Tuesday, August 27, 2013
MSHINDI WA BIGBROTHER AFRICA 2013 DILISH WA NAMIBIA AKIMWAGA RADHI
Mshindi wa Bigbrother africa 2013 Dilish akioga bila chenga. Dilish kutoka Namibia amefanikiwa kuibuka kidedea katika kinyang'anyiro hicho kilichodumu kwa siku 90 na kuondoka na kitita cha dola 300,000. usipimee....
Dilish
MAN U CHELSEA ZATOSHANA NGUVU
Rooney akijaribu kumhadaa Lampard katika mtanange huo
Rooney akijaribu kufunga bia mafanikio.
Klabu za Chelsea na Manchester United zimeminyana uwanjani Old Trafford. Pande zote mbili zimekosa kufunga bao, na hivyo kutoka sare ya bila kwa bila.
Matokeo hayo yanamaanisha kwamba mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza, wote wamepoteza pointi katika siku kumi na sita za kwanza wa msimu huu, na zinaifuata Manchester City iliyopoteza pointi pia kufuatia mechi dhidi ya Cardiff.Meneja wa Chelsea Jose Mourinho aliiambia BBC Sport " Hakuna Upande uliostahili kushinda na kushindwa vile vile, unataka kushinda lakini pande zote zilikua na ulinzi mkali. Na kwa mashabiki najua angalau bao moja lingewafurahisha, iwapo ungekuwa mchuano mzuri''.
Naye meneja wa Manchester United, David Moyes alisema, alivunjika moyo kwa sababu hawakuzoa pointi yoyote, lakini ndivyo ilivyo na hawana budi kujifunza kutokana na hali hiyo.
Chelsea kwa sasa inaongoza ligi kuu kwa pointi saba, ikifuatwa kwa karibu sana na Liverpool na Tottenham, zote zikiwa na pointi sita. Machester United inashikilia nafasi ya nne ikiwa na pointi nne.
Wednesday, August 14, 2013
HAPPY BIRTHDAY ENNA
Leo ni siku nzuri ya kuzaliwa mtoto wa rafiki yangu mpenzi Maria Kitenge. Enna ambaye pia ni kipenzi changu "mchumba" alizaliwa mwezi na tarehe kama ya leo. Yangu machache kwake ni haya;
Monday, August 12, 2013
MAN U YATWAA NGAO YA HISANI, MOYES AUANZA MSIMU VYEMA
Timu ya soka ya Manchester United ya Uingereza imetwaa ngao ya hisani ikiwa ni ishara ya ufunguzi mwema wa msimu huu kwa kuitandika timu ya Wigan kwa bakora 2-0 katika dimba la Wembley.
Ushindi huo ni wa kwanza kwa kocha mpya wa Man U Moyes ambaye amepokea mikoba ya aliekuwa kocha wa Man U kwa miaka mingi Sir Alex Furguson , na hii ni kiashirio kizuri kwa Moyes.
Katika mpambano huo wa Ngao ya hisani sio mwingine alieipatia ushindi Man U bali ni ile ile LULU waliyoiokota Emirates,Robin Van Persie aliepachika mabao yote mawili katika mpambano huo.

Umati wa mashabiki ukielekea katika dimba la Wembley kushuhudia mpambano wa ngao ya hisani kati ya Man UNITED na Wigan Athletics.

Van Persie akipiga kichwa kutupia bao la kwanza la Man United.

Van Persie akijaribu kuwatoka walinzi wa Wigan Athletic

Van Persie na wenzake wakishangilia goli

Kocha wa Man United David Moyes akifurahia ngao ya hisani

Robin Van Persie akiwa na furaha tele baada ya kuiwezesha Man U kutwaa ngao ya hisani

Man U 2-0 wIGAN

Tuesday, August 6, 2013
Friday, August 2, 2013
Subscribe to:
Posts (Atom)