Andre Villa-Boas maarufu kama AVB
Klabu Tottenham imemtimua kocha wake Andre Villas
Boas siku moja baada ya Tottenham kupata kichapo cha magoli 5- 0 kutoka
Liverpool
Kipigo hicho cha magoli 5 - 0 ni moja kati ya
matokeo mabaya kutokea katika uwanja wao wa nyumbani wa Tottenham wa
White Hart Lane kwa takriban miaka 16 iliyopita.
Wakati Tottenham wakitimua kocha kwa upande wake Meneja wa Liverpool
Brenden Rodgers amesema hatua ya timu yake kuisambaratisha Tottenham kwa
magoli 5 - 0 katika uwanja wao wa nyumbani wa White Hart Lane ni moja
kati ya mechi ya viwango vya juu vilivyoonyeshwa na Liverpool katika
kipindi cha uongozi wake.
Rodgers alishika hatamu ya kuinoa Liverpool
mwaka 2012 ambapo kwa sasa timu hiyo ipo nafasi ya pili ikiwa nyuma ya
Arsenal katika msimamo wa ligi kuu ya England.
"Ni matokeo mazuri na viwango vya hali ya juu," amesema Rodgers.
"Tumepata magoli matano na inawezekana tungepata mengi hata saba au nane. Huo ndio uzuri wa timu ambapo inapata magoli."
Mshambuliaji wa timu hiyo Luis Suarez alifunga
magoli mawili wakati Jordan Henderson, John Flanagan na Raheem Sterling
wakifunga kila mmoja.
Wakati wa mchezo huo Tottenham alishindwa
kulenga hata mara moja kwenye goli la Liverpoool ambayo imefunga timu
hiyo katika mechi nane za ligi kuu ya England ziliyochezwa kwenye
kiwanja hicho.