Pep Guardiola kocha anayetazamiwa kubwaga mikoba ya kuinoa Barcelona
Kocha wa mabingwa wa Ulaya Barcelona ambao hivi karibuni walitupwa nje katika kinyang'anyiro cha kutetea ubingwa wa klabu bingwa ya Ulaya na Chelsea, Pep Guardiola atabwaga manyanga mwishoni mwa msimu huu baada ya kufikia uamuzi wa kutoongeza mkataba wake na Klabu hiyo ya Barcelona katika ligi kuu ya Uhispania.
Rais wa Barcelona Sandro Rosell aliliambia shirika moja la Habari kuwa msimu huu ndio wa mwisho Guardiola kukinoa kikosi cha Barcelona baada ya kukataa kuongeza mkataba wake ambao unamalizika mwishoni mwa msimu huu.
Rais huyo alimshukuru Guardiola kwa kusema"Thank you for your work and your love,"
akimaanisha akhsante kwa kazi yako na upendo wako.
Polisi wa Dubai akiingalia Ferrari Enzo iliyotelekezwa Dubai na mtu aliyesadikiwa kuwa ni raia wa Uingereza, habari zaidi zinasema mshkaji huyo alifikia uamuzi wa kusepa na kuacha ndinga yenye mkwanja mrefu baada ya kushindwa kulipa kodi za ndani na kodi za askari wa usalama barabarani.
Ndinga hiyo iliyotelekezwa mwaka jana mwezi wa nane(8) na mchizi huyo, kwasasa serikali ya Dubai imeshatoa amri kwa jeshi la Polisi la nchi hiyo kulipiga mnada, wanahabari wanasema mnada huo haujawahi kutokea katika historia ya minada iliyowahi kufanywa na Polisi kutokana na ukweli kuwa ndinga hiyo ina ya Ferrari Enzo ina thamani ya kufa mtu,kiasi kinachofikia dola za kimarekani milioni 1.6
Habari zinasema kwa Dubai ni kitu cha kawaida kukuta magari ya biashara au ya thamani yakiwa yametelekezwa maeneo ya kuegeshea magari au maeneo ya viwanja vya ndege na wenye mali hizo kusepa kinyemela kukwepa kodi.