Friday, September 20, 2013
Thursday, September 19, 2013
MNIGERIA ASHINDA SHINDANO LA UREMBO WA KIISLAMU (MISS WORLD MUSLIMAH 2013)
Mwanadada wa Nigeria ndiye mshindi wa shindano la urembo kwa wasichana wa kiisilamu mjini Jakarta Indonesia.
Obabiyi Aishah Ajibola, 21, alishinda shindano
la kimataifa la wasichana wa kiisilamu kwa jina Muslimah mwaka 2013 siku
ya Jumatano.Obabiyi Aishah Ajibola, 21, akivishwa taji la urembo
Washindani 20 walishiriki mashindano hayo kuonyesha mitindo ya kiisilamu pamoja na maadili ya kiisilamu wakati wa mashindano hayo.
Mashindano yalifanyika kabla ya shindano kubwa zaidi la mwanamke mrembo zaidi duniani, ambalo limeghadhabisha makundi ya watu wenye msimamo mkali nchini Indonesaia kwa kutaka kuandaliwa huko.
Waliofuzu kwa fainali ya mashindano hayo, walichaguliwa kutoka miongoni mwa watu 500 waliochaguliwa kwa kutumia njia ya mtandao.
Moja ya vikwazo vya kuruhusiwa kushirki kwenye mashindano ilikuwa kusimulia kisa chako na ambavyo ulianza kuvalia Hijab au mtandio, ambacho kilikuwa kikwazo kwa wote waliotaka kushiriki.
Washiriki walitoka Bangladesh, Iran, Malaysia, Nigeria na Brunei.
Kabla ya fainali, washindani walihitajika kuamuka kwa sala ya asubuhi na kuswali pamoja huku wakijifunza kusoma Koran.
Bi Ajibola, mwenye umri wa miaka 21, alilia na kusoma aya kutoka kwa Korani, jina lake lilipotajwa. Alituzwa dola 2,200, pamoja na ziara ya mji mtukufu wa Mecca na nchini India.
Kabla ya kushinda alisema kuwa nia yake ya kushiriki mashindano hayo ilikuwa tu kuonyesha dunia nzima kuwa dini ya kiisilamu ni nzuri sana.
Eka Shanti, aliyefutwa kazi kwenye televisheni kwa kukataa kuvua mtandio wake, ndiye alianzisha shindano hilo miaka mitatu iliyopita.
Aliambia shirika la habari la Agence France-Presse kuwa walifanya shindano hili siku chache kabla ya shindano la kimataifa la mwanamke mrembo zaidi duniani kuonyesha wasichana kuwa kuna njia zengine tofauti ambazo unaweza kuwa mrembo.
Indonesia ndio nchi yenye idadi kubwa ya waisilamu duniani.
Obabiyi Aishah Ajibola akishindwa kujizuia Baada ya kutangazwa mshindi.
Obabiyi Aishah Ajibola akitoa neno la shukrani
LIGI YA MABINGWA ULAYA CHELSEA YACHAPWA BARCELONA, ARSENAL KAMA KAWA KAMA DAWA

Ligi ya mabingwa barani ulaya imeendelea tena hapo jana huku wapenda soka ulimwenguni wakishuhudia Vijana wa Mourinho Chelsea wakitandikwa na FC Basel palepale darajani kwa bao 2-1.
Huku nako ikishuhudiwa timu mbili zenye soka safi na la kuridhisha yaani FC Barcelona ya Uhispania na Arsenal ya Uingereza zikifanya mauaji, Barcelona wakiiadabisha Ajax ya Uholanzi nayo Arsenal ikiitandika Marseille ya Ufaransa.
Oscar akishangilia goli la kwanza la Chelsea
Marco Streller akishangilia goli lililoizamisha Chelsea darajani
Wachezaji wa FC Basle wakishangilia ushindi dhidi ya Chelsea
CHELSEA 1-2 FC BASLE
Katika mpambano kati ya Chelsea waliokuwa wenyeji wa mchezo huo pale darajani mabao ya timu zote mbili yalitupiwa kambani na Oscar (44) na yale ya Basle yalitupiwa kambani na M Salah (70) na Steller (81).
Katika mtanange baina ya Arsenal na Marseille mabao yalitupiwa kambani na Walcott (64) na Ramsey (83) na la kufutia machozi lilitupiwa kambani kwa mkwaju wa penati na Jordan Ayew (90).
Theo Walcott Walcott akitupia kambani bao la kwanza
Walcott akishangilia
Ramsey akishangilia baada ya kutupia kambani bao la pili
Giroud na Ozil wakimpongeza Ramsey
Ozil kibaruani
MARSEILLE 1-2 ARSENAL
Barcelona na Ajax mabao yalitupiwa kambani na Leonel Messi (21,54 na 74) na Pique (68).
Messi akifanya mauaji
Zuia hiyooooooooooooooooooooooo
Messi akipiga faulo iliyoenda moja kwa zote kambani
Iniesta akifanya udambwidambwi
Messi akitoka na mpira wake baada ya kutupia kambani mabao matatu ''Hat Trick''
BARCELONA 4-0 AJAX
Matokeo ya mechi zote
AC Milan 2-0 Celtic
Chelsea 1-2 FC Basle Marseille 1-2 Arsenal Atletico Madrid 3-1 Zenit St Petersburg Austria Vienna 0-1 Porto Barcelona 4-0 Ajax Napoli 2-1 Borussia Dortmund Schalke 04 3-0 Steaua Bucharest |
Wednesday, September 18, 2013
LIGI YA MABINGWA ULAYA VIGOGO WATAKATA MADRID,MAN U PSG ZAFANYA MAUAJI
Ligi ya mabingwa wa Ulaya jana ilianza kwa kasi huku ikishuhudiwa Vigogo katika ligi hiyo wakifanya mauaji ya kutisha, matokeo ya jumla ni kama ifuatavyo:
Manchester United 4 - 2 Bayer Leverkusen
Real Sociedad 0 - 2 Shakhtar Donetsk
Galatasary 1 - 6 Real Madrid
Kobenhavn 1 - 1 Juventus
Benfica 2 - 0 Anderlecht
Olympiacos 1 - 4 PSG
Bayern Munich 3 - 0 CSKA Moskva
Viktoria Plzen 0 - 3 Manchester City
Manchester united na Real Madrid zafanya mauaji.
Manchester United iliilamba Bayer Leverkusen mabao 4-2 katika mchezo uliopiigwa katika dimba la Old Trafford. Magoli ya Manchester yalitupiwa kambani na
Wayne Rooney (21)
Robin van Persie (58)
Wayne Rooney (69)
Antonio Valencia (78)
Robin van Persie (58)
Wayne Rooney (69)
Antonio Valencia (78)
Na yale ya Leverkusen yalifungwa na
Simon Rolfes (53)
Omer Toprak (87)
Omer Toprak (87)
Wayne Rooney akishangilia goli
Van PERSIE akishangilia
Fellaini kibaruani
Hapa kazi tuuu
MAN UTD 4-2 B LEVERKUSEN
Real Madrid nayo imeipatia kichapo Galatasaray kwa mabao 6-1, mabao ya Madrid yakitupiwa kambani na
Alarcon Isco (32)
Karim Benzema (53)
Cristiano Ronaldo (62)
Cristiano Ronaldo (65)
Karim Benzema (80)
Cristiano Ronaldo (90)
Karim Benzema (53)
Cristiano Ronaldo (62)
Cristiano Ronaldo (65)
Karim Benzema (80)
Cristiano Ronaldo (90)
Ronaldo na Bale wakishangilia ushindi
Pepe akiwajibika ipasavyo
Drogba hoi kwa kichapo
GALATASARAY 1-6 REAL MADRID
OLYMPIACOS 1-4 PSG
BAYERN MUNICH 3-0 CSKA MOSCOW
PLZEN 0-3 MAN CITY
Tuesday, September 17, 2013
MAJEMBE YA ARSENAL YAKIJIFUA KUWAKABILI MARSEILLE JUMATANO

Walcott,Ozil,Vermalain,Gibbs,Geroud na Chamberlain wakijinoa

Watoto wa Wenger mazoezini

Sagna,Giroud na Koscielny

Ozil na Per Mertesacker

Vermaelen

Arsene Wenger akifuatilia mazoezi


Ozil


Szcieny

Walcott

Subscribe to:
Posts (Atom)
