Thursday, April 3, 2014

UEFA PSG YAICHARAZA CHELSEA, REAL MADRID YAITANDIKA DORTMUND

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho ametangaza wazi kuudhika sana na safu yake butu ya mashambulizi.
Mourinho aliyasema hayo punde baada ya kushuhudia PSG ya Ufaransa ikiititima 'the blues' mabao matatu kwa moja katika mkondo wa kwanzawa mechi ya robo fainali ya kombe la mabingwa Barani Ulaya.
 
Wayaaaaaaaa
 
Laveziiiii wayaaaaaaaaaaaa

Wenyeji PSG waliweka wazi ari yao ya kusonga mbele baada ya dakika pekee kupitia kwa Ezequiel Lavezzi .
Vijana wa Jose Mourinho nao wakajifurukuta na kufanya mashambulizi ambayo yalizaa penalti baada ya Oscar kuchezewa visivyo katika eneo la lango.
Eden Hazard akafanya mambo kuwa 1-1 katika dakika ya 27.
Nipe nikupe iliendelea hadi kipindi cha pili PSG walipofaidika na bao la kujifunga mwenyewe la David Luiz kunako dakika ya 61.
Hawakukomea hapo ,Javier Pastore alihakikisha Chelsea itakuwa na mlima wa kupanda nyumbani kwao Stamford Bridge katika mkondo wa pili mbali na kuibua kumbukumbu za mwaka wa 2004 timu hizo
mbili ziliposajili matokeo sawia na hayo PSG ilipokuwa mbioni kucheza katika fainali ya kombe la mabingwa .
Aidha mechi ya kwanza kwa mkufunzi Jose Mourinho alipochukua hatamu Stamford bridge ilikuwa dhidi ya Paris St-Germain mwezi September 2004.
Wakati huo The Blues waliwatandika PSG 3-0 John Terry na Didier Drogba wakiandikisha majina yao katika orodha ya wafungaji.
 
Ibrahimovic akiwanjonjofya wachezaji wa Chelsea
 
Mwamuzi na wachezaji wa PSG wakimuangalia Zlatan Ibrahimovic baada ya kutengenezwa na Ramires.

Hatoki mtu hapa.....Ibrahimovic akioneshana udamwidambwi na David Luiz

ThiagoSilva na Torres hakatwi mtu hapa

We bwege tuuu......mwamuzi wa pembeni akiwahi mpambano kati ya Cavani na Luiz

''Mhhh hali tete'' Kocha wa Chelsea Jose Mourinho akiduwazwa na matokeo.

REAL MADRID Vs DORTMUND

 Vigogo wa ligi kuu ya Uhispania ambao wamekuwa wakisuasua katika mechi za la liga Real Madrid, wamedhibitisha udedea wao katika ligi ya mabingwa bara Uropa baada ya kuiadhibu vikali Borussia Dortmund ya Ujerumani katika mkono wa kwanza wa robo fainali ya mchuano huo iliyochezwa Santiago Bernabeu.
Real iliilaza Borussia Dortmund mabao matatu kwa Ubuyu .
Real ilidhihirisha nia yao mapema Gareth Bale alipofuma bao la kwanza kunako dakika ya tatu ya mechi hiyo.
 
 
Bale akitupia kambani bao la kwanza
 
CR9 akishangilia baada ya kutengeneza kamba ya pili

Isco alitikisa wavu na bao la pili katika dakika ya 27, huku bao la tatu likifungwa naye Cristiano Ronaldo dakika ya 57 kipindi cha pili.
Bao hilo la mchezaji bora msimu wa 2013 lilimsaidia Ronaldo kusawazisha rekodi ya idadi kubwa ya mabao kuwahi kufungwa kwa msimu mmoja wa dimba hilo la mabingwa barani Uropa.
Bao la Ronaldo lilikuwa la 14 katika mechi nane za ligi ya mabingwa , sawia na rekodi iliyowekwa na Lionel Messi katika mwaka wa 2011-2012.
Kwa upande wao Dortmund ambao walishindwa katika fainali mwaka uliopita na Bayern Munich watajilaumu wenyewe kwa kutotumia vyema fursa 12 walizopata kushambulia lango la Real.
Hata hivyo vijana hao wa Jurgen Klopp walidhihirisha wazi bila nyota wao Robert Lewandowski safu yao ya ushambulizi ni butu.
Wajerumani hao wanajuma moja tu kusahihisha makosa walioyafanya jana kabla ya mechi ya marudio ambayo imeratibiwa kuchezwa tarehe 8 Aprili huko ujerumani.


Namie nimooooooooooooo...Isco akishangilia goli pamoja na Bale
 
Safi sana dogo, CR9 akimpongeza Isco

Msifikiri nimefurahi naumiaaaaaaaaa...kocha wa Borussia Dortmund
 
PSG 3-1 CHELSEA
 
REAL MADRID 3-0 DORTMUND

Wednesday, April 2, 2014

ROBO FAINALI UEFA MAN UTD YAIDINDIA BAYERN OT, ATLETICO YAIVIMBIA BARCELONA

 
 
Vidic akiifungia Manchester bao dhidi ya Bayern
  
Tulia weweeeeee

Kulikuwa na mechi mbili za mkondo wa kwanza wa robo fainali ya ligi kuu ya mabingwa barani Ulaya iliyochezwa Jumanne usiku, Manchester United ya Uingereza ikikabana koo na mabingwa watetezi waligi hiyo Bayern Munich ya Ujerumani.
Nayo Barcelona ya Uhispania ikikabiliana na Athletico Madrid vilevile ya Uhispania.

 
Wachezaji wa Man U wakishangilia bao

Licha ya kuwa Bayern Munich ilikuwa imepigiwa upatu kutamba dhidi ya Manchester United vijana wa pep Gardiola walikabiliwa na ukuta mrefu wa Manchester uwanjani Old Traford.
Na walipopata fursa nahodha wa Manchester Nemanja Vidic alifunga bao maridadi la kichwa baada ya kuunganisha vizuri kona kutoka kwa Wayne Rooney kunako dakika ya 58 ya kipindi cha pili.

Gonga gonga ya Wajerumani ilikosa kuzaa matunda lakini bao la Bastian Schweinsteiger kunako dakika ya 66 iliwatunuku mabingwa hao wao watetezi bao muhimu la ugenini kabla ya mkondo wa pili utakaochezwa huko Ujerumani .
Bila shaka mashabiki na watani wa kocha David Moyes watakubaliana naye kuwa United itajutia fursa aliopoteza Danny Welbeck alipokuwa ni yeye pekee dhidi ya kipa wa Bayern Manuel Neuer .

United vilevile itamshukuru kipa David de Gea aliyefanya kazi ya ziada kuzuia mashambulizi haswa kutoka kwa Arjen Robben.
Kutokana na sare hiyo sasa mkufunzi Pep Guardiola ana kibarua kigumu pale Man United itakapozuru uwanja wa Allianz Arena wiki ijayo.
Mechi nyingine 2 zimeratibiwa kuchezwa baadaye Jumatano, Real Madrid ya Uhispania ikivaana na Borussia Dortmund kutoka Ujerumani nayo Paris st Germain ikiikaribisha wawakilishi wengine wa Uingereza Chelsea ya Uingereza Katika uwanja wa Parc des Princes. 


ATLETICO YAIVIMBIA BARCA
 
Messi akijaribu kumhadaa Gabi

Messi akikokota kijiji

Vita vya mahasimu wa nyumbani Atletico Madrid na Barcelona viliishia sare ya nne msimu huu timu hizo mbili za Uhispania zilipotoka sare ya moa kwa moja katika mkondo wa kwanza wa
ligi kuu ya mabingwa barani Ulaya iliyochezwa katika uwanja wa Camp nou.
Atletico inayoongoza katika dimba la nyumbani ya la Liga sasa imejipatia bao muhimu la ugenini licha ya kuwa ilifuzu kuingia katika robo fainali hizo kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1997.
Licha ya barcelona kupigiwa upatu kushinda taji hilo ni Atletico iliyofunga ya kwanza kupitia kwa kiungo Diego aliyekuwa ameingia kuchukua nafasi yake Diego Costa aliyelazimika kuondolewa uwanjani 
 

 
Neymar akishangilia goli

baada ya kupata jeraha katika dakika ya 30.
Barca ilijifurukuta na kufunga baada ya Andre Iniesta kupenyeza pasi safi katikati ya ulinzi mkali wa Atletico iliyopokelewa na Neymar aliyesawazisha zikiwa zimesalia dakika 20 mechi hiyo kukamilika.
Juhudi za Barcelona za kutafuta bao la Ushindi ziliambulia patupu ngome ya ulinzi ya Atletico ilipoimarishwa na mambo yakasalia kuwa sare .
Athletico inaongoza ligi ya nyumbani kwa alama moja zaidi ya Barca.

Wednesday, March 26, 2014

SHABIKI WA MAN U AKIMPA ''MAKAVU LIVE'' DAVID MOYES


Hii ilikuwa katika mechi dhidi ya Man City..shabiki uzalendo ulipomshinda na kuanza kumporomoshea mitus kocha wa Man United 'The Chosen One'' David Moyes.

MAN UNITED MDEBWEDO YANYOLEWA 3 NA CITY

 
 

 Edwin Dzeko akishangilia


Manchester City iliendelea kujiimarisha na kuikosesha amani klabu ya Manchester United katika ligi kuu ya premier.
Sio hilo tu bali Man City wanaongeza shinikizo kali kwa Chelsea walio juu kwenye jedwali la ponti katika ligi hiyo.
Man Uinted walipata kichapo cha mbwa cha mabao matatu bila nyumbani Old Trafford.
Edin Dzeko alitupia mabao mawili katika kila kipindi kwa City hapo jana huku Yaya Toure akizidisha machungu kwa bao la tatu mwishoni mwa mechi bila jibu kutoka kwa Man United.
Sasa vijana hao wa City wanashikilia nafasi ya pili nyuma ya Chelsea.

 
Kocha wa United Moyes akilia kwa uchungu


 Kambaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

 
Hapa kazi tuu

Fellaini akijaribu kumwaga majaro

Niache bhanaaaa mbona shoboo

 
MAN UTD 0-3 MAN CITY

Friday, March 21, 2014

Affiliate Program ”Get Money from your Website”

REAL MADRID INAONGOZA KUNYAKUA KOMBE LA UEFA CHAMPIONS LEAGUE

UEFA Champions League

Wakati draw ya kutafuta timu zitakazopambana katika hatua ya robo fainali ya UEFA itakayochezeshwa majira ya saa 8 mchana kwa saa za Afrika ya mashariki huko jijini Nyon,Switzerland. Real Madrid mpaka sasa inaongoza kwa kulibeba kombe hilo kwa kulinyakua mara 9. 
Ifuatayo ni orodha ya timu zilizokwisha jitishwa ndoo hiyo. Real Madrid (9), Bayern Munich (5), Barcelona (4), Manchester united (3), wakati Chelsea na Borussia Dortmund mara 1 kila moja.

  • Atletico Madrid imetinga robo fainali baada ya miaka 17 kwa kuichabanga AC Milan jumla ya mabao 5-1.
  • Kwa mwaka wa pili mfululizo Spain imeingiza timu nyingi katika hatua ya robo fainali ikifuatiwa na Uingereza 2,Ujerumani 2,France 1.
  •  
Baada ya draw kuchezeshwa leo mechi za robo fainali zitachezwa April 1 na 2. Marudio April 8 na 9.