Thursday, March 28, 2013

UEFA WAMFUTIA ADHABU IBRAHIMOVIC KUIVAA BARCELONA


 Zlatan Ibrahimovic

Kamati ya nidhamu ya UEFA imemfutia adhabu mshambuliaji mahiri wa Paris Saint German Zlatan Ibrahimovic huku akiwa tayari ametuikia kwa kukosa mechi moja dhidi ya Valencia. 
Kutokana na kufutiwa adhabu hiyo sasa atakuwemo kwenye kikosi cha PSG kitakachoivaa Barcelona katika mchezo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya wiki ijayo.




MANDELA HALI TETE ARUDISHWA HOSPITALI

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amelazwa tena hospitalini baada ya kuugua ugonjwa wa mapafu kwa mara nyingine.
Taarifa kutoka kwa serikali ya nchi hiyo, ilisema kuwa Mandela mwenye umri wa miaka 94 alilazwa hospitalini muda mfupi kabla ya saa sita usiku.







Nelson Mandela

Mandela alilazwa siku kumi na nane hospitalini mwezi Disemba mwaka jana kupokea matibabu ya ugonjwa wa mapafu na kibofu.
Anasifika sana kama baba wa taifa hilo kwa kuongoza vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi.
Kadhalika Mandela alihudumu kama rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini tangu mwaka 1994 hadi mwaka 1999, ingawa hali yake ya kiafya imezua wasiwasi kwa muda sasa.
Rais Jacob Zuma alimtumia taarifa ya kumpa pole na kumtakia kupona Mandela
"tunawataka watu wa Afrika Kusini pamoja na duniani kote kuwa watulivu na kumuombea Madiba na familia yake. Tuna imani kuwa kikosi cha madaktari wanaomtibu Mandela watafanya kila hali kuhakikisha anapona,'' alisema Zuma katika taarifa yake.
Mapema mwezi huu bwana Mandela alilazwa hospitalini mjini Pretoria baada ya kufanyiwa ukaguzi wa kiafya.

Tuesday, March 26, 2013

WEMA WA WEMA WAMRUDISHA KAJALA URAIANI


Kajala akimkumbatia Wema Sepetu kwa machozi ya furaha baada ya kumtolea faini ya milioni 13 na kumuepusha na kifungo cha miaka 8 jela baada ya kupatikana na hatia ya kula njama ya kubadilisha umiliki wa nyumba na kosa jingine la kushiriki kusafisha pesa chafu ambacho ni kinyume cha sheria.


Kajala na Wema nje ya mahakama.

Kajala akiwa na Lulu akizungumza na waandishi wa habari.

Kajala na Dk Cheni nje ya mahakama baada ya hukumu.


Thursday, February 21, 2013

AC MILAN YAITEPETESHA BARCELONA 2-0

Timu ngumu ya Barcelona ya Uhispania jana ilitepeteshwa na vigogo wa soka wa Italia AC Milan kwa bakora 2 kwa buyu katika dimba la San Siro, huku mtanange huo ukishuhudiwa na mashabiki 75,000 akiwemo Mario Balotelli na mchumba wake pamoja na masela kibao.

Mtanange huo ulitawaliwa na Barcelona lakini walishindwa kabisa kuipenya ngome ya AC Milan waliokuwa wanalinda lango lao na kufanya mashambulizi ya kushtukiza na ya kasi. AC Milan walianza kuwazidi akili Barcelona katika dk 56 pale mzaliwa wa Ghana Kevin Prince-Boateng alipotupia kambani goli la kuongoza na kulipua nderemo na vifijo toka kwa mashabiki9 waliofurika katika dimba la San Siro.

Barcelona walihaha kusawazisha goli bila mafanikio kabla ya kutepeteshwa kwa bao la pili katika dk 80 likitupiwa kambani na Raia wa Ghana Suley Muntari.

Mchezaji mtukutu aliesajiliwa hivi karibuni na AC Milan akitokea Manchester City ambae nae pia ni mchezaji mwenye asili ya Ghana Mario Barwuah Balotelli alionekana uwanjani akiwa na mchumba wake na kundi la masela wakishangilia ushindi wa AC Milan kwa hisia kali.

Boateng na Muntari wakishangilia goli la kwanza

Nimeuaaaaaaaaaaaaaaaaa

Kazi kweli kweli Iniesta na Boateng

Mungu wangu tumetepeteshwa namna hii...

Messi akijaribu kuchanja mbuga

Kamata mwizi meeeeeeeeeeeeen!! Boateng akijaribu kumchimoka Puyol

Kulala kwenuu..Messi na Alves wakiwa chini kufuatia patashika nguo kuchanika ya mpambano huo

Muntari akiachia kombora kuandika bao la pili dk 80

Muntari na Boateng wakishangilia goli la pili
 


Balotelli na mchumba wake wakifuatilia mpambano

Wednesday, February 20, 2013

BAYERN YAISULUBU ARSENAL

Timu ya soka ya Bayern Munich ya Ujerumani imeisulubu Arsenal ya Uingereza katika mpambano wa kwanza wa klabu bingwa ya Ulaya katikla dimba la Emirates huku mashabiki wapatao 59,974 wakishuhudia fedheha ya kichapo cha mabao 3-1.

Magoli ya Bayern yalifungwa na Kroos dk 6 kabla Thomas Muller kuongeza la pili dk 20 mpaka mapumziko magbao yalikuwa 2-0. Kipindi cha pili kama Arsenal waliamka vile lakini waaap pamoja na kupata bao la kufutia machozi katika dk 54 lililotupiwa na Podolski kwa kichwa baada ya kipa wa Bayern kufanya makosa katika kudaka mpira wa kona, na dk 76 Mandzukic alipeleka kilio London kwa kutupia kamba ya tatu.


Kroos akifunga goli la kwanza


Muller akitupia la pili

Mandzukic akitupia la tatu

Wilshere na Shwerzteinger

Twendeni tumeshapigwa

Pole mzee wenger unayataka mwenyewe nyoooooo!
ARSENAL 1-3 BAYERN MUNICH