Tuesday, October 18, 2011

Kim Kardashian kusherehekea siku yake ya kuzaliwa 21 october 2011

CAT HOUSE   photo | Kim Kardashian
Kim Kardashian katika vazi la chui

Mwanamitindo Kim Kardashian atasherehekea siku yake ya kuzaliwa siku ya tarehe 21 october 2011, kama atafanikiwa kusherehekea siku hiyo mwanamitindo huyo atakuwa anatimiza miaka 31. Tayari ameshaanza kupokea salamu za pongezi kutoka sehemu mbalimbali maalum kwa siku yake hiyo ya kuzaliwa. Happy Birthday Kim Kardashian. 

Wednesday, October 12, 2011

JE,unaweza kusoma neno hili kwa mara ya kwanza?

http://groups.yahoo.com/group/babes_in_blue

Ili usome vizuri neno hili fumba macho yako kwa 80% uangalie kwa mbaaali....nimetishaaaa

KASA HATARINI KUTOWEKA DUNIANI MAYAI YAKE DILI

Aibu kubwa duniani inafanyika huko pwani ya Costa Rica ambapo maisha na kizazi cha viumbe wa baharini aina ya kasa hatarini kupotea kutokana na watu wa maeneo hayo kufanya biashara ya kuuza mayai ya kasa kwa kasi kubwa.
Picha zifuatazo zinaonesha watu katika shughuli ya kukusanya mayai ya kasa katika pwani ya Costa Rica na kwenda kuyauza.
http://groups.yahoo.com/group/babes_in_blue/
Kasa katika pwani ya Costa Rica

http://groups.yahoo.com/group/babes_in_blue/
Mwanamama akikusanya mayai ya Kasa mbele yake bila huruma kwenda kuyauza

http://groups.yahoo.com/group/babes_in_blue/
Safari kuelekea sokoni kuuza mayai ya kasa

http://groups.yahoo.com/group/babes_in_blue/
Kazi ya kukusanya mayai ikiendelea

http://groups.yahoo.com/group/babes_in_blue/

http://groups.yahoo.com/group/babes_in_blue/

http://groups.yahoo.com/group/babes_in_blue/
Hakuna mtu kubaki nyumbani kazi ni moja tu

http://groups.yahoo.com/group/babes_in_blue/
http://groups.yahoo.com/group/babes_in_blue/
Oyaa picha hiyo nomaaa

http://groups.yahoo.com/group/babes_in_blue/

PICHA YA LEO

    Mpishi katika Hotel moja ya nyota tano nchini Italia akifanya mambo.

PICHA AMBAZO HUJAWAHI KUZIONA POPOTE





Bruce Lee na Chuck Norris

Cheguevara na Fidel Castro

Copacabanna Beach,Rio De Jeneiro.BRAZIL

Meli ya Titanic ikiwa chini ya Bahari

Familia ya OSAMA,Osama amezungushiwa kiduara chekundu

Tuesday, October 11, 2011

VAN PERSIE AWEKA "MJENGO" SOKONI

Van Persie says he believes in Arsenal, puts house up for sale
Nyumba ya Van Persie ambayo ameiweka sokoni inauzwa paundi za Uingereza milioni 1,395,000.

Van Persie says he believes in Arsenal, puts house up for sale
Sehemu hii ni  dhahiri kuwa nyumba hii inamilikiwa na mwanamichezo kutokana na mpangilio wa upambaji wake.

Thursday, September 29, 2011

Yanga yafanya maangamizi yaisambaratisha Coastal Union 5-0














Davis Mwape akichanja mbuga

Kenneth Asamoah alitia kambani mabao mawili na kuiongoza Yanga kuwasambaratisha wagosi wa kaya ambao ni vibonde wa ligi Coastal Union kwa mabao 5-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mabingwa hao waliopoteza mvuto kwa mashabiki wao kutokana na kuanza ligi kwa kusuasua jana walionekana tofauti kabisa kwani katika dakika ya nne mshambuliaji wao wa kimataifa wa Ghana, Asamoah alifunga bao la kwanza kabla ya Shamte Ally, Davies Mwape, Nurdin Bakari na Mghana huyo kufunga kalamu hiyo ya kishindo.

Kiungo Idrisa Rajabu alitoa mchango mkubwa kwenye mauaji hayo kwa kutengeneza mabao matatu kati ya matano ikiwa ni mechi yake ya tatu kuanza kuitumikia Yanga.

Umakini huo wa safu ya ushambuliaji ya Yanga unamfanya kocha Sam Timbe kutomfikiria kabisa mshambuliaji wake Jerryson Tegete aliyefunguliwa na uongozi wake hivi karibuni.

Timbe aliwapumzisha Mwape, Shamte na Asamoah na kuwaingiza Rashid Gumbo, Julius Mrope na Hamis Kiiza.

Mabingwa hao sasa wamefikisha pointi 12, huku Coastal wakibaki mkiani na pointi zao nne katika ligi hiyo inayoongozwa na Simba yenye pointi 18.

Mshambuliaji Davies Mwape alijaribu kufunga bao la mapema katika dakika ya 2, lakini mpira wake wa kichwa ulidakwa na kipa wa Coastal Union, Omar Hamis na dakika mbili baadaye Asamoah alifungia Yanga bao la kuongoza akimalizia kwa kichwa krosi nzuri ya Idrisa Rajabu.

Mshambuliaji wa kimataifa wa zamani wa Kenya, Ben Mwalala alikaribia kuipatia timu yake bao katika dakika 11 baada ya kuunganisha vizuri krosi kutoka upande wa kulia iliyopigwa na Daniel Lianga, lakini kipa wa Yanga, Yaw Berko aliupangua mpira huo.

Winga Shamte Ally aliipatia Yanga bao la pili katika dakika ya 21 akiunganisha kwa umakini krosi ya Asamoah kutoka upande wa kushoto, wakati Wagosi hao wakishaanga uwanja wa Taifa, Mwape aliendeleza kalamu ya mabao kwa kufunga bao la tatu kwa Yanga katika dakika ya 30 kwa kuunganisha kwa shuti kali pasi ya Rashid kutoka winga ya kushoto.

Mshambuliaji Mwalala alijaribu kuwaongoza vijana wake bila ya mafanikio kwa sababu katika dakika ya 35 alipiga shuti kali lililopanguliwa na Berko na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

Nurdin Bakari aliipatia Yanga bao la nne katika dakika ya 41, akimalizia pasi nzuri ya Asamoah.

Yanga ambayo safu yake ya ushambuliaji ilikuwa ikilaumiwa kwa ubutu ilionekana kuwa bora mbele ya mabeki dhaifu wa Coastal Union ambao wameruhusu timu hiyo kufungwa mechi sita kati ya nane ilizocheza msimu huu.

Coastal mabingwa wa mwaka 1988 wanaofundishwa na Hafidh Bardu walishindwa kucheza kabisa na kumtegemea Mwalala wakati wapinzani wao Yanga wakitawala asilimia 80 ya ya mchezo huo katika nafasi ya kiungo na ushambuliaji.

Asamoah alipachika bao la tano katika dakika ya 46 akipokea krosi ya Rajabu na kuifanya Yanga kushinda kwa mabao 5-0. Asamoah amefunga mabao manne tangu msimu huu wa Ligi Kuu uanze.

Kocha wa Coastal Union, Badru alimpumzisha kipa wake Hamis aliyeruhusu mabao manne na kumwingiza Godson Mmasa, pia Coastal ilimtoa Mwinyi Abdulrahman na kumuingiza Said Swed