Andriy Shevchenko akitupia kambani kwa kichwa goli la kwanza Mwachemwache kati ya Ibrahimovic wa Sweden na Khacheridi wa Ukraine
Mtanange wa michuano kombe la mataifa ya Ulaya umeendelea kwa mtindo wa kipekee kwa wenyeji Ukraine kuishushia kichapo Sweden cha mabao 2-1, huku mshambuliaji matata Andriy Shevchenko 'Sheva' akifunga mabao yote mawili maridadi kabisa kukamilisha siku njema kwa waandaaji hao wenza wa michunao ya UEFA EURO 2012 katika kundi D. Zlatan Ibrahimovic aliifungia Sweden goli la pekee dakika saba baada ya kipindi cha mapumziko. Kisha baadaye mchezaji nyota wa zamani wa timu ya Milan, Shevchenko mwenye umri wa miaka 35 aliwasazisha dakika tatu baada ya bao la Ibrahimovic na kisha kupachika bao la ushindi dakika ya 68 ya mchezo.
Schevchenko akitupia la pili Schevchenko akishangilia msumari wa pili Ibrahimovic akishangilia goli la kufutia machozi
Baada ya mechi hiyo Schevchenko alisema anahisi ni kama ana umri wa miaka 20 na wala sio 35. "Tuna nafasi nzuri ya kusonga mbele katika michuano hii. Najisikia vizuri. Ulikuwa mchuano wa kihistoria kwetu. Ni ushindi wa kihistoria," aliongeza kusema Schevchenko. Kocha wa Sweden, Erik Hamren hajaridhishwa na matokeo hayo. Amesema ili kushinda mechi zao wanahitaji wachezaji 11 waonyeshe mchezo wa hali ya juu kabisa. "Leo pengine watano au sita walionyesha ujuzi ninaoutaka. Hiyo haitoshi," akaongeza kusema kocha huyo.
UKRAINE Vs SWEDEN
Ufaransa yatoka sare na England Kwenye mechi ya kwanza ya kundi D, England ilitoka sare ya 1:1 dhidi ya Ufaransa. Mkwaju wa 'freekick' uliopigwa na Steven Gerrard baada ya mwenzake James Milner kufanyiwa madhambi na Patrice Evra wa Ufaransa, ulipachikwa wavuni na Joleon Lescott kwa kichwa dakika ya 30 ya mpambano huo. Samir Nasri aliutikisa wavu wa England na kusawazisha dakika chache baadaye.
Lescott akipiga ndosi iliyokwenda moja kwa moja kambani na kuipatia England bao la kuongoza
Bao la Nasri lilikuwa na umuhimu mkubwa zaidi kuliko kusawazisha tu kwa sababu limeisaidia Ufaransa kuepuka aibu nyengine baada ya balaa la michuano ya kombe la dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini na michunao ya kufuzu kwa EURO 2008 ambapo wachezaji walirejea nyumbani wakiwa na aibu baada ya kutolewa kwenye raundi ya kwanza. Nasri mwenyewe amesema ana imani wanayo nafasi nzuri katika michuano ya mwaka huu na lengo lao ni kufika robo fainali. "Hatujapoteza kwa hiyo ni muhimu kuzingatia mpambano wetu dhidi ya Ukraine siku ya Ijumaa."
Mwajiri wetu mmoja kaka adoadoo!!! ndivyo Nasri wa Ufaransa anavyomuambia mlinda mlango wa Uingereza Joe Hart ambae wanakipiga nae Manchester City mwachemwache kati ya Ashley Cole na Samir Nasri Huendi popote hapa!!! Gerradi akimpiga mkwara Ribery
Kocha wa Ufaransa, Laurent Blanc, amesema hawajafurahishwa sana na matokeo ya mechi hiyo lakini hawajavunjika moyo. "Tungepoteza mechi hii kama hatungejitahidi, lakini ukiangalia kwa ujumla tumecheza vizuri zaidi kuliko England," ameongeza kusema kocha huyo. Naye kocha wa England, Roy Hodgson kwa upande wake amesema mechi ilikuwa ngumu lakini wameridhika na matokeo. Ufaransa sasa itachuana na Ukraine ambayo iko katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa robo fainali hukoDonetsk Ijumaa ijayo. England kwa upande wao wataumana na Sweden.
Mshambuliaji wa Star Mbwana Samatta"Samagoal" akipiga kichwa langoni mwa Gambia
Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars jana iliwatoa kimasomaso watanzania baada ya kuibugiza Gambia kwa mabao 2-1 katika mchezo mkali uliopigwa katika dimba kuu la taifa jijini Dar es salaam.Gambia ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji Mustafa Jarju akitupia kambani kwa kichwa. Wakati Gambia wakiamini wataiadhiri Stars nyumbani hamad...Shomari Kapombe akazifuta ndoto za wagambia kwa kusawazisha goli maridadi akitupia kambani kwa kichwa na kufanya matokeo kuwa 1-1 dakika ya 65 ya mtanange huo.
Mbwana Samatta"Samagoal" kama wanavyomuita mashabiki wa TP Mazembe ya kule jamhuri ya kidemokrasia ya kongo anakokipiga alikuwa mwiba mkali katika mechi hiyo kwa udambwidambwi wake kama kawa akaipepeta ngome ya Gambia kwa kumuadhiri beki wa kushoto kwa vyenga vya maudhi na kumuacha chini,Samatta alimimina krosi maridadi langoni katika mwachemwache ndipo beki wa Gambia akaunawa mpira katika eneo la hatari na mwamuzi bila ajizi akatenga maguu kumi na mbili ya mtu mzima..kama analia Erasto Nyoni akatupia kamba ya pili kwa Stars na ndipo hekaheka ,nderemo,mwachemwache zilipoibuka katika dimba kuu la Taifa..mpaka mwisho wa Mchezo Stars 2-1 Gambia. na Stars imejiweka pazuri katika kampeni za kuwania kushiriki kombe la dunia nchini Brazil 2014. Kikosi cha Stars Kikosi cha Gambia
Mbwana Samatta akiwa amewekwa chini baada ya kutaka kuleta madhara langini mwa Gambia
Nyinyi watoto wadogo tuu!!!
Mwachemwache kati ya Samatta na mabeki wa Gambia
Kambaaaaaaa!! Erasto Nyoni akishangilia pamoja na Samatta baada ya Nyoni kutupia kamba ya pili na ya ushindi ya Stars
Ndio ukubwa kakaa..Ndivyo anavyosema kocha wa Stars Kim Poulsen akimwambia kocha wa Gambia Luciano Mancini baada ya mtanange kumalizika kwa Star kuibuka washindi
Goooooooooo, bao la kwanza la Croatia Goli la pili la Croatia...kazi imeanza!!
Matumaini ya Jamhuri ya Ireland kuvuka hatua ya makundi katika mashindano ya
Euro 2012 yalididimia, baada ya kulazwa magoli 3-1 na Croatia katika mji wa
Poznan, Poland. Mario Mandzukic aliweza kufunga kwa kichwa, huku juhudi za kipa Shay Given
kuuzia mpira huo zikikosa kufua dafu.
Lakini juhudi za wachezaji wa Jamhuri ya Ireland hatimaye zilifanikiwa,
wakati Sean St Ledger aliposawazisha. Ireland wakisawazisha bao na kuwa 1-1 kabla ya dhahama kuwaangukia Shabiki wa Jamhuri ya Ireland akiwa katika swaga za aina yake
Hata hivyo, kabla kipenge cha kukamilisha nusu ya kwanza ya mchezo, Nikica
Jelavic alibadilisha matokeo, na kuiwezesha Croatia kuongoza 2-1. Mandzukic aliweza kuandikisha bao la tatu, ambalo mpira uliingia wavuni
ukisindikizwa kimakosa na kipa wa Given. Jamhuri ya Ireland haiwezi kulalamika sana kuhusiana na matokeo ya mechi
hiyo, kwani ilikuwa wazi timu yao bado haijajiandaa vyema. Kabla ya mechi, mashabiki wengi kutoka Jamhuri ya Ireland walikuwa na
matumaini ya kufanya vyema katika mechi hiyo ya kundi C, lakini uwanjani ilikuwa
ni wazi kwamba Croatia ndio timu bora, meneja wao mzoefu, Giovanni Trapattoni,
bila shaka itambidi kufanya kazi ya ziada ikiwa Jamhuri ya Ireland itaepuka
fedheha katika mashindano hayo.
Mabingwa wa Dunia Uhispania wameanza utetezi wa Kombe lao la
ubingwa wa mashindano ya Ulaya kwa sare ya 1-1 dhidi ya Italia katika pambano la
kundi C mjini Gdansk. Barwuah Balloteli akioneshana kazi na Pique
Italia ndiyo iliyotangulia baada ya kipindi cha kwanza kumalizika bila bao
lolote kufungwa na alikua Antonio Di Natale aliyeingia badala ya Balloteli
kufunga bao katika dakika ya 60. Mwachemwache za mashabiki wa Italia
Dakika nne baadaye Mabingwa wa Dunia na Ulaya walifumania lango la Italia na
licha ya juhudi na umahiri wa Mabeki David Silva alimuona Cesc Fabregas na
kumuwekea pasi maridhawa na bila kufanya makosa akaupenyeza mpira kumpita goli
wa Italia Buffon.
Fabregas akiiandikia Hispania bao la kuongoza
Matokeo hayo yanaliweka kundi la C wazi ambapo Italia na Uhispania zinaondoka
zote zikiwa na pointi moja.
Kabla ya mashindano haya wadadisi walionelea kama Uhispania itakabiliwa na
kibarua kigumu kutetea taji lake kutokana na wachezaji wake wengi kuwa wachofu
mno. Jumla ya wachezaji 23 wa timu hii ya Taifa wamecheza jumla ya dakika 89,884
katika msimu uliopita ikilinganishwa na wenzao walioshiriki kwa upungufu wa
dakika 17,000. Walinda milango Iker Casillas wa Hispania na Buffon wa Italia wakipeana pongezi kwa kupangua michomo mikali katika mtifuano wa timu zao
Timu mbili zilizomo kwenye kundi la C Jamhuri ya Ireland na Croatia lazima
zimeridhishwa na matokeo haya zikiona kua na fursa ya kufanya vyema na uwezekano
mkubwa wa kufuzu kutoka michuano ya makundi.
Ujerumani ilianza kampeni yake ya kutafuta kombe la UEFA EURO 2012 kwa ushindi muhimu wa goli moja kwa sifuri dhidi ya Ureno. Nayo Denmark iliiduwaza Uholanzi kwa kuifunga hilo hilo goli moja kwa sifuri.
Ujerumani iliendeleza sifa yake ya kuanza taratibu vinyang'anyiro vikubwa Jumamosi jioni mjini Lviv, Ukraine. Mchezo wa nguvu, wenye mtiririko ambao ulidhihirishwa na Ujerumani katika fainali za kombe la dunia mwaka wa 2010 nchini Afrika Kusini, kwa mfano, ulikosekana hasa katika kipindi cha kwanza. Tulia wewe yangu hiyoo!!! Mwachemwache na udambwidambwi kati ya Christiano Ronaldo na Bastian Jerome Boateng mjerumani mwenye asili ya Ghana akimwaga udambwidambwi
Ni kiungo mshambuliaji pekee Mesut Özil ambaye alionekana kuonyesha ubunifu katika safu ya katikati mwa uwanja kwa upande wa kikosi cha Wajerumani. Lakini wakati Wajerumani wakishjindwa kuonyesha makali, Ureno nayo ilikuwa katika hali hiyo hiyo. Nahodha Cristiano Ronaldo ndiye aliyejaribu tu kuonyesha umahiri wake na kuitatiza Ujerumani, na chanzo kingine cha hatari kilikuwa mchezaji wa ubavuni Nani. Bao la Ujerumani lilitokea katika dakika ya 72 kwa njia rahisi. Bastian Schweinsteiger alikuwa amenyimwa krosi safi katika upande wa kulia, wakati alipoipokea nje ya kijisanduku. Krosi yake ilimgonga mchezaji wa Ureno Joao Moutinho na Gomez akatia kichwa safi hadi pembeni mwa lango. Ujerumani na Uholanzi sasa zitarejesha uhasimu wao wa jadi mjini Kharkiv siku ya Jumatano. Kocha wa Uholanzi Bert van Marwijk anasema hawatavunjika moyo. Kwamba ni lazima waizabe Ujerumani.
Uholanzi yachapwa Katika mchauno wa kwanza, Uholanzi ilipoteza nafasi chungu nzima za wazi katika kichapo hicho ambacho hakikutarajiwa. Nyota kama vile Robin van Persi, ambaye ni mfungaji bora wa ligi ya Uingereza, na Arjen Robben ndio waliofanya makosa makubwa wakati timu hiyo iliposhindwa kutumia nafasi 28 za goli walizopata.
Mhh tumeumbuka!!!!! Ndivyo anavyotafakari Mshambuliaji wa Uholanzi Arjen Robben Hatoki mtu hapa!!! mwachemwache kati ya Bendtner wa Denmark na Heitinga wa Uholanzi
Denmark, ambaye ndiye mshindi wa UEFA EURO 1992, ilijipatia goli mojja safi lililotupiwa kambani na Michael Krohn-Dehli katika dakika ya 24 na kujihakikishia ushindi kwenye kundi B. Awali nchini Poland, shirikisho la soka la Urusi lilishitakiwa na shirikisho la UEFA baada ya ukanda wa video kuonyesha mashabiki wa Urusi wakiwashambulia walinzi wa uwanjani baada ya ushindi wa timu hiyo wa mabao manne kwa moja dhidi ya Jamhuri ya Czech mjini Wroclaw Ijumaa. Wafanyakazi wanne wa usalama walitibiwa hospitalini. Jopo la nidhamu la UEFA litaisikiliza kesi hiyo dhidi ya Urusi Jumatano ijayo. Linatafuta ushahidi zaidi ili kuchunguza madai ya ubaguzi yaliyofanywa dhidi ya wachezaji wa Czech.