Wednesday, October 26, 2011

Toleo maalum la marafiki zangu wa FACEBOOK-wanawake















































LIFE WITHOUT WIFE IS NOT BRIGHT



Man United "Mansita",Arsenal "Gunners" zasonga mbele Carling Cup

Manchester United imesonga mbele na kuingia katika 16 za mwisho baada ya kuizaba Aldershot 3-0 katika mchezo wa raundi ya nne wa Kombe la Carling.

Magoli ya United yalifungwa na Dimitar Berbatov, Michael Owen na Antonio Valencia.

Man United walipoiadhibu Aldershot

Arsenal nayo imeichapa Bolton 2-1. Bolton ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango la Gunners kupitia Fabrice Muamba.

Hata hivyo Arsenal walijibu mashambulizi na kupata bao la kusawazisha kupitia Andrey Arshavin, na goli la ushindi kufungwa na Park Chu Young.

Arsenal ikiichabanga Bolton

Kwingineko Cardiff ilipata ushindi baada ya kuichapa Burnley 1-0.

Crystal Palace nayo ikaifunga Southampton 2-0.

Michezo mingine ya raundi ya nne itachezwa siku ya Jumatano, ambapo Stoke City itacheza na Liverpool, Wolverhampton kupambana na Manchester City, Blackburn kucheza na Newcastle, na Everton kuikaribisha Chelsea.

ABIRIA WATEKETEA KWA MOTO NDANI YA BASI

Katika eneo la Misugusugu lililopo Barabara Kuu ya Dar es Salaam - Morogoro wilayani Kibaha mkoani Pwani, pale basi la Kampuni ya Deluxe lilipopinduka kisha kuwaka moto na kusababisha abiria zaidi ya 25 kuungua.Ajali hiyo ni mbaya zaidi ya zilizotokea hivi karibuni katika barabara hiyo kwani baadhi ya abiria waliteketea kabisa na kubaki majivu huku wenzao wachache waliowahi kutoka ndani ya gari hilo wakishuhudia, lakini hawakuweza kusaidia kuwaokoa.

Ajali hiyo lilitokea saa 9:00 alasiri na basi lililohusika na tukio hilo ni aina ya Volvo mali ya kampuni Diluxe, likitokea Dar es Salaam kwenda Dodoma.

Polisi wathibitisha
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ernest Mangu alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo alisema ni abiria 17 tu ndio walionusurika na kwamba kumi kati yao walipata majeraha ya kawaida wakati wengine saba walipata majeraha ya moto.

Kamanda Mangu alisema majeruhi wote walikimbizwa kupelekwa katika hospitali teule ya Tumbi, Kibaha .

Mangu alisema chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa gurudumu la mbele kulia la gari hilo ambalo baadaye lilipinduka na kutumbukia korongoroni na kuwaka moto ambao kila baada ya dakika chache ulionekana kuongezeka kuwa mkubwa kutokana na upepo mkali uliokuwa ukivuma muda huo wa alasiri.

"Kwa kweli hii ajali naweza kusema ni mbaya na inasikitisha sana maana ni abiria wachache tu ndio walioweza kuokolewa na wenzao zaidi ya 25 tunakadiria waliungua na kuteketea kabisa hadi kuwa majivu kutokana na moto uliokuwepo kuwa mkubwa sana,"alisema Mangu.

Alisema ajali hiyo kama ikilinganishwa na zilizotokea hivi karibuni mkoani humo, wao kama polisi wanakiri hiyo ya jana ni mbaya zaidi na inayosikitisha kwani idadi halisi ya abiria walioteketea haijajulikana na kwamba ofisi yake inafuatilia zaidi kujua idadi halisi ya abiria waliosajiliwa kwenye ofisi za basi hilo Ubungo Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, basi hilo lilikuwa limebeba abiria 42 kutoka Ubungo, lakini kukawa na taarifa kwamba huenda idadi hiyo ikawa imeongezeka kutokana na abiria wengine waliopandia njiani.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabani, Mohamed Mpinga, alipoulizwa jana jioni alisema bado haikuweza kuthibitika mara moja idadi halisi ya waliofariki na majeruhi.
Mpinga ambaye alikuwa eneo la tukio alisema uchunguzi na juhudi za kufahamu idadi halisi ya vifo na majeruhi ilikuwa ikifanyika.



Mashuhusa wa ajali
Hata hivyo, taarifa zisizo rasmi zinaeleza awali, basi hilo liliondoka katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo kikiwa na abiria 45, lakini walikuwepo wengine baadhi ambao walipandia njiani katika eneo la Kimara, Mbezi na Maili Moja Kibaha.

Kwa upande wao mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema basi hilo lilikua kwenye mwendo kasi na lilipofika eneo hilo walisikia kishindo kikubwa na walipofuatilia waliona basi hilo likitumbukia kwenye mtaro mkubwa pembezoni mwa barabara huku moshi mkubwa ukifuka kutoka ndani ya gari hilo.

''Sisi kama kawaida yetu tulikua kijiweni na hili basi lilitupita kwa kasi hapa, lakini muda mfupi tulisikia kishindo na tukatoka na kufatilia, tukagundua ni ajali, tulianza kukimbilia kuokoa watu, lakini masikini tulifanikiwa kuwatoa 10, moto ukawa umetuzidi nguvu. Wengi wakawa wanalia kuomba msaada,”alisema Ramadhani Hussein na kuongeza:,

Shuhuda mwingine, Adam Sultan alisema chanzo cha ajli hiyo ni uzembe wa dereva ambaye alikuwa akijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake hali eneo hilo halistahili kufanya hivyo kwa kuwa lina mlima.

Kwa upande wa shuhuda Abdallaha Kijukuu alisema kuna uwezekano mkubwa kwamba ajali hiyo imesababishwa na mtarimbo unaoshika matairi ya nyuma (diff), kwamba ilikuwa imepata moto kisha kusababisha gari hilo kupinduka.Mashuhuda hao walisema baada ya ajali hiyo kutokea, waliamua kusogelea gari kwa ajili ya kuokoa watu, lakini walikuta vioo vyote vimefungwa hivyo walianza jitihada za kuvipasua ili kuokoa watu hao.

Alisema walifanikiwa kuokoa majeruhi 8 na wengine walitoka wenyewe na kukimbia eneo la tukio wakati gari likifuka moshi.

Majeruhi anena
Mmoja wa majeruhi wa ajali, Danda Juju alisema kwamba huenda kukawa na zaidi ya abiria tisa waliungua ndani ya basi hilo. ,” Nilitokea dirishani na nikaanza kuokoa baadhi ya watu kupitia madrisha mawili tu, moto ulipozidi sikuweza kuendelea, lakini kwa haraka nadhani kama watu tisa watakuwa wameteketea ndani kwa moto,” alisema Juju ambaye ni kada wa NCCR-Mageuzi

Kwa upande wake, Juju alisema ameumia kwenye mguu na mkonono, lakini hali yake haikuwa mbaya sana hivyo aliweza kurejea nyumbani kwake Dar es Salaam.

Monday, October 24, 2011

FERGUSON AMWAGA CHOZI KATIKA KIPIGO CHA 6-1


Kocha wa Man U, Sir Alex Ferguson alishindwa kuvumilia kipigo cha bao 6 kutoka kwa Man City na kujikuta akilimwaga chozi hadharani...inaumaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

MAN CITY YAISAMBARATISHA MAN UNITED 6-1 OLD TRAFFORD, "MKORA"BALOTELLI ATUPIA 2 AGUERO 3. ARSENAL YAIADHIBU STOKE VAN PERSIE ATUPIA 2

Balotelli
Balotelli

Kinyume na matarajio ya Wengi, Man United walishindwa kabisa kuhimili vishindo vya majirani zao na mahasimu wao wa jadi. Hadi mapumziko City walikuwa wakiongoza kwa goli moja lililofungwa na Mario Balotelli.

Balotelli akishangilia na ujumbe WHY ALWAYS ME?

Man United walicheza karibu kipindi chote cha pili wakiwa na mchezaji mmoja pungufu baada ya beki Jonny Evans kupewa kadi nyekundu kwa kumzuia Balotelli kwenda kumuona kipa wa United David De Gea.

Video ya matukio na magoli yote Man C vs Man U

Baada ya kutolewa kwa Evans, karamu ya magoli ilianza kwa City. Balotelli aliongeza bao la pili katika dakika ya 60. Sergio Aguero akafunga bao la tatu katika dakika ya 69. Edin Dzeko baada ya kuingia kama mchezaji wa akiba alifunga bao la nne katika dakika ya 90, David Silva bao la tano na Dzeko tena kupiga msumari wa mwisho katika filimbi ya mwisho ya mchezo.

Bao pekee la kufutia machozi la United lilifungwa na Darren Fletcher katika dakika ya 81.

Matokeo haya yanaipa City pointi tatu ambazo zinaifanya kuendelea kuongoza kwa pointi tano zaidi ya United.

Katika michezo mingine, Arsenal iliizaba Stoke City 3-1. Gervino aliandika bao la kwanza katika dakika ya 27, ingawa bao hilo lilisawazishwa na Peter Crouch. Hata hivyo Robin Van Persie ambaye alianza bechi katikika mchezo huo aliingia na kufunga mabao mawili.

Video ya magoli Arsenal vs Stoke City
Everton nayo ikicheza ugenini ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Fulham. Mabao ya Everton yakifungwa na Royston Drenthe, Luis Saha na Jack Rodwell. Bao la Fulham lilifungwa na Bryan Ruiz.

SIMBA YANGA ZAWABANGUA MAAFANDE KUKUTANA USO KWA MACHO JUMAMOSI 29 Oktoba 2011

SIMBA, juzi walizidi kujiimarisha kileleni mwa Ligi Kuu Bara baada ya kuilaza Ruvu Shooting mabao 2-0, katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam. Kwa ushindi huo, Simba imefikisha pointi 24 na kuzidi kukalia kiti cha ligi hiyo, huku ikiwa imecheza mechi 10 na kuiacha JKT Oljoro ikiwa ya pili kwa kujikusanyia pointi 19.

Ruvu Shooting walikuwa wa kwanza kulifikia lango la Simba, dakika ya sita, Abdallah Juma, alishindwa kuitumia vizuri nafasi aliyoipata kwa kupiga mpira nje ya lango.

Dakika tano baadaye, Kassim Linde, alishindwa kuitumia vizuri nafasi aliyopata baada ya kupiga shuti lililotoka nje.

Simba walijibu mashambulizi, dakika ya 16, Emmanuel Okwi, alipiga shuti kali lililookolewa na mabeki wa Ruvu Shooting.

Mshambuliaji Uhuru Seleman, dakika ya 25, alipiga shuti kali lililogongwa mwamba wa goli na kuokolewa na mabeki Shooting.

Hassan Dilunga wa Ruvu Shooting, alipata nafasi nzuri ya kufunga dakika ya 42, lakini mpira aliopiga ulitNa Speciroza Joseph

SIMBA, jana walizidi kujiimarisha kileleni mwa Ligi Kuu Bara baada ya kuilaza Ruvu Shooting mabao 2-0, katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo, Simba imefikisha pointi 24 na kuzidi kukalia kiti cha ligi hiyo, huku ikiwa imecheza mechi 10 na kuiacha JKT Oljoro ikiwa ya pili kwa kujikusanyia pointi 19.

Ruvu Shooting walikuwa wa kwanza kulifikia lango la Simba, dakika ya sita, Abdallah Juma, alishindwa kuitumia vizuri nafasi aliyoipata kwa kupiga mpira nje ya lango.

Dakika tano baadaye, Kassim Linde, alishindwa kuitumia vizuri nafasi aliyopata baada ya kupiga shuti lililotoka nje.

Simba walijibu mashambulizi, dakika ya 16, Emmanuel Okwi, alipiga shuti kali lililookolewa na mabeki wa Ruvu Shooting.

Mshambuliaji Uhuru Seleman, dakika ya 25, alipiga shuti kali lililogongwa mwamba wa goli na kuokolewa na mabeki Shooting.

Hassan Dilunga wa Ruvu Shooting, alipata nafasi nzuri ya kufunga dakika ya 42, lakini mpira aliopiga ulitoka nje ya lango.

Simba, ambao walipata nafasi sita za mpira wa adhabu, lakini walishindwa kuzitumia nafasi hizo.

Dakika ya 47, Okwi, aliwainua mashabiki wa Simba, baada ya kuifungia timu yake bao akitumia vizuri mpira ulioanza kwa Haruna Moshi 'Boban' aliyempasia Jerry Santo, kabla ya mfungaji wa bao hilo kuukwamisha wavuni.

Boban aliyeingia kuchukua nafasi ya Uhuru Seleman, aliifungia bao la pili Simba, dakika ya 54, kwa shuti la mbali lililomshinda kudaki kipa wa Ruvu Shooting, Benjamin Haule.

Bao hilo linakuwa na pili kwa wachezaji wazawa, baada ya Kapombe kufunga katika mechi dhidi ya African Lyon wiki iliyopita. Mabao 12 ya Simba, yamefungwa na wachezaji kutoka nje ya nchi.

Kufungwa kwa bao hilo, kuliwazindua Shooting ambao walikuwa wakisaka mabao ya kusawazisha, hata hivyo walikutana na ngome imara iliyokuwa ikiongozwa na Juma Nyosso na Obadia Mungusa.

Simba: Juma Kaseja, Nassoro Masoud 'Cholo', Juma Jabu, Juma Nyosso, Obadia Mungusa, Patrick Mafisango/Shomari Kapombe, Jerry Santo, Ulimboka Mwakingwe, Emmanuel Okwi, Felix Sunzu, Uhuru Seleman/Haruna Moshi 'Boban'.

Ruvu Shooting: Benjamin Haule, Michael Pius, Paul Ngalema, George Michael, Shaban Suzan, Iddi Nyambiso, Ayoub Kitala, Hassan Dilunga, Abdallah Juma/Seif Abdallah, Kassim Linde/ Juma Mdindi, Raphael Keyala/Abdallah Abdulrahman.
oka nje ya lango.

Simba, ambao walipata nafasi sita za mpira wa adhabu, lakini walishindwa kuzitumia nafasi hizo.

Dakika ya 47, Okwi, aliwainua mashabiki wa Simba, baada ya kuifungia timu yake bao akitumia vizuri mpira ulioanza kwa Haruna Moshi 'Boban' aliyempasia Jerry Santo, kabla ya mfungaji wa bao hilo kuukwamisha wavuni.

Boban aliyeingia kuchukua nafasi ya Uhuru Seleman, aliifungia bao la pili Simba, dakika ya 54, kwa shuti la mbali lililomshinda kudaki kipa wa Ruvu Shooting, Benjamin Haule.

Bao hilo linakuwa na pili kwa wachezaji wazawa, baada ya Kapombe kufunga katika mechi dhidi ya African Lyon wiki iliyopita. Mabao 12 ya Simba, yamefungwa na wachezaji kutoka nje ya nchi.

Kufungwa kwa bao hilo, kuliwazindua Shooting ambao walikuwa wakisaka mabao ya kusawazisha, hata hivyo walikutana na ngome imara iliyokuwa ikiongozwa na Juma Nyosso na Obadia Mungusa.

Simba: Juma Kaseja, Nassoro Masoud 'Cholo', Juma Jabu, Juma Nyosso, Obadia Mungusa, Patrick Mafisango/Shomari Kapombe, Jerry Santo, Ulimboka Mwakingwe, Emmanuel Okwi, Felix Sunzu, Uhuru Seleman/Haruna Moshi 'Boban'.

Ruvu Shooting: Benjamin Haule, Michael Pius, Paul Ngalema, George Michael, Shaban Suzan, Iddi Nyambiso, Ayoub Kitala, Hassan Dilunga, Abdallah Juma/Seif Abdallah, Kassim Linde/ Juma Mdindi, Raphael Keyala/Abdallah Abdulrahman.


YANGA YAISAMBARATISHA JKT OLJORO
Wakati huohuo jana Yanga ya Dar es salaam wameiadhibu Timu ya maafande wa JKT Oljoro kwa bao 1-0 katika uwanja wa Chamanzi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Kazi nzuri ya mshambuliaji wa kimataifa Haruna Nyonzima akiwatoka akiwazidi ujanja mabeki wa Oljoro na kutoa pande maridadi kabisa lililomkuta Hamis Kiiza akiwa katika nafasi nzuri ya kushinda nae bila ajizi akaachia kombora kali lilioenda mojo kwa moja kimiani na kuihakikishia timu yake ya Yanga ushindi wa goli 1-0 katika mechi hiyo.