Wednesday, May 29, 2013

REST IN PEACE ALBERT MANGWAIR

 
 Albert Mangwair enzi za uhai wake

Mwanamuziki wa Hip-Hop ALBERT MANGWAIR amefariki dunia jana usiku huko Afrika Kusini katika hospitali ya Hellena Joseph.
Alikuwa Ghetto Moja Na Msanii M To The P. Walivyokwenda Kuwagongea Asubuhi Walikuta Ngwear Amefariki Na M To The P Amepoteza Fahamu Kabisa. 
Pia Daktari Ameshatoa Taarifa Kwa Watu Wa Karibu Wa Ngwear Huko South Africa.  
Ngwea akiwa na msanii M to the P. mtu wa karibu anasema walitakiwa kurudi Dar leo lakini waliwakuta wamezima kwenye room wote wawili baada ya kuji overdose madawa ya kulevya na M to the P yupo hoi hospitali.
Mwili wa marehemu upo katika hospitali ya Hellene Joseph. 
 
 
 
Mangwair akifanya makamuzi stejini enzi za uhai wake

Tuesday, April 23, 2013

NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA 2013..LEO NI LEO!

 
Vita kusaka tiketi ya kusafiri kwenda jijini London kwenye mchezo wa fainali wa klabu bingwa barani Ulaya inaanza usiku huu kati ya Mabingwa wa soka nchini Ujerumani dhidi ya inayotajwa kuwa timu bora kwa vilabu vya soka duniani kwa wakati huu FC Barcelona.
Kocha wa Bayern Munich, Jupp Heynckes amesema haogopeshwi na urejeo wa nyota wa Barcelona, Lionel Messi kuelekea mchezo huo wa kwanza wa nusu fainali ya klabu bingwa barani Ulaya.
Messi hajacheza mchezo wowote wa Barcelona toka alipoingia kama mchezaji wa akiba na kuisaidia timu yake kufuzu nusu fainal katika mchezo robo fainali dhidi ya Paris St-Germain ya Ufaransa. Lakini kuna kila dalili Muanjetina huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye ndiye mchezaji bora wa dunia kwa sasa,akajumuishwa kwenye kikosi cha Barcelona kwenye mchezo wa usiku wa leo.
Mwezi uliopita Messi aliweka rekodi kwenye ligi ya Hispania kwa kuwa mchezaji aliyezifunga timu zote zinazoshiriki ligi kuu nchini humo maarufu kama La Liga kwa misimu miwili mfululizo.
Barcelona inapambana kutaka kutwaa taji la tatu la klabu bingwa barani Ulaya ndani ya miaka mitano,Huku Bayern Munich ambao msimu ujao watakuwa chini ya aliyekuwa kocha wa Barcelona, Pep Guardiola, wao wanapambana kutafuta nafasi ya kucheza fainali yao ya tatu ndani ya miaka minne.
 

Kocha wa Bayern Munich, Jupp Heynckes ambaye aliwahi kuwafundisha mahasimu wa Barcelona, Real Madrid amesema licha ya kumheshimu mrithi wake wa kiti cha ukocha kwenye timu hiyo lakini hajaomba ushauri wowote kutoka kwa Guardiola na amejiandaa kwa kila namna kuhakikisha anaifunga Barcelona usiku huu. Aliongeza kwa kusema anaijua vizuri sana timu yake kuliko mtu yeyote na anafahamu soka ya Hispania na Barcelona wenyewe kwa undani mkubwa.
Wakati Barca wakiwa hawajaweka wazi kama watamuanzisha Messi au la, Baadhi ya wachezaji wa Barcelona akiwemo Xavi Hernandez alinukuliwa siku ya jumatatu akisema, kombe la ligi kuu nchini Hispania, La Liga lina umuhimu mkubwa kuliko klabu bingwa barani Ulaya.
Mechi hiyo itachezwa kwenye uwanja wa Allianz Arena mjini Munich nchini Ujerumani,majira ya saa nne kasorobo usiku kwa saa Afrika Mashariki.

Wednesday, April 17, 2013

BIBI KIDUDE AFARIKI DUNIA

Mwanamuziki gwiji nchini Fatuma Binti Baraka "Bi Kidude" hatunaye tena. Taarifa toka kwa familia yake zinasema Bi Kidude aliekuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Hindu Mandal amefariki leo. Bi Kidude atakumbukwa kama mwanamuziki mkongwe zaidi nchini ambaye alianza muziki akiwa na umri wa miaka 10 tu na aliwahi kupokea tuzo mbalimbali kutokana na mchango wake katika muziki wa mahadhi ya mwambao. Hakika sanaa nchini imepoteza moja ya nguzo kubwa.

Pumzika kwa amani Fatuma Binti Baraka.
 
 

 

Friday, April 12, 2013

RATIBA NUSU FAINALI UEFA 2013



SF 1

BayernBayern(GER)
v
BarcelonaBarcelona(ESP)

SF 2

DortmundDortmund(GER)
v
Real MadridReal Madrid(ESP)

Wednesday, April 3, 2013

BALAA LA KHANGA MOKO HILI HAPA





Balaa linaanza mtu anamwagiwa Kinywaji kwenye makalio ooo maaamaaa
  
Sasa ni ndembendembe

Balaa hilo mie simoooo

Twende kazi..asie na mwana aeleke jiwe

PSG YAIKOMALIA BARCELONA, BAYERN YAITUNGUA JUVENTUS



Messi akitupia kambani goli la kwanza Katika dakika ya 37 kabla Zlatan Ibrahimovic hajaisawazishia PSG katika dk 78. Na Barcelona waliongeza bao la pili likitupiwa kambani na Xavi kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 88 lakini PSG walikomaa na kusawazisha katika dakika ya 90 bao la nduki kali ya Matuidi. Mpambano huo ulihudhuriwa na mashabiki wapatao 45,000.

Ibrahimovic akishangilia goli la kwanza la kusawazisha


Iniesta chini ya ulinzi mkali


Goli la pili na la kusawazisha la PSG likitinga wavuni

Mfungaji wa goli la kusawazisha la PSG Matuidi akishangilia


Messi na Beckham shughuli pevu

Messi baada ya kuumia akijiandaa kutoka nje
 
PSG 2-2 BARCELONA


 Katika robo fainali nyingine ya kwanza timu ngumu ya Ujerumani Bayern Munich waliiadabisha Bibi kizee wa Turin,Juventus kwa bao 2-0. Goli la kwanza likifungwa na Alaba dakika ya 0, Na sio mwingine alietupia msumari wa pili bali ni Thomas Muller katika dakika ya 62.

  
 
Nimetupiaaa..Alba akishangilia baada ya kufunga goli la mapema mno katika dakika ya 0.
  
Robben chini ya ulinzi
 
BAYERN 2-0 JUVENTUS

Tuesday, April 2, 2013

CHELSEA YAIPIGA MAN UNITED CHA NGURUWE KOMBE LA FA

Timu ya soka ya Chelsea imeisambaratisha timu ngumu ya Man united katika kombe la chama cha soka cha Uingereza FA kwa bao moja kwa nunge katika dimba la Stamford Bridge, ukiwa ni mchezo wa marudiano baada ya mchezo wa kwanza uliopigwa katika dimba la Old Trafford kuisha kwa matokeo ya sare ya 2-2.


 
Demba BA akifunga goli pekee

Katika mchezo huo uliohudhuriwa na watazamaji wapatao 40,704 walishuhudia mtanange wa kukata na shoka. Wenyeji walionja tamu ya mtanange huo pale Mshambuliaji raia wa Senegal Demba BA alipofunga goli maridadi baada ya kutanguliziwa pande murua na Juan Mata katika dakika ya 48 ya mtanange huo. Goli hilo lilidumu mpaka mtanange unamalizika na hivyo Man United kuondoshwa katika michuano hiyo ya FA na kuiacha Chelsea kusonga mbele.

Wachezaji wa Chelsea wakimpongeza Demba BA baada ya kuitengeneza Man United

Danny Welbeck akijaribu kumtoka Oscar
 
Chelsea 1-0 Man United