Hapana chezea jeuri ya pesa, kama huna sema sina pesa sio useme hela hakuna. Katika hali ya kustaajabisha kwa wale wenzangu na mimi tusiokuwa na hata baiskeli, Mtoto wa Bilionea wa Tanzania Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhressa ajulikanae kwa jina la Yussuf Bakhressa ameingiza nchini gari aina ya Brabus kwa oda maalum sawa sawa na lile linalomilikiwa na mmiliki wa timu kubwa ya soka ya Manchester City ya Uingereza. Gari hilo lililoonekana mjini linasemekana limemgharimu dola la kimarekani 500,000 ambazo ni sawa na Shilingi za kitanzania milioni 805. Cheki kwa uzuri ''ndinga'' hilo. Gari aina ya Brabus
Huu ni muhtasari uliotolewa na BBC Yaliyojiri Huko Westagate
15:20 Polisi waonekana wakikimbia huku na kule katika harakati zao hizo dhidi ya Al Shabaab
14:56 Mkuu wa majeshi Meja Jenerali Julius Karangi amesema magaidi
hao wanaweza kujisalimisha ikiwa wanataka kwa sababu jeshi litakabiliana
nao vilivyo. Pia amesema kuwa Kenya inakabiliana na magaidi wa
kimataifa
14:35 Ole Lenku anasema kuwa hali ingali tete
lakini vikosi vya usalama vya Kenya vinakaribia kuwazingira magaidi
hao...Hadi kufika sasa watu 62 wamefariki na wengine zaidi ya 175
kujeruhiwa. Pia ameongeza kuwa magaiodi wote ni wanaume, kutokana na
taarifa za awali kuwa magaidi hao walikuwa wanaongozwa na mwanamke
14:30 Ole Lenku anasema kuwa wanajeshi kumi
wamejeruhiwa na wanapokea matibabu. Pia mateka karibu wote wameweza
kuokolewa. Ole Lenku pia amesema kuwa wameweza kuwaua magaidi wawili
14:28 Waziri wa usalama Joseph Ole Lenku anasema
kuwa moshi ulitokana na moto uliosababishwa na magaidi wlaioko ndani ya
jengo hilo kujaribu kusambaratisha juhudi za wanajeshi wa Kenya dhidi
yao
14:03 Mkuu wa polisi David Kimaiyo asema kuwa vikosi vya usalama
vinakaribia kudhibiti jengo hilo lote na vimeingia ndani kabisa ya jengo
hilo kiasi cha kuwaokoa baadhi ya mateka
14:00 PM: Milipuko zaidi yasikika katika jengo hilo
13:54: Mwandishi wa BBCIdriss Situmaaliye katika
eneo la Westgate anasema duru zinaarifu kuwa vikosi vya usalama vya
Kenya vinasema kuwa ndivyo vimelipua sehemu ya jengo kujaribu kuingia
ndani kabisa ya jengo hilo
13:52 PM Magari ya Ambulance yaobnekana yakienda
katika eneo la shambulizi pamoja na magari ya zima moto. Vikosi vya
usalama vinawataka watu kuondoka karibu na eneo la operesheni hiyo ili
kuwawezesha kufanya kazi yao
13:49 pm: Moshi mkubwa mweusi waonekana ukitoka juu ka juu katika jengo hilo haijulikani nini kilichosababisha
13:19 pm Moshi mkubwa unaonekana ukitoka katika
jengo la Westgate ambako wapiganaji wa Al Shabaab wanawazuilia mateka
wakenya ambao idadi yao haijulikani
13:12 PM Viongozi wa kidini watoa taarifa kulaana kitendo cha Al Shabaab
12:30 PM: Milipuko zaidi na milio ya risasi
imesikika katika jengo la Westgate huku vikosi vya usalama vikifanya
jitahada za misho kuwa Westgate ikiwaka moto Wanausalama wakikabiliana na Magaidi Mwamanchi akijaribu kujinusuru Polisi wakiwanusuru wananchi Wanausalama wakiokoa wananchi Maiti Westage Majeruhi wakisaidiwa
Vijana wa Arsene Wenger wameendeleza wimbi la ushindi kwa kuicharaza Stoke City kwa goli 3-1 katika dimba la Emirates. Sio mwingine aliefanikisha ushindi huo 100% bali ni Metsut Ozil alienunuliwa kwa gharama kubwa toka Real Madrid. Magoli yalitupiwa kambani na Aaron Ramsey,Martesacker na Sagna.Wakati la kufutia machozi likifungwa na Cameron
Ozil akiongoza mashambulizi
Wachezaji wa Arsenal wakimpongeza Ramsey baada ya kufunga goli
Mfungaji wa goli pekee la Stoke City Metesacker akipiga kichwa kufunga goli la pili Metersacker oyeeeeeeeeeeeeeeeee Giroud akichanja mbuga