Wednesday, September 11, 2013

PICHA ZA KWANZA ZA OZIL AKIWA ARSENAL


Ozil akiwa katika pozi na mchezaji mwenzake wa Arsenal Charmberlain
Mesut Ozil
Ozil


BALE AKUTANA NA CRISTIANO RONALDO


1
Bale akisalimiana na Ronaldo muda mfupi baada ya kutua Spain kujiunga na klabu yake mpya ya Real Madrid akitokea Uingereza katika klabu ya Tottenham Hotspurs. Usajili wa Bale umevunja rekodi ya dunia kwa kusajiliwa kwa kiasi cha paundi za uingereza milioni 86. Rekodi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Ronaldo aliesajiliwa kwa Paundi milioni 80.


3




28
Bale na kocha Ancelloti

Tuesday, September 10, 2013

JOSEPH KANIKI ''GOLOTA'' MKWANDA MATUMLA WABAMBWA NA MADAWA YA KULEVYA ETHIOPIA


 
Joseph Kaniki katika poss
 
Dar es Salaam. Mshambuliaji wa nyota wa zamani wa timu ya soka ya Simba na Taifa, Joseph Kaniki ‘Golota’ na bondia Mkwanda Matumla wanashikiliwa huku Addis Ababa, Ethiopia wakituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya.
Kukamatwa kwao kumezidi kuongeza idadi ya Watanzania maarufu waliotiwa mbaroni nje ya nchi katika siku za karibuni wakituhimiwa kwa makosa hayo.
Tukio hilo limetokea miezi miwili baada ya Watanzania wawili, wasanii Agnes Gerald Masogange na Melisa Edward kukamatwa kwenye Uwanja wa Oliver Tambo, Afrika Kusini wakituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 150 na thamani ya Sh6bilioni.
Aidha, hilo limetokea baada ya meli ya mizigo ya Gold Star iliyosajiliwa nchini kukamatwa na maofisa Forodha na askari wa doria wa Italia katika Pwani ya Sicily, Bahari ya Mediterranean ikiwa na tani 30 ya dawa za kulevya aina ya bangi zenye thamani ya Pauni za Uingereza 50milioni (Sh125 bilioni).
Kaniki na Matumla walikamatwa Agosti 31, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Bole, Addis Ababa wakati wakijiandaa kupanda ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia tayari kwa safari ya kuelekea Paris, Ufaransa.
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Samuel Shelukindo alithibitisha jana kwamba wanamichezo hao wanashikiliwa nchini humo na Polisi wa Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai.
Wanamichezo hao wamepandishwa kizimbani katika Mahakamu Kuu ya Ethiopia iliyoko kwenye eneo la Arada, Addis Ababa kujibu tuhuma za kubeba kilo saba za dawa hizo haramu. Mkwanda anadaiwa kubeba kilo nne wakati Kaniki akidaiwa kubeba kilo tatu. Kama watapatikana na hatia, wanaweza kufungwa kifungo cha miaka tisa hadi 15.
Alisema uwezekano wa kesi ya Kaniki na Matumla kurudishwa Tanzania haupo kwa kuwa nchi hizi mbili hazina utaratibu wa kubadilishana wafungwa.
“Wameshikiliwa hapa Ethiopia kwa zaidi ya siku 10 sasa, sisi tulipigiwa simu na polisi wa hapa Alhamisi iliyopita kujulishwa kwamba kuna Watanzania wawili wameshikiliwa kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya, tulipokwenda tukamkuta ni Kaniki na Matumla,” alisema Shelukindo.
“Wao wenyewe wanaeleza kwamba walipitia Mombasa na huo mzigo walipewa na mtu mmoja. Lakini Kaniki yeye anajitetea kwamba huyo aliyewapa huo mzigo pale Mombasa anajuana vizuri na Mkwanda. “Kwa hiyo alichofanya yeye ni kuubeba tu. Walikuwa wapitie hapa Addis wakashuke Paris, Ufaransa ndipo warudi Sweden kwa njia zao wanazojua wenyewe. Walipofika hapa Mkwanda alifanikiwa kupenya akapanda ndege lakini Kaniki akanaswa na mbwa ndipo akajitetea kwa polisi kwamba lile begi lilikuwa lake lakini mizigo mingine ilikuwa ya Mkwanda.
“Ndipo hapo sasa Mkwanda akashushwa kwenye ndege wakashikiliwa na Jumatatu ya wiki iliyopita wakapandishwa kwenye Mahakama ya hapa kutajiwa kesi yao lakini hawakupewa nafasi ya kujitetea. Kesi itatajwa tena Jumanne (jana) na Jumatano (leo) na uchunguzi wa polisi bado unaendelea.”
Wanamichezo hao walidai kwamba walikabidhiwa mizigo hiyo kwenye Uwanja wa Ndege wa Mombasa walipokuwa wakikabidhiwa pasi za kupandia ndege baada ya kupita sehemu zote za ukaguzi
“Kilichotokea ni jambo la aibu kwa nchi na hata wachezaji wenyewe wanajuta. Kwa mfano, Kaniki anasema alikuwa aende England kucheza mpira Desemba lakini sisi tukamwambia hatuwezi kumsaidia inabidi akabiliane na kesi iliyoko mbele yake. Mkwanda yeye ametuambia kwamba anaishi Sweden hatuna maelezo yake zaidi,” alisema Shelukindo na kuongeza kuwa wamewapelekea wanamichezo hao msaada wa mablanketi kwa vile bado wako mahabusu na Ethiopia kwa sasa kuna baridi kali.
Shelukindo alisema wachezaji hao wapo mahabusu kwenye Kituo cha Polisi cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai (Federal Police Crime Investigation) na hawana chochote zaidi ya nguo walizokuwa wamevaa.
Watanzania wengine kuachiwa leo
Shelukindo alisema kuna Watanzania wanne wanaotazamiwa kuachia leo baada ya kumaliza vifungo vyao baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya.
“Kuna Watanzania wengine walinaswa hapa miaka ya nyuma wao walikuwa wamemeza wakapasuliwa dawa zikatolewa na baadhi yao walifariki. Hata hivyo, wanne ambao wamemaliza vifungo vyao vya miaka minne wanaweza kurudishwa Tanzania,” alisema Shelukindo.

BURUDANI YA LEO: Video ya Diamond Platnumz-Number ONE


Thursday, August 29, 2013

ETO'O ATUA CHELSEA KWA PAUNDI MIL 7

Mtajiri wa London Chelsea hatimae wamekamilisha usajili wa mshambuliaji hatari wa Anj Makhachkhala Mcameroon Samuel Phils Et'oo, Hii ni baada ya Chelsea kushindwa kumnasa mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney.
Et'oo amesaini mkataba wa mwaka mmoja kwa makubaliano ya kiasi cha paundi milioni 7 kutoka milioni 17 za hapo awali.
Et'oo aliwasili jana usiku jijini London katika stesheni ya Mtakatifu Pancras (St Pancras) . Et'oo mwenye umri wa miaka 32 sasa atafanyiwa vipimo vya afya katika viwanja vya mafunzo vya Chelsea vya Cobham kabla ya kumalizia taratibu zingine za usajili leo hii baadae.
 Samuel Eto'o
Samuel Et'oo
Eto'o akiwa London tayari kukamilisha usajili wake na Chelsea.

4
5
Eto'o akiwa ndani ya Taxi dakika chache baada ya kuingia London usiku wa jana.
Et'oo muda mchache baada a kuwasili London

BREAKING NEWZZ!! MAJAMBAZI YAVAMIA BENKI KARIAKOO NA KUPORA FEDHA KIBAO

Watu wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi wamevalia sare za Jeshi la Polisi wamevamia Habib Afriican Bank Kariakoo DSM na kupora kiasi kikubwa cha Fedha. Jeshi la polisi kanda maalum wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo. Habari kamili itakujia hivi punde......