Wednesday, February 12, 2014

NI ARSENAL Vs MAN UNITED...HATUMWI MTOTO SIGARA

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, anatarajiwa kuwa nyota wake aliyesajiliwa kwa kitita cha pauni milioni 42, atarejea katika hali yake ya kawaida na kuonyesha mchezo mzuri, baada ya matokeo mabaya wikendi iliyopita.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, kutoka Ujerumani,Metsut Ozil hajatupia kambani katika mechi nane zilizopita huku akiwa amechangia kupatikana kwa magoli mawili pekee katika mechi hizo.
 
Metsut Ozil

Lucas Podolski
 
Ozil, ambaye alijiunga na Arsenal, kutoka kwa klabu ya Real Madrid Septemba mwaka uliopita, alianza vyema kwa kufunga magoli manne na kuchangia magoli sita katika mechi zake kwanza kumi na mbili za ligi kuu.
Lakini mcheza kiungo huyo, alishutumiwa vikali kufuatia mchezo aliouonesha wakati Arsenal ilipovurugwa magoli 5-1 na Liverpool, hali iliyomlazimu Wenger kumuondoa kunako dakika ya sitini na moja.
Akiongea kabla ya mechi yao katika Uwanja wa Emirates siku ya Jumatano usiku, Wenger alisema kuwa anadhani David Moyes anaweza kufanikiwa kama kocha wa United ikiwa atapewa muda.
 
Van Persie

Wayne Rooney

Julai mwaka uliopita, Moyes aliteuliwa kuchukua mahala na Sir Alex Ferguson ambaye alistaafu kama kocha wa Manchester United baada ya kushinda ligi kuu ya Premier mara 13 katika kipindi cha miaka 27, lakini amekuwa na kibarua kigumu kufuata nyayo za Ferguson.
Manchester United inashikilia nafasi ya saba kwenye msururu wa ligi kuu na alama 41 na hata ikishinda mechi yake dhidi ya Arsenal, Vijana hao wa Moyes watasalia katika nafasi hiyo hiyo.

Tuesday, February 4, 2014

HUU NDIO MSIMAMO LIGI KUU UINGEREZA BAADA YA MECHI YA JANA

CHELSEA YAITULIZA MASHETANI MAN CITY

Ivanovic akitupia kambani bao la pekee.
  
Muuaji Ivanovic akishangilia goli la pekee dhidi ya Man City

Manchester City imevutwa shati na Chelsea kwa kucharazwa bao 1-0 katika uwanja wao wa nyumbani. kabla ya mechi hiyo Man City ilikuwa imeshinda mechi zote 11 ilizokuwa imecheza katika dimba la nyumbani Ettihad Stadium kabla ya kukutana na Chelsea.
Mtanange huo umeweka historia mpya kwa mara ya kwanza kwa Manchester City kushindwa kufunga bao katika mechi za nyumbani tangu mwaka 2010.
Bao la Chelsea lilifungwa na Branislav Ivanovic katika kipindi cha kwanza .
Kutokana na matokeo hayo Manchester City na Chelsea zinalingana pointi lakini Man City imetupia kambani mabao mengi.
Liverpool iko katika nafasi ya nne, Everton ni ya tano ilhali Tottenham ni ya sita huku Manchester United ikishikilia nafasi ya saba.
 
Kwangu mimi huyu dogo,Hazard ndio alikuwa "Man of the Match"

Hali tete Wachezaji wa Man City ''wameshavurugwa"

Hii ndio hali ilivyokuwa baada ya kukosakosa magoli

Hii ni hali na vituko vya Mourinho pale alipohisi mwamuzi hatendi haki

TAZAMA VIDEO YA MPAMBANO HUO

Monday, January 27, 2014

MOHAMED SALAH ASAJILIWA CHELSEA

 Mohamed Salah

Mohamed Salah weekend hii alikamilisha vipimo vya afya jijini Paris na kupewa mkataba wa miaka mitano na nusu, Salah amekabidhiwa uzi namba 15.

Baada ya kusaini mkataba jijini Paris Salah alisikika akisema 'I'm very happy to sign for Chelsea, such a big club in the world. I hope I can make the Chelsea supporters happy and have a good career at the club for many years to come.'

BAINES AONGEZA MKATABA EVERTON

Leighton Baines ameongeza mkataba na timu yake ya Everton ambapo mkataba huo wa miaka minne utambakisha Everton mpaka 2018. Baines amekamilisha taratibu hizo na kuzima kabisa uvumi uliokuwepo kwamba huenda angesajiliwa na Manchester United.

Kocha wa Everton Roberto Martinez amesema "ni kati ya mabeki wa kushoto mahiri katika soka la Uingereza na duniani kote na hvyo nategemea makubwa toka kwa Baines"

Leighton Baines

ARSENAL YAKAMILISHA UDHAMINI WA PUMA KULAMBA PAUNDI MILIONI 150

Timu ya soka ya Arsenal imethibitisha kuwa kampuni ya Puma ndio watakuwa wadhamini wakuu wa vifaa vya michezo, kabla ya hapo Arsenal ilikuwa ikidhaminiwa na kampuni ya Nike.

Udhamini huo utafikia paundi milioni 150 ndani ya miaka mitano.
Taarifa kutoka klabu ya Arsenal zimesema mkataba huo wa udhamini wa vifaa utaanza rasmi
Effective from July 1, 2014, PUMA will become the official kit partner of Arsenal. In addition to producing the playing and training kit for all Arsenal teams, PUMA has acquired wide-ranging licensing rights to develop other Arsenal branded merchandise on a global basis. This new commercial partnership represents the biggest deal in PUMA and Arsenal’s history.

Read more at: http://ladyarse.co.uk/2014/01/arsenal-confirm-puma-deal-to-the-stock-exhange/ | Daily Cannon
 1 julai,2014 ambapo Puma watadhamini vifaa kwa timu zote za Arsenal.

puma-giroud

CABAYE KUTUA PSG

Taarifa zilizopo kwenye gazeti la Le Parisien la leo limeripoti kwamba PSG wataelekea Newcastle kukandamiza dau la pili la Paundi milioni 20 kutoka milioni 14 ili kumnasa Yohan Cabaye.

Mkurugenzi wa PSG Olivier Letang ataelekea Kufanya mkutano na Uongozi wa Newcastle ili kumnasa Cabaye.

Yehan Cabaye