Monday, August 12, 2013

MAN U YATWAA NGAO YA HISANI, MOYES AUANZA MSIMU VYEMA

Timu ya soka ya Manchester United ya Uingereza imetwaa ngao ya hisani ikiwa ni ishara ya ufunguzi mwema wa msimu huu kwa kuitandika timu ya Wigan kwa bakora 2-0 katika dimba la Wembley.
Ushindi huo ni wa kwanza kwa kocha mpya wa Man U Moyes ambaye amepokea mikoba ya aliekuwa kocha wa Man U kwa miaka mingi Sir Alex Furguson , na hii ni kiashirio kizuri kwa Moyes.
Katika mpambano huo wa Ngao ya hisani sio mwingine alieipatia ushindi Man U bali ni ile ile LULU waliyoiokota Emirates,Robin Van Persie aliepachika mabao yote mawili katika mpambano huo.
 
Umati wa mashabiki ukielekea katika dimba la Wembley kushuhudia mpambano wa ngao ya hisani kati ya Man UNITED na Wigan Athletics.
 
Man U 2-0 wIGAN

Van Persie akipiga kichwa kutupia bao la kwanza la Man United.
 
Van Persie akijaribu kuwatoka walinzi wa Wigan Athletic

Van Persie na wenzake wakishangilia goli

Kocha wa Man United David Moyes akifurahia ngao ya hisani

Robin Van Persie akiwa na furaha tele baada ya kuiwezesha Man U kutwaa ngao ya hisani

Friday, August 2, 2013

VIDEO YA MAWAIDHA YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI


UNAIKUMBUKA TSUNAMI? TAZAMA VIDEO HII


PICHA YA SIKU

KAULI YA PINDA "YAMCOST" ASHITAKIWA NA HAKI ZA BINADAMU


Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba akiwaonyesha waandishi wa habari, stakabadhi na hati ya mashtaka yaliyofunguliwa dhidi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika Mahakama Kuu ya Tanzania Dar es Salaam jana.

Kauli ya Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Kayanza Peter Pinda aliyoitoa hivi karibuni kuwa mtu yeyote atakaekaidi amri ya dola apewe kichapio imemtia matatani, kwani kituo cha sheria na haki za Binadamu kimeamua kumfungulia mashtaka.


Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Kayanza Peter Pinda.

Wednesday, May 29, 2013

REST IN PEACE ALBERT MANGWAIR

 
 Albert Mangwair enzi za uhai wake

Mwanamuziki wa Hip-Hop ALBERT MANGWAIR amefariki dunia jana usiku huko Afrika Kusini katika hospitali ya Hellena Joseph.
Alikuwa Ghetto Moja Na Msanii M To The P. Walivyokwenda Kuwagongea Asubuhi Walikuta Ngwear Amefariki Na M To The P Amepoteza Fahamu Kabisa. 
Pia Daktari Ameshatoa Taarifa Kwa Watu Wa Karibu Wa Ngwear Huko South Africa.  
Ngwea akiwa na msanii M to the P. mtu wa karibu anasema walitakiwa kurudi Dar leo lakini waliwakuta wamezima kwenye room wote wawili baada ya kuji overdose madawa ya kulevya na M to the P yupo hoi hospitali.
Mwili wa marehemu upo katika hospitali ya Hellene Joseph. 
 
 
 
Mangwair akifanya makamuzi stejini enzi za uhai wake