Monday, December 24, 2012
CHELSEA YAIRARUA ASTON VILLA 8-0 HUKU SWANSEA WAKIIKALIA KOONI MAN UNITED
Chelsea imeiangushia kipigo kizito Aston Villa kwa kuicharaza
magoli 8-0 katika mechi ya ligi kuu ya England, iliyochezwa katika uwanja wa
Stamford Bridge, Jumapili.
Fernando Torres, ndiye aliyeanza kufungua karamu ya magoli kwa vijana wa Rafael Benitez, pale alipopachika bao katika dakika ya tatu ya mchezo.
David Luiz kiungo mahiri aliongeza goli la pili katika dakika ya 29 huku Branislav Ivanovic akishindilia goli la tatu kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika.
Ivanovic akitupia kwa kichwa goli la pili
Frank Lampard alifungua kipindi cha pili kwa bao lake la dakika ya 58 huku Ramires akifunga magoli mawili, na mengine yakifungwa na Oscar, Eden na Hazard wakifunga kila mmoja goli moja moja.
Ushindi huo umezidi kuiimarisha Chelsea katika nafasi ya tatu ya ligi kuu ya England ikiwa na pointi 32 katika mechi 17 ilizocheza.
Katika mchezo mwingine uliochezwa Jumapili, vinara wa ligi hiyo Manchester United walitoka sare ya bao 1-1 na Swansea.
Patrice Evra aliifungia timu yake bao la kuongoza katika dakika ya 16 kwa njia ya kichwa kufuatia kona iliyochongwa na Robin van Persie.
Hata hivyo Michu aliisawazishia Swansea katika dakika ya 29.
Mpaka sasa Manchester United inaongoza ligi kuu ya England ikiwa na pointi 43 katika michezo 18, ikifuatiwa na Manchester City yenye pointi 39 na Arsenal imejikita katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 30.
Michu akiisawazishia Swansea
Wayne Rooney akikukuruka
Michu akishangilia goli
Patrice Evra akishangilia goli
CHELSEA 8-0 ASTON VILLA
SWANSEA 1-1 MAN UNITED
Friday, December 21, 2012
VIDEO KALI ZA BONGO FLAVOUR MWAKA 2012
Baadae-Ommy Dimples
Nai nai-Ommy Dimples Ft AliKiba
ME n U-Ommy Dimples Ft Vanessa Mdee(audio)
Marry ME-Rich Mavoko
Silali-Rich Mavoko
Mapito-Mwasiti Ft Ally Nipishe
Samboira-Ben Pol
Nikikupata-Ben Pol
Pete-Ben Pol
Mawazo-Diamond Platinum
Nataka Kulewa-Diamond Platinum
Leka Dutigite-Kigoma All Stars
Aifora-Linex
Mwanayumba-Chegge
Dear God-Kala Jeremiah
Ya Moyoni-Dogo Janja Ft PNC
Single Boy-Lady Jay Dee Ft AliKiba
Njalo-Lady Jay Dee
Hatuna Habari nao-Abdu Kiba
Sondella-Sharo Milionea
Chuki Bure-SharoMilionea Ft Dully Sykes
Lawama-Shilole Ft Q Chief
Nidanganye-Shetta
Dem sio-Tunda Man
Amekua-Tunda Man
Starehe Gharama-Tunda man
Milele Daima-Barnaba
Gube Gube-Barnaba
Nabembelezwa-Barnaba
Oliver Twist remix-Linah
Bora Nikimbie-Linah
Tushukuru kwa Yote-Lameck Ditto
Wapo-Lameck Ditto
Kabwela-Momba Ft Ney wa Mitego
Mi Sio Sharobaro-Momba
Nichum-Bob Junior
Nanini-Bob Junior
GODBLESS LEMA AIBUKA KIDEDEA ARUDISHIWA UBUNGE

Lema akiwa na Freeman Mbowe,Nassari na Mnyika mahakamani leo asubuhi kusikiliza matokeo ya kesi ya Lema ambapo Lema aliibuka kidedea

Furaha pamoja na wafuasi wa CHADEMA baada ya kushinda rufaa.
Thursday, December 20, 2012
RATIBA KAMILI 16 BORA UEFA CHAMPIONS LEAGUE
RATIBA 16 BORA LIGI YA MABINGWA ULAYA
Wednesday, December 19, 2012
INDIA Vs CHINA
|
KUUNGANISHA UMEME SASA BEI CHEE
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), limetangaza rasmi kupunguza viwango vya kuunganisha umeme kuanzia Januari Mosi, 2013 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo aliyoitoa katika Bunge la Bajeti lililopita.
Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud amesema kupunguzwa kwa viwango hivyo kutasaidia wananchi wengi kuunganisha umeme.
Badra alisema gharama za kuunganisha umeme vijijini katika umbali usiozidi mita 30 bila nguzo sasa itakuwa Sh177,000 na wateja wa mijini watatakiwa kulipia Sh320,000 badala ya Sh455,108 za sasa akisema punguzo hilo ni sawa na asilimia 61.11 kwa wateja waishio vijijini na asilimia 29.48 kwa wateja wa mijini.
Alisema kwa wateja wanaoishi vijijini wanaohitaji umeme wa njia moja na nguzo moja watatakiwa kulipia Sh337,740 wakati wale wa mijini watalipia Sh515,618 badala ya Sh1,351,884 zinazolipwa na wateja hivi sasa.
“Punguzo hilo ni sawa na asilimia 75.02 kwa wateja waishio vijijini na asilimia 61.86 kwa wateja waishio mijini.”
Alisema wateja wa vijijini watakaojengewa njia moja na nguzo mbili watatakiwa kulipia Sh454,654 na wa mijini watalipia Sh696,670, badala ya Sh2,001,422 ambazo zinalipiwa hivi sasa.Alisema punguzo hilo ni sawa na asilimia 77.28 kwa wateja waishio vijijini na asilimia 65.19 kwa wateja wa mijini.

Meneja mawasiliano wa Tanesco,Badra Masoud akifafanua jambo.

Subscribe to:
Posts (Atom)