Monday, July 2, 2012

SPAIN BINGWA EURO 2012 YAITUNGUA ITALIA 4-0


Uhispania waliandikisha historia kwa maarifa ambayo sio rahisi kuiga, kwa kuitungua Italia magoli 4-0 katika fainali ya Euro 2012 usiku wa Jumapili, mjini Kiev, Ukraine.

Licha ya mchezo mzuri wa Italia, vijana wa meneja wa Uhispania, Vicente del Bosque walithibitisha kwamba kimataifa wanaweza kujigamba wao ndio wenye mchezo bora zaidi duniani, kwa kuzingatia namna walivyoichezea timu ya Italia, na kuwalazimisha kusalimu amri.

David Silva aliifungia Uhispania bao la kwanza, na kabla nusu ya kwanza ya mchezo kumalizika, mchezaji mpya wa Barcelona, Jordi Alba aliandikisha bao la pili, baada ya kukimbia kwa kasi na kumalizia kwa ustadi kabisa.

Ingawa Italia walikuwa na upungufu wa mchezaji mmoja, baada ya kumpoteza mchezaji wa zamu wa tatu Thiago Motta baada ya kujeruhiwa, walicheza kwa bidii, lakini wataalamu wa kandanda kwa upande wa kupokezana mpira, Uhispania, waliwadunisha kabisa.

Fernando Torres aliingia kama mchezaji wa zamu, na akafanikiwa kuubadilisha mchezo, na akiandikisha bao la tatu la Uhispania, kabla ya mwenzake katika klabu ya Chelsea, Juan Mata, kuandikisha bao la nne na la mwisho la Italia, na ambalo bila shaka liliwavunja moyo kabisa mashabiki wote wa Italia.

Mchezo huo bila shaka umeyazima matamshi ya baadhi ya watu ambao awali walimlazimu kocha wa Uhispania Del Bosque na wachezaji wake kujitetea katika mkutano na waandishi wa habari, kabla mechi ya fainali kuanza, kwamba mchezo wao katika mashindano ya Euro 2012 umekosa msisimko.

Lakini usiku wa Jumapili mambo yalikuwa tofauti.

Maarifa yote yaliyowawezesha kuwa mabingwa wa Euro 2008 na vile vile Kombe la Dunia la mwaka 2010 nchini Afrika Kusini yalijitokeza.

Ilikuwa ni fainali ambayo ilimvunja moyo kabisa kocha wa Italia, Cesare Prandelli, lakini bila shaka haikuwa fedheha kushindwa na timu yenye maarifa ya hali ya juu kiasi hicho.

Italia itaweza kujivunia namna ilifika katika fainali, licha ya kushindwa kwa magoli mengi na timu ambayo ilikuwa ni wazi imo katika kiwango cha pekee.

Tulia ngedere weeee!! Kazi kati ya Pique na Balotelli


Kambaa..David Silva akianza kuwatia njaa Italia





Friday, June 29, 2012

RIDHIWANI KIKWETE AFANYIWA KITU MBAYA


Ridhiwani Kikwete akiwa na mwendeshaji The Mboni Show, Mboni Masimba

Katika dunia ya leo maendeleo ya sayansi na teknolojia yamekuwa yakileta tija kila kukicha na kukuza ustawi wa jamii mbalimbali. Kwa kuizungumzia teknolojia ya mawasiliano ambayo imekuwa kwa kasi na kuifanya jamii yetu kuishi maisha ya kisasa ambayo kila kazi imerahisishwa, Maendeleo hayo yamewezesha jamii mbali mbali kubadilishana ujuzi na kuvumbua vitu vipya kila kukicha na kutokana na ukweli juu ya utendaji wa teknolojia hizo sasa dunia imekuwa ni ndogo mno yaani kama kijiji kimoja ambapo watu wanaweza kufanya shughuli mbalimbali bila kujali umbali waliopo baina yao na haya yote ni matunda ya Maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano.

Maendeleo hayo na faida zote pia kuna madhara ya matumizi ya teknolojia hizo hususani za mawasiliano ambapo katika dunia ya sasa kuna mitandao ya kijamii ambayo huwaweka watu karibu zaidi, Na miongoni mwa wahanga wa madhara ya teknolojia hizi ni Ridhiwani Kikwete ambaye ni mtoto wa Rais wa Tanzania Mh Dk Jakaya Mrisho Kikwete.

Akizungumzia yaliyomsibu kutokana na teknolojia ya mawasiliano wakati akihojiwa katika kipindi Cha The Mboni Show kinachoendeshwa na Mboni Masimba na kurushwa na kituo bora kabisa kwa vijana wa kisasa cha East Africa (EATV), Ridhiwani alisema maendeleo ya teknolojia yamemuathiri pale account yake ya mtandao wa Kijamii wa FACEBOOK (ambao umejizolea umaarufu mkubwa ulimwenguni kwa hivi sasa) ilipovamiwa ama kupokwa na wahalifu wanaojulikana kama kitaalamu kama "HACKERS". Walitumia utaalamu wao na kujimilikisha account hiyo na kupost status ambayo ilizua utata mkubwa kwa Ridhiwani na familia yake.

Akielezea kuhusu mkasa huo anasema baada ya ile status kuonekana akiwa hajui hili wala lile alipokea simu usiku wa saa saba, na mara alipopokea hakupata hata salamu na neno la kwanza akaulizwa,"Hivi wewe zinakutosha?" alipatwa na mshangao asijue la kufanya. ndipo alipoingia kwenye internet akagundua kuwa kuna kitu kimefanyika kwenye account yake ya FACEBOOK.
Baada ya kufuatilia sana wale wote waliodhani kuwa maneno yale aliyaandika Ridhiwani waligundua kuwa kweli sio yeye bali kuna wahalifu wa mitandaoni ndio waliomfanyia kitendo kile.
Ridhiwani anasema "haiingii akilini,Rais ni baba yangu halafu niseme maneno kama yale, na itakuwa ni usaliti kwa Chama changu kwani mimi ni mwanachama wa CCM,Hata kama nawapenda wapinzani siwezi kusema kwenye internet nitakaa nalo moyoni"

Wageni wa The Mboni Show kushoto Ridhiwani Kikwete,Mboni,Barnaba na Lisa Jensen


Mboni Masimba katikati akiwa na wageni wake Ridhiwani na Lisa Jensen






Linsa Jensen na Barnaba wakisalimiana na mashabiki waliohudhuria kipindi cha The Mboni Show

BALOTELLI AWALIZA WAJERUMANI AIPELEKA ITALIA FAINALI EURO 2012


Mpira uliopigwa na Balotelli ukitinga kambani kuandika bao la kwanza

Barwuah Balotelli alitupia kambani magoli mawili ya kupendeza mno na kuiwezesha timu yake ya Italia kuishangaza na kuiacha kinywa wazi Ujerumani kwa kuitandika magoli 2-1 katika nusu fainali ya Euro 2012, na kujihakikishia nafasi ya kucheza mechi ya fainali mjini Kiev dhidi ya Uhispania.

Mabao ya mtukutu huyo wa klabu ya Manchester City ya England, alitupia goli la kwanza wavuni kwa kichwa, na la pili kwa mkwaju wa kasi mno katika uwanja wa mjini Warsaw, na Italia kuwathibitishia Wajerumani katika kipindi cha kwanza kwamba ilikuwa na nia kamili ya kufika fainali.
Wajerumani, kufuatia mshituko, walianza kucheza kwa makini zaidi, lakini bao lao la penalti, ambalo lilipatikana katika dakika ya 92, kupitia Mesut Ozil, lilichelewa mno, na halikuweza kuwaokoa.

Italia kamwe hawajawahi kushindwa na Ujerumani katika mashindano makubwa, na wamefanikiwa sasa kucheza mechi nane dhidi ya Ujerumani pasipo kushindwa.

Hii sasa itakuwa mara ya tatu kwa Italia kuingia fainali za michuano hii ya mataifa ya Ulaya, na wataingia fainali kama timu inayodhaniwa kuwa dhaifu ikilinganishwa na mabingwa watetezi Uhispania.

Timu hii ya meneja Cesare Prandelli ilistahili ushindi, kwani sio tu waliweza kupambana na Ujerumani ambayo iliwashinda wapinzani wao kwa urahisi, bali pia walifunga mabao yao mapema katika kipindi cha kwanza.

Timu hiyo ya Azzurri ilikuwa na nafasi ya kujiongezea magoli, lakini ilicheza kwa tahadhari kwa kuhofia kwamba iwapo ingeliongoza mashambulizi zaidi dhidi ya Italia, kulikuwa na uwezekano wa ngome yao kuachwa ikiwa dhaifu, na Wajerumani kuwashambulia.

Italia 2-1 Ujerumani


Mtaalamu Pirlo akiyoyoma na mpira


Balotelli akishangilia bao la pili


Gomez akipiga kichwa kilichopaa golini


I am superman...Balotelli akitunisha misuli baada ya kutupia kambani bao maridhawa


Ukiujua ni raha sana..kama nnaliaaaaaaaa!!!


Viti vya moto..wajerumani wamesepa!!!


Mesut Ozil



Wera weraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!


Mlinga mlango wa Italia Gianluigi Buffon akishangilia ushindi dhidi ya Ujerumani



Muuaji wa Ujeruman Barwuah Balotelli akishangilia ushindi mwanana



Thursday, June 28, 2012

SUMMER SUMMA-C.KHiD


USIENDESHE GARI KARIBU NA MAGARI YALIYOPAKIA MAKONTENA (ANGALIZO)

www.dilsedesi.org
Gari kubwa lililobeba kontena likiwa limeliangukia gari dogo!!

www.dilsedesi.org
Mashuhuda na waokoaji wakiwajibika kujaribu wawezalo kuokoa maisha ya watu..mhhh itakuwa ngumu hapa mtu kuchomoka.

www.dilsedesi.org
Sehemu ya mbele ya gari dogo lililoangukiwa na kontena linavyoonekana. Ina maana jamaa alichoambulia kizima ni 'plate number' tu.

www.dilsedesi.org
Mmoja kati ya timu ya waokoaji akiwa hajui aanzie wapi na aishie wapi jinsi vigari vilivyosagwa na kontena.

www.dilsedesi.org
Watu wa huduma ya kwanza wakijaribu kuokoa maisha kwa kumuwekea maji majeruhi wa ajali hiyo huko Indonesia.

www.dilsedesi.org

www.dilsedesi.org
Hakuna mwenye uhakika kuwa atapona au la!!!

61 Easy Ways To Lose Weight

61 Easy Ways To Lose Weight

URENO YATOLEWA KAMASI NA SPAIN, SPAIN YATINGA FAINALI EURO 2012


Andre Iniesta akijaribu kumtoka beki wa Ureno.

Mhhh sikio la kufa halisikii dawa.....C.Ronaldo akiwa ameduwaa baada ya kipigo

Mabingwa watetezi Uhispania wametinga fainali ya EURO 2012 baada ya kuifumua Ureno 4-2 katika changamoto za mikwaju ya penalti, baada ya dakika 90 na dakika 30 za ziaida kumalizika kwa timu hizo mbili kushindwa kufungana.

Bao la penati la mwisho lilitupiwa kambani kwa umaridadi mkubwa na Cesc Fabregas, na kuwapa wenzake matumaini ya kutetea ubingwa wa EURO 2012  na sasa wanasubiri mshindi katika nusu fainali nyingine  leo  kati ya Ujerumani na Italia katika fainali ya Jumapili.

Fabregas, ambaye ni kiungo wa  kati wa timu ya Barcelona, alipiga mkwaju ambao baada ya kugonga mwamba upande wa kushoto, ulitambaa wavuni, na ikawa ni tiketi ya Uhispania kufanya mipango ya kusafiri hadi Kiev, Ukraine, katika mchezo wa fainali.

Mchezaji wa Ureno, Bruno Alves, alielekea kuwa na wasiwasi, na kushindwa kufunga mkwaju wake, baada ya mpira kugonga mwamba, na Ronaldo, akiwa amepangwa na timu yake katika nafasi ya tano kwa wapigaji penalti, hakupata hata nafasi ya kutimiza wajibu huo.

Wengine waliokosa kufunga kupitia mikwaju ya penalti ni mchezaji wa Ureno, Joao Moutinho, wakati kipa wa Uhispania, Casillas, alipoweza kuokoa kwa kuruka upande wa kkulia.

Awali mchezaji wa Uhsipania Xabi Alonso naye alikosa kutupia kambani  mkwaju wa penalti, licha ya kwamba ulikuwa ni mkwaju wa kasi na uliopigwa kwa nguvu, lakini kipa Rui Patricio akaunyaka.

C.Ronaldo akijiangusha katikati ya mabeki Pique na Silva


Luis Nani wa Ureno akijaribu kukukuruka katika mechi hiyo


Beki wa Ureno Contrao akitunishiana misuli na D.Silva wa Uhispania


Beki wa Spain Gerald Pique akimmudu ipasavyo Christiano Ronaldo wa Ureno

URENO Vs UHISPANIA