya England, wataamua siku ya Alhamisi iwapo michezo ya ufunguzi wa msimu mpya wa ligi iahirishwe au la baada ya ghasia kuendelea usiku wa kuamkia siku ya Jumanne.
Ghasia mjini Manchester
Ghasia mjini Manchester

Ghasia zimekuwa zikiendelea sehemu mbalimbali nchini Uingereza tangu siku ya Jumamosi, hali inayowafanya askari polisi wawe na kazi nyingi zaidi.
Taarifa ya pamoja iliyotolewa na Premier League imesema: "Tupo katika mazungumzo na vilabu vya London, polisi na mamlaka nyingine zinazohusika.
"Taarifa zaidi zitatolewa baada ya kutathmini hali ilivyo katika mkutano wa Alhamisi."
Kuna ratiba ya mechi tatu za Ligi Kuu ya England zitakazochezwa siku ya Jumamosi: Tottenham v Everton, Fulham v Aston Villa na QPR v Bolton.
Taarifa iliyotolewa siku ya Jumanne, imesema"hakuna sababu za kufikiria iwapo mechi nje ya London zitaathirika ", lakini hayo yalizungumzwa kabla ghasia hazijaenea hadi mji wa Manchester.
West Bromwich itaikaribisha Manchester United siku ya Jumamosi saa kumi jioni, kabla ya Manchester City kupambana na Swansea siku ya Jumatatu saa mbili usiku.
Ratiba za mechi kadha tayari zimeathirika kutokana na ghasia hizo. Mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya England na Uholanzi iliyokuwa ichezwe siku ya Jumatano imeahirishwa, Ghana na Nigeria pia mchezo wa kimataifa wa kirafiki nao ukaahirishwa uliokuwa ufanyike siku ya Jumanne.
Mechi ya kufuzu kwa Kombe la Carling kati ya Bristol Rovers na Watford pia ziliahirishwa kutokana na ushauri wa polisi, kufuatia kufutwa kwa mechi nyingine siku ya Jumanne za Charlton, West Ham, Crystal Palace na Bristol City.

RIPOTI UNYANYASAJI WA WATOTO TANZANIA YATOLEWA

Ramani ya Tanzania
Ramani ya Tanzania

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika linaloshughulikia maslahi ya watoto la UNICEF karibu theluthi moja ya watoto wa kike nchini Tanzania wanakabiliwa na unyanyasaji wa kijinsia na kuingiliwa bila hiari kabla hawajatimia umri wa miaka 18.
Shirika hilo linasema kuwa watoto wa kiume idadi yao inafika asili mia 13.4.
Kinachotumika sana katika unyanyasaji huu ni kuwatomasa watoto ambako baadae hufuatiwa na jaribio lakutaka kuwaingilia.
"Tanzania ndio nchi ya kwanza kuwa jasiri kufichua tatizo hilo linalowakabili watoto wa kike na wakiume" alisema Andy brooks afisa wa UNICEF.
Afisa mmoja wa shirika hilo Andy Brooks amesema uchunguzi huu ndio uliokamilika zaidi na umeonesha kuwa serikali iko tayari kukabiliana na tatizo hili.
Uchunguzi huu pia uligundua kuwa wale ambao wamejihusisha na mapenzi kabla ya kutimia umri wa miaka 18, asili mia 29.1 ya watoto wa kike na asili mia 17.5 ya wale wa kiume wamesema kuwa mara ya kwanza wao kujihusisha na ngono haikuwa kwa hiari yao.
Unicef inasema hii ina maana walilazimishwa ama kushawishiwa kujihusisha na ngono.
Waziri wa Elimu wa Tanzania Shukuru Kawambwa amesema kuwa serikali imejitolea kukomesha unyanyasaji wa kijinsia na kuingiliwa watoto.
Bw Brooks amesema uchunguzi sawa na huo utafanywa nchini Kenya, Rwanda, Malawi, Zimbabwe na Afrika Kusini.

Mtoto wa Gbagbo ashtakiwa Ivory Coast

Mtoto wa kiume wa aliyekuwa Rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo ni miongoni mwa watu 12 waliofunguliwa mashtaka ya kuhusika kwenye ghasia za baada ya uchaguzi na kusababisha vifo vya watu 3,000.
Bw Laurent Gbagbo

Michel Gbagbo, aliye na uraia pacha wa Kifaransa na Ivory Coast, alishtakiwa na washirika wengine wa karibu wa baba yake.
Miongoni mwao ni pamoja na waziri mkuu Pascal Affi N'Guessan, mkuu wa chama cha Bw Gbagbo.
Watu hao ni miongoni mwa wengi waliopewa kifungo cha ndani na Bw Gbagbo mwezi Aprili.
Mwandishi wa BBC John James wa Abidjan alisema viongozi wote waliokamatwa na Bw Gbagbo wameshtakiwa, isipokuwa yeye Bw Gbagbo na mkewe Simone.
Watu hao 12 wanashtakiwa kwa kushiriki kwenye uasi.
Bw Gbagbo alikataa kukubali kushindwa katika uchaguzi wa Rais mwezi Novemba.
Aliondolewa madarakani baada ya majeshi yanayomtii Rais Alassane Ouattara- mshindi anayetambulika kimataifa- kuingia Abidjan na kumkamata huku akiungwa mkono na umoja wa mataifa na majeshi ya Ufaransa.

KIKOSI KAMILI CHA ARSENAL LIGI YA MABINGWA

Kikosi cha Arsenal Champions League:
List A…
Manuel Almunia
Andrey Arshavin
Nicklas Bendtner
Marouane Chamakh
Abou Diaby
Johan Djourou
Emmanuel Eboue
Lukasz Fabianski
Cesc Fabregas
Gervinho
Kieran Gibbs
Carl Jenkinson
Laurent Koscielny
Vito Mannone
Samir Nasri
Alex Oxlade-Chamberlain
Tomas Rosicky
Bacary Sagna
Alex Song
Sebastien Squillaci
Armand Traore
Robin van Persie
Carlos Vela
Thomas Vermaelen
Theo Walcott

List B...
Aaron Ramsey
Wojciech Szczesny
Jack Wilshere
Benik Afobe
Chuks Aneke
Zak Ansah
Daniel Boateng
George Brislen-Hall
Francis Coquelin
Craig Eastmond
Luke Freeman
Emmanuel Frimpong
Sead Hajrovic
Conor Henderson
Gavin Hoyte
Jernade Meade
Ignasi Miquel
Rhys Murphy
Nigel Neita
Oguzhan Ozyakup
Gilles Sunu
Sanchez Watt
Nico Yennaris