Monday, February 20, 2012
R.I.P Mohammed Wardi
Mohammed Wardi
Mwimbaji maarufu wa Sudan, Mohammed Osman Wardi, amefariki mjini Khartoum akiwa na umri wa miaka 80.
Alivutia watu kupenda ala za asili za kabila lake, la WaNubi.
Kwa sababu ya maoni yake ya mrengo wa kushoto, Mohammed Osman Wardi alifungwa na Rais Jaafar Numeri katika miaka ya '80, na akahamia uhamishoni wakati rais wa sasa, Omar al-Bashir, aliponyakua madaraka mwaka wa 1989.
Mohammed Wardi kwenye concert Addis Ababa
Thursday, February 16, 2012
ARSENAL NYANYA YASASAMBULIWA 4-0 NA AC MILAN
Robinho alikuwa mwiba mkali kwa Arsenal
Matumaini ya Arsenal kuvuka salama robo fainali za klabu bingwa Ulaya ni kitumbua kilichotiwa mchanga, baada ya Jumatano jioni kunyoroshwa magoli 4-0 na AC Milan ya Italia katika mechi ya mkondo wa kwanza, ikiwa ni kati ya timu 16 zilizosalia katika mashindano hayo.
The Gunners hawakuwa na lao tangu Kevin-Prince Boateng alipoiwezesha Milan kupata bao la kuongoza. AC MILAN 4-0 ARSENAL
Zlatan Ibrahimovic alikamilisha kibarua kwa kuandikisha bao la nne la penalti, na wakati huohuo akiandikisha historia kwa upande wa Arsenal, ikiwa ndio matokeo mabovu zaidi ya Arsenal kufungwa kwa mabao mengi kiasi hicho katika pambano la Ulaya.
Miaka minne iliyopita, Arsenal ilikuwa ni timu ya kwanza ya Uingereza kufanikiwa kuishinda AC Milan ikiwa nyumbani, katika uwanja wa San Siro, wakati ilipopata ushindi wa magoli 2-0 katika mechi ya mkondo wa pili, na kuiondoa timu hiyo kutoka vilabu 16 vilivyokuwa vimesalia katika mashindano hayo ya klabu bingwa.
Benchi la ufundi la Arsenal likiwa limelowa kwa kipigo cha 4-0
Arsenal ya wakati huo ilikuwa tofauti kabisa na timu iliyoshiriki katika mchezo wa Jumatano jioni.
Mwaka 2008 Arsenal ilikuwa na uhodari mkuwa wa ulinzi, na ilicheza kwa ustadi na ikawa ni burudani kwa mashabiki wengi, kinyume na Arsenal ilivyopambana katika mechi hiyo ya San Siro.
Mshambulizi Robin van Persie amekuwa ni nyota msimu huu, lakini katika uwanja wa San Siro, inaelekea alikuwa zaidi ni abiria, na mkwaju wake uliokuwa na matumaini katika kipindi cha pili ukizuiwa na Christian Abbiati, na hata nguvu mpya za Thierry Henry alipoingia uwanjani baadaye hazikubadilisha lolote.
Bila shaka akiwa katika ndege kuelekea New York, Henry atawaza ni kwa nini aliamua kuichezea tena Arsenal.
Mambo magumu, wachezaji wa Arsenal Thierry Henry,nahodha Van Persie,Song (17) na Djourou(20) wakijadili jambo kabla ya kuanza mpira baada ya goli la tatu.
Meneja wa Arsenal alikuwa na matumaini kwamba Henry angelibadilisha mambo alipoingia katika kipindi cha pili, lakini hata kabla ya kuupata mpira, Milan tayari walikuwa wameandikisha bao la tatu.
Wenger atawaza pia juu ya umuhimu wa kufuzu kushirikishwa katika mechi za klabu bingwa, halafu kupigwa mabao mengi kiasi hicho.
Wednesday, February 15, 2012
Zambia yaingia 50 bora viwango vya FIFA, 43 Duniani ya 4 Afrika
Timu ya soka ya Zambia maarufu kama Chipolopolo wamepanda kwa nafasi 28 juu na kuingia katika 50 bora za viwango vya soka vya FIFA baada ya miaka 11 tangu ilipowahi kuwa katika 50,sasa Zambia inashika nafasi ya 4 kwa ubora wa soka barani Afrika, Zambia imepata mafanikio hayo baada ya kunyakua ubingwa wa Afrika kwa kuinyuka Ivory Coast kwa mikwaju ya penati 8 kwa 7 katika fainali kali na ya kusisimua iliyochezwa nchini Gabon katika jiji la Libraville.
Katika viwango hivyo vya soka vilivyotolewa na FIFA Ujerumani imeivuka Uholanzi na kuwa ya pili wakati huohuo Ureno(6) imepanda nafasi 1,Ivory Coast(15) imepanda nafasi 3,Mali(44) imepanda kwa nafasi 25, Ghana (23) imepanda nafasi 3 na Italy(8) imepanda nafasi 1 nazo zikipata maendeleo mazuri katika viwango vya soka Ulimwenguni.
Subscribe to:
Posts (Atom)