Tuesday, August 6, 2013
Friday, August 2, 2013
KAULI YA PINDA "YAMCOST" ASHITAKIWA NA HAKI ZA BINADAMU
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba akiwaonyesha waandishi wa habari, stakabadhi na hati ya mashtaka yaliyofunguliwa dhidi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika Mahakama Kuu ya Tanzania Dar es Salaam jana.
Kauli ya Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Kayanza Peter Pinda aliyoitoa hivi karibuni kuwa mtu yeyote atakaekaidi amri ya dola apewe kichapio imemtia matatani, kwani kituo cha sheria na haki za Binadamu kimeamua kumfungulia mashtaka.
Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Kayanza Peter Pinda.
Wednesday, May 29, 2013
REST IN PEACE ALBERT MANGWAIR
Albert Mangwair enzi za uhai wake
Mwanamuziki wa Hip-Hop ALBERT MANGWAIR amefariki dunia jana usiku huko
Afrika Kusini katika hospitali ya Hellena Joseph.
Alikuwa
Ghetto Moja Na Msanii M To The P. Walivyokwenda Kuwagongea Asubuhi
Walikuta Ngwear Amefariki Na M To The P Amepoteza Fahamu Kabisa.
Pia Daktari Ameshatoa Taarifa Kwa Watu Wa Karibu Wa Ngwear Huko South Africa.
Ngwea
akiwa na msanii M to the P. mtu wa karibu anasema
walitakiwa kurudi Dar leo lakini waliwakuta wamezima kwenye room wote
wawili baada ya kuji overdose madawa ya kulevya na M to the P yupo hoi
hospitali.
Mwili wa marehemu upo katika hospitali ya Hellene Joseph.
Mwili wa marehemu upo katika hospitali ya Hellene Joseph.
Mangwair akifanya makamuzi stejini enzi za uhai wake
Tuesday, April 23, 2013
NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA 2013..LEO NI LEO!
Vita kusaka tiketi ya kusafiri kwenda jijini London kwenye mchezo wa fainali wa klabu bingwa barani Ulaya inaanza usiku huu kati ya Mabingwa wa soka nchini Ujerumani dhidi ya inayotajwa kuwa timu bora kwa vilabu vya soka duniani kwa wakati huu FC Barcelona.
Kocha wa Bayern Munich, Jupp Heynckes amesema haogopeshwi na urejeo wa nyota wa Barcelona, Lionel Messi kuelekea mchezo huo wa kwanza wa nusu fainali ya klabu bingwa barani Ulaya.
Messi hajacheza mchezo wowote wa Barcelona toka alipoingia kama mchezaji wa akiba na kuisaidia timu yake kufuzu nusu fainal katika mchezo robo fainali dhidi ya Paris St-Germain ya Ufaransa. Lakini kuna kila dalili Muanjetina huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye ndiye mchezaji bora wa dunia kwa sasa,akajumuishwa kwenye kikosi cha Barcelona kwenye mchezo wa usiku wa leo.
Mwezi uliopita Messi aliweka rekodi kwenye ligi ya Hispania kwa kuwa mchezaji aliyezifunga timu zote zinazoshiriki ligi kuu nchini humo maarufu kama La Liga kwa misimu miwili mfululizo.
Barcelona inapambana kutaka kutwaa taji la tatu la klabu bingwa barani Ulaya ndani ya miaka mitano,Huku Bayern Munich ambao msimu ujao watakuwa chini ya aliyekuwa kocha wa Barcelona, Pep Guardiola, wao wanapambana kutafuta nafasi ya kucheza fainali yao ya tatu ndani ya miaka minne.
Kocha wa Bayern Munich, Jupp Heynckes ambaye aliwahi kuwafundisha mahasimu wa Barcelona, Real Madrid amesema licha ya kumheshimu mrithi wake wa kiti cha ukocha kwenye timu hiyo lakini hajaomba ushauri wowote kutoka kwa Guardiola na amejiandaa kwa kila namna kuhakikisha anaifunga Barcelona usiku huu. Aliongeza kwa kusema anaijua vizuri sana timu yake kuliko mtu yeyote na anafahamu soka ya Hispania na Barcelona wenyewe kwa undani mkubwa.
Wakati Barca wakiwa hawajaweka wazi kama watamuanzisha Messi au la, Baadhi ya wachezaji wa Barcelona akiwemo Xavi Hernandez alinukuliwa siku ya jumatatu akisema, kombe la ligi kuu nchini Hispania, La Liga lina umuhimu mkubwa kuliko klabu bingwa barani Ulaya.
Mechi hiyo itachezwa kwenye uwanja wa Allianz Arena mjini Munich nchini Ujerumani,majira ya saa nne kasorobo usiku kwa saa Afrika Mashariki.
Subscribe to:
Posts (Atom)