Wednesday, January 25, 2012

Breaking NEWS: Washiriki BIG BROTHER AFRICA 7 Kushiriki na wapenzi wao



Unaweza kupata nafasi ya kushiriki katika shindano la Big Brother Afrika 7 mwaka huu kuanzia februari 5 lakini lakini hautashiriki peke yako utahitajika kuingia na mpenzi wako.

Waandaji wa Big Brother Afrika wameleta mshangao "suprise" nyingine katika mashindano hayo baada ya kutangaza kuwa katika mashindano ya mwaka huu washiriki wote kila mmoja atahitajika kuingia mjengoni na mpenzi wake.
Katika hali ya kushangaza zaidi mshindi wa mwaka huu atajinyakulia kitita cha dola za kimarekani 300,000 na ili kunyakua kitita hiki utaingia katika shindano ukiwa na mpenzi wako.

Kwahiyo kama utaamua kuingia na baba,mama,dada,kaka,rafiki wa kike,rafiki wa kiume,mpenzi,mchumba,mume,mke au yeyote lakini ili mradi muwe wawili (pair), je,nani atayatoa maisha pamoja na wewe? kumbuka unaweza kutumia muda mwingi na mtu ulieingia nae kama mpenzi wako hivyo kuwa makini katika kuchagua nani wa kuingia nae.

Katika shindano la mwaka huu waandaaji wametangaza Ethiopia kushiriki kwa mara ya kwanza katika mashindano hayo. Ina maana ili ushiriki mwaka huu lazima uwe na mwenzi wako kutoka katika nchi wasiriki kama ifuatavyo Angola, Botswana, Ghana, Kenya, Liberia, Malawi, Namibia, Nigeria, Sierra Leone, South Africa, Tanzania, Uganda, Zambia and Zimbabwe.
Wapenzi lazima wawe wametoka nchi moja, wawe wanajua kuzungumza vizuri lugha ya kiingereza,umri miaka 21 na kuendelea  na wawe na pasi ya kusafiria iliyo hai (valid passport).

Fomu za kushiriki zitanza kutolewa tarehe 5 februari na mwisho itakuwa tarehe 27 februari. kwenye mtandao fomu zitapatikana kwenye mtandao wa www.endemol.co.za .
Kazi kwenu mnaotaka kuuza sura na mademu zenu ndani ya nyumba wahini mkajiandikishe mimi mwenzenu tayari.

Real Madrid kufuta uteja kwa Barcelona leo?


Kocha wa Barca Pep Guardiola


Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho

REAL Madrid wanatakiwa kusahau mbinu yao ya kujilinda na kucheza kwa kushambulia dhidi ya Barcelona kwenye mchezo wa pili wa robo fainali ya Kombe la Mfalme leo.Kocha wa Madrid, Jose Mourinho amekuwa kwenye wakati mgumu kwa mbinu yake hiyo iliyosababisha wakafungwa 2-1 wiki iliyopita na Barcelona, Mreno huyo alirudia tena Jumapili waliposhinda 4-1 dhidi ya Athletic Bilbao.
Ushindi huo ulionyesha ubora wa kushambulia wa Madrid wakiongoza ligi na kuicha Barcelona kwa pointi tano baada ya kufunga mabao 67 katika mechi 19 walizocheza hadi sasa.Bado Mourinho hajaomba radhi mbinu za Madrid katika mchezo wa kwanza, kitendo kilichowaudhi hata mashabiki wa kocha huyo pamoja na vyombo vya habari vya Madrid.
Jumapili gazeti la Marca liliandika kuwa kumekuwa na mvutono kwenye vyumba vya kubadilisha wakati Mourinho alipokuwa akitangaza kikosi cha kucheza dhidi ya Bilbao kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu hiyo ni mara ya kwanza kutokea kwa kocha huyo tangu alipotua hapo 2010.
“Chochote kilichosema kuhusu mgawanyiko au madai ya kugombana ni uongo,” Sergio Ramos aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, siku moja baada kutokea mabishano kati ya beki huyo wa Madrid na Mourinho. “Hili ni kundi bora wenye umoja, bila ya kujali nini kimesemwa.”Safu ya ushambuliaji wa Madrid itaimarika kama mshambuliaji wa Argentina, Angel di Maria atakuwa amepona majeruhi yake.
Beki Pepe haijulikana kama atacheza baada ya kuwekwa benchi kwenye mchezo dhidi ya Bilbao kufutia kitendo chake cha kumchezea vibaya Lionel Messi kwenye mchezo wa kwanza.Madrid imeshinda mechi moja kati ya 13 walizocheza dhidi ya Barcelona hiyo ilikuwa kwenye fainali ya Kombe la Mfalme mwezi Aprili na wamefungwa mechi tisa.
Barcelona itashuka dimbani ikiwa na rekodi ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Malaga, huku Messi akiweka rekodi ya kufunga mara 10 katika ligi mabao matatu 'hat trick' kwa mabingwa hao wa Ulaya.
Messi kwa sasa amefunga mabao 36 kwenye mashindano yote msimu huu, huku Alexis Sanchez ameweza kuendana na mchezo wa mabingwa hao na tayari mshambuliaji huto wa Chile ameshafunga mabao tatu katika mechi nne zilizopita.
“Wanaongoza ligi, wanaweza kufuzu kwa nusu fainali ya Copa na wapo kwenye raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa. Kwa mtazamo wa nje ni vigumu kujua kama wana matatizo au hapana,” alisema kiungo wa Barcelona, Andres Iniesta juzi.
Pia, Mirandes inahitaji kuifunga Espanyol ili kuwa timu ya kwanza ya daraja la tatu kufika nusu fainali tangu ilipofanya hivyo Fugueres mwaka 2002. Mirandes ipo nyuma kwa 3-2 itashuka kwenye uwanja wake Manispalaha ya Andova wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 6,000.
Wakati huo huo, Valencia na Athletic Bilbao wenye wanajivunia ushindi wao mkubwa waliopata kwenye mechi za kwanza.Valencia watakuwa wageni wa Levante kesho wakiwa mbele kwa 4-1 nao Bilbao walioshinda 2-0 wataivaa Mallorca leo.

Gabon ngoma inogile kombe la mataifa ya Afrika

Waandalizi wenza wa Kombe la Mataifa ya Afrika, Gabon wameanza vizuri mchezo wao wa kwanza katika kundi C walipoifunga Niger mabao 2-0 mjini Libreville.

Gabon vs Niger
Wagabon walikuwa wakiwachagiza tangu mwanzoni mwa mchezo kutafuta bao ambalo halikuja hadi kipindi cha pili zikiwa zimesalia dakika thelathini kabla mpira haujamalizika.
Nyota wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang aliunganisha krosi kutoka kwa Stephane Nguema na kufunga bao la kwanza kwa kichwa.
Nguema aliandika bao la pili kwa Gabon.
Baada ya waandaaji wenzao Equatorial Guinea kushinda mchezo wa ufunguzi kwa kuilaza Libya 1-0 siku ya Jumamosi, Gabon walikuwa katika changamoto kubwa na wao kufanya kile wenzao walichokifanya.

Tunisia vc Morocco

Nayo Tunisia walitumia makosa ya wachezaji wa Morocco waliocheza kwa kiwango cha chini kwa kuwalaza majirani zao wa Afrika Kaskazini kwa mabao 2-1 katika mchezo wa ufunguzi wa kundi C.
Khaled Korbi alikuwa wa kwanza kuipatia bao Tunisia kwa mkwaju wa adhabu ya moja kwa moja hadi ndani ya nyavu za Morocco.
Youssef Msakni aliyeingia mchezaji wa akiba aliiongezea Tunisia bao la pili kwa mkwaju mkali bada ya kuwazunguka na kuwatoka walinzi wa Morocco kwa chenga za kuvutia, kabla ya nahodha wa Houcine Kharjah kupata bao la kufutia machozi.
Morocco walipoteza nafasi nyingi za kupata mabao lakini Tunisia walistahili kushinda baada ya kuonesha kandanda ya kuvutia.

BREAKING NEWS...Boko Haram wakamatwa


Wafuasi wa Boko Haram

Nchini Nigeria kumetokea kamata kamata ambapo wafuasi wa Boko Haram walikamatwa na katika kamatakamata hiyo watu wawili wameuwawa.

Tuesday, January 24, 2012

Wenger atetea upuuzi wake wa kumpumzisha Chamberlain ilipochapwa na Man U

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger, ametetea uamuzi wake wa kumpumzisha Alex Oxlade-Chamberlain na nafasi yake kuchukuliwa na Andrey Arshavin wakati walipolazwa mabao 2-1 na Manchester United.

Wenger akitetea uamuzi wake wa kumtoa Chamberlain na kumuingiza Arshavin

Baadhi ya mashabiki wa Arsenal walisikika wakizomea wakati Oxlade-Chamberlain, aliyekuwa chachu ya kupatikana bao la kusawazisha la Arsenal, alipompatia pasi nzuri mfungaji Robin van Persie alipopumzishwa.
"Nimekuwa meneja kwa miaka 30 na nimeshabadilisha wachezaji mara 50,000. Siwajibiki kueleza sababu za kumpumzisha mchezaji kwa mtu yeyote," alisema.
Arsenal iko nyuma ya Chelsea wanaoshilikia nafasi ya nne kwa pointi tano katika mbio za kuwania kufuzu kwa ajili ya kuwania Ubingwa wa Ulaya msimu ujao.
Oxlade-Chamberlain alikuwa mmoja wa wachezaji waliong'ara kwa Arsenal katika mtanange huo uliochezwa katika uwanja wa Emirates.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18, ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuanza kucheza mechi yake ya Ligi Kuu ya England, alikuwa akimlisha sana mipira Van Persie wakati wa kipindi cha pili ambapo Arsenal walionekana kucharuka.
"Naelewa mashabiki wamechukizwa kutokana na kumbadilisha Oxlade-Chamberlain, hasa baada ya mabadiliko hayo yaliposhindwa kuzaa matunda, lakini alianza kuchoka," Wenger alifahamisha kutokana na uamuzi wake wa kumpumzisha winga huyo wa zamani wa Southampton.
"Wiki hii alikuwa akiumwa. Arshavin ni nahodha wa timu ya taifa ya Urusi. Una kijana mwenye umri wa miaka 18 akiwa ndio anaanza kwa mara ya kwanza mechi ya Ligi Kuu na mchezaji ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya nchi yake na watu wanahoji kwa nini nimefanya mabadiliko hayo?"
Alipoulizwa namna kufungwa huko kulivyoiathiri timu yake, Wenger alisema ilikuwa ni mechi ya Arsenal "ambayo isingepaswa kupoteza" kabla ya kuongeza: "Imetuweka katika nafasi ngumu sana."
Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson alisema kikosi chake kilistahili kushinda hali iliyowaweka pointi tatu nyuma ya Manchester City wanaoongoza ligi kwa sasa.
"Hatimaye nilihisi kikosi chetu kilikuwa imara," alisema. "Hongera kwa wachezaji nafasi ya ulinzi, ambao walifanya kazi kubwa.
Alipoulizwa juu ya kuikamata Manchester City, alisema: "Itakuwa ni kibarua kigumu kwetu sote."

Drogba aing'arisha Ivory Coast kombe la mataifa ya Afrika


Ivory Coast imeanza kampeni ya kunyakua Kombe la Mataifa ya Afrika kwa ushindi dhidi ya Sudan walionekana kusumbua.
Nahodha Didier Drogba alifunga bao kwa kichwa kutokana na krosi iliyochongwa na Salomon Kalou, lakini haukuwa ushindi wa kujivunia sana kwa timu inayopewa nafasi kubwa ya kunyakua kombe hilo.
Sudan itakuwa imefurahi kutokana na kandanda iliyoonesha wakati walipowasumbua Ivory Coast ambayo inajengwa na wachezaji wengi nyota wanaocheza kandanda ya kulipwa Ulaya.
Ivory Coast inamatumaini itafanya vizuri katika mchezo ujao dhidi ya Burkina Faso.
Na mshambuliaji wa Angola Manucho aliipatia ushindi Angola dhidi ya Burkina Faso katika mechi yao ya ufunguzi ya kundi B michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
Baada ya kosakosa za kipindi cha kwanza, Angola ilifanikiwa kupachika bao la kwanza lililofungwa na Mateus aliyetumia makosa ya walinzi wa Burkina Faso kuokoa mpira.
Alain Traore baadae akaisawazishia Burkina Faso kwa mkwaju wa free-kick umbali wa yadi 25.
Lakini mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Manucho aliifungia bao la pili Agola baada ya kuipangua ngome ya Burkina Faso.
Bao hilo la Manucho limeifanya Angola maarufu kwa jina la Palancas Negras, kuongoza kundi B baada ya mapema Ivory Coast kupata ushindi mwembaba wa bao 1-0 dhidi ya Sudan.
Burkina Faso walitibitishwa kushiriki michuano hiyo tarehe 10 mwezi wa Januari baada ya madai ya Namibia kutupwa pale waliposema Burika faso walimchezesha mchezaji asiyestahiki katika michezo ya kufuzu.

Monday, January 23, 2012

Bob Junior apiga show nyumbani kwa "jimama" alipwa milioni 7

Msanii wa bongo fleva ambaye ni muimbaji na mtayarishaji wa muziki (Producer) na anajulikana kama Rais wa wasafi,rais wa masharobaro,shombeshombe hivi karibuni alipiga show nyumbani kwa mama mmoja mwenye mahela ya kufa mtu na kulipwa pesa taslimu shilingi za kitanzania milioni 7 bila punguzo,hapa namzungumzia Raheem Rummy Nanji a.k.a Bob Junior.


Raheem Nanji a.k.a Bob Junior katika moja ya show zake

Katika mahojiano ya Bob Junior na radio moja jijini Dar es salaam alifunguka na kuelezea jinsi ilivyokuwa. "Aaah mimi nilipewa issue kuwa kuna mama anahitaji ukapige show maeneo ya Masaki nikakubali kwa malipo ya milioni 5" Alisema Bob Junior.
Huku akitegemea labda akifika atakuta nyomi la watu wakimsubiri atoe show, Bob Junior alishangaa kuingia kwenye nyumba ya jimama lililoshiba pesa huku mama huyo akiwa peke yake,"Nilipofika nyumbani kwake nilishangaa yupo peke yake,nikamuuliza nitafanyaje show? mama akajibu we fanya show usijali".alisema Bob Junior.

Kutokana na mshtuko jimama lilimtolea uvivu Bob Junior na kumuuliza unataka kiasi gani? tofauti na mapatano ya awali safari hii Bob Junior akataka alipwe shilingi milioni 7, bila ajizi mama akakubali kutoa dau la milioni 7 ili apate show huku akiwa peke yake hapo katika "bangalow" lake.

Baada ya mama kukubali kutoa milioni 7 Bob Junior alianza kutoa show."Kweli nilipiga show huku mama akiwa peke yake, kwanza nilipiga sebene la dakika kadhaa yaani mama alicheka sanaaaa" alisema Bob Junior.
Mtangazaji wa radio hiyo alipotaka kujua kama baada ya show mama hakumpa usumbufu mwingine? Bob Junior alifunguka kama ifuatavyo,"Hamna kitu mimi baada ya kupiga show nikatambaa,mimi pale nilienda kikazi nilipopata changu nikatambaa,au nimefanya vibaya?" Bob Junior alimuuliza mtangazaji.