Monday, December 17, 2012

KINA DADA/MAMA FUNGA MWAKA NA STYLE MPYA YA RANGI ZA KUCHA

 


WANYAMA NAO SIKUKUU YA X-MAS INAWAHUSU







































CORINTHIANS YAIDUNGUA CHELSEA FAINALI YA KOMBE LA KLABU BINGWA YA DUNIA

Klabu ya Corrinthians kutoka Brazil, imeibuka kidedea katika michuano ya kuwania kombe la klabu bingwa duniani baada ya kuidungua Chelsea ya Uingereza kwa bao moja kwa "nunge" katika mechi ya fainali iliyochezwa nchini Japan.
Paolo Guerrero ndie aliepeleka msiba Uingereza akitupia bao la pekee na la ushindi kwa Corinthians.
Hata hivyo Chelsea, ilipoteza bafasi nyingi za kufunga wakati wa mechi hiyo pale washambuliaji wake walipokuwa wakipepesa macho na kutetemeka miguu kutupia kambani pindi wanapofika katika eneo la hatari la Corinthians.
Katika muda wa ziada Fernando Torres, alipoteza nafasi nzuri sana ya kuzawazisa licha ya kuwapiku walinzi wa Corinthians na kubakia yeye na mlinda mlango Cassio alieonekana "mnoko" kwa kuchomoa hatari nyingi zilizoelekezwa langoni mwake ambapo Torres alijaribu kumlamba chenga kipa huyo wa Corinthians na kuachia fataki lakini kombora lake likawa hafifu na kudakwa kwa urahisi na kipa.

Chelsea ilimaliza mechi hiyo ikiwa na wachezaji kumi baada ya Gary Cahil, kupewa kadi nyekundu baada ya kumfanyika madhambi mchezaji wa Corrinthians Emerson.
Bao la chelsea lililofuingwa kwa kichwa na Fernando torres lilikataliwa na hivyo vijana hao kutoka brazil wakaibuka na ushindi.

Paolo Guerrero akitupia bao pekee kwa kichwa katika mpambano huo...mtazame Ramires na Ashley Cole wanatamani waudake lakini waaaapi baaadae sanaaaa!!



Guerrero akishangilia goli huku Ashley Cole akisafisha vyombo kambani na David Luiz akiwa tayari kumsaidia.


Ashley Cole akimthibiti Henrique

Hazard akipata kichapo..hapa braza mawili, mpira ubaki wewe uende au mpira uende wewe ubaki..upo!?


Tulia nimwage majaro weweee...


Aiyaaaaaaah tumekosa!!?? Tulieni nyinyi tumetumwa kombe sisi alaaaaahh


Wachezaji wa Corinthians wakiwashukuru mashabiki kwa support baada ya mtanange kuisha


Inauma sana unajuaa . Nahodha wa Chelsea Frank Lampard akiwa na majonzi ya kulikosa kombe.


Emerson wa Corinthians akimfariji Mbrazil mwenzake Ramires..ndio ukubwa kaka kama vipi rudi home ushangilie makombe.



Kazi tuliyotumwa kutoka Brazil imetimia hureeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!

Friday, December 14, 2012

KOCHA WA PSG YA UFARANSA KUMRITHI MILOVAN SIMBA S.C

Mabingwa wa Soka Tanzania,Bara Simba S.C  imemtangaza Patrick Liewig ambaye ni raia wa Ufaransa kuwa kocha mpya baada ya kusitisha mkataba na kocha wa sasa Mserbia Milovan Cirkovic. Liewig ameshazifundisha PSG ya Ufaransa, Club African ya Tunisia pamoja moja klabu kubwa barani Afrika ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast. Anatarajiwa kutua nchini baada ya wiki 2 kuanza kukinoa kikosi cha wekundu hao wa Msimbazi.

Wasifu wa Lewig
Date of birth:04.10.1950
Age:62
Nationality:-France
ΓΈ-Incumbency as manager:1,97 Years
success-ratio as manager:30,77 % Wins
38,46 % Draw
30,77 % Loss
Preferred formation:4-2-3-1
 



Patrick Liewig

WIMBO WA LEO-Hatuna Habari nao (Abdu Kiba)


KASEJA APATA MRITHI KUTOKA UGANDA

Mabingwa wa Soka Bara, Simba wamekamilisha usajili wa mrithi wa kipa Juma Kaseja, Mganda Abbel Dhaira.

Dhaira amesaini mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya dola 40,000 (Sh43 milioni) na mshahara wa mwezi Sh2 milioni mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hanspope.

Kusajiliwa kwa kipa huyo kunakuja baada ya muda mrefu mashabiki wa Simba kuhoji kiwango cha Kipa Juma Kaseja.
Kaseja alikuwa gumzo kwa mashabiki wa Simba katika mechi za mwisho za duru la kwanza Ligi Kuu akituhumiwa kufungwa mabao ya kizembe.
Akizungumza jana baada ya kukamilika kwa usajili wa Dhaira, Hanspope alisema wanajivunia kupata kipa mwenye umbo kubwa kama Mohamed Mwameja aliyewahi kuidakia klabu hiyo.

Hanspope alisema kusajiliwa kwa kipa huyo Mganda kulitokana na mapendekezo kutoka kwa kipa wao wa kwanza hivi sasa, Kaseja.
“Kaseja ndiye aliyependekeza kwa uongozi kumsajili kipa huyu. Tunaamini mawazo yake yataisaidia Simba kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake, Dhaira alisema amefurahi kusajili Simba akiamini ni moja ya timu kubwa Afrika.
“Nimekuwa nikiisikia Smba kwa muda mrefu, nafahamu ni moja ya timu nzuri Ukanda wa Afrika Mashariki na Afrika kwa jumla,” alisema kipa huyo.



Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba S.C Zakaria Hanspope akimkaribisha Abbel Dhaira


Golikipa kutoka Uganda Abbel Dhaira akiangusha saini na Dole gumba kuichezea Simba S.C kwa nyundo mbili



Abbel Dhaira akifanya vitu vyake uwanjani

Wednesday, December 12, 2012

TYSON SASA NI MWANAMKE ASEMA TOKEA ZAMANI ALITAMANI KUWA MWANAMKE

BINGWA maarufu wa zamani katika masumbwi wa uzito wa juu duniani, Mike "IRON" Tyson, anasemekana yuko katika hali nzuri baada ya kujibadili na kuwa mwanamke katika operesheni aliyofanyiwa huko Beverly Hills, Marekani, hivi karibuni ambapo amebadili jina na anajiita Michelle.
Kuna wakati Tyson alikuwa anajulikana kama “Mtu mwenye sura mbaya zaidi duniani”!sasa ni Dem inakuwaje?


MIKE TYSON sasa anaitwa MICHELLE

“Watu wanaona ni ajabu mie kuwa mwanamke hivi sasa,” alisema Tyson ambaye aliwahi kufungwa kwa kubaka, na ambaye amefanyiwa mabadilko kadhaa ya uso, pua na viungo vingine kwa masaa 16. Aliongeza kwamba: “Hata nilipokuwa bondia nilikuwa natamani sana kuwa na matiti na nyeti za mwanamke.”
Iron Mike au Iron Maiden kama anavyojulikana sasa aliyasema hayo akiwa ametulia huku amevaa wigi la kike, suruali ya ‘jeans’ ya bluu na T-shirt yenye picha ya Vanessa Bruno ambapo alidokeza kwamba mara sehemu zote nyeti za kike zitakapojitokeza atawadhihirishia Wamarekani kwamba yeye si “mvulana mbaya” tena.
Amesema ameutunza uume wake ulioondolewa katika chupa ili kuwakumbusha wabaya wake waliokuwa wakimfanyia vitendo vya kuchukiza yeye na “wavulana wazuri” wengine huko gerezani.
Japokuwa wachambuzi wa masuala ya ndondi mwanzoni walishangazwa na maneno hayo ya Tyson, wengi wamekiri kwamba alama za yeye kupenda hivyo zilikuwepo.

Mtu Mmoja amesema kwamba: “Huko nyuma, alikuwa anapenda sana kuvaa sana glovu za kike, viatu virefu vya ngozi vya kike na magauni ya hariri, na pia alikuwa ni mtu mwenye kupenda sana heleni.” 


TYSON(MICHELLE) ENZI ZAKE ULINGONI

TYSON (KUSHOTO) AKIKABILIANA NA BRUNO (KUSHOTO)

SIKU TYSON ALIPOMNG'ATA SIKIO EVANDER