Mabingwa wapya wa Uingereza 2014-2015 Manchester City.
Vijana wa Manuel Pelligrini walitawazwa mabingwa katika siku ya mwisho
ya ligi kuu ya Uingereza baada ya kuilaza West Ham mabao 2-0.
Samir Nasri nahodha Vincent Kompany ndio waliomhakikishia Pelleigrini
alama tatu muhimu zilizotosha kuipiku Liverpool iliyomaliza katika
nafasi ya pili alama 86 mbili nyuma ya City ambao wametwaa taji lao la
pili katika kipindi cha miaka mitatu. Umati uliojaa uwanjani Etihad ulimiminika uwanjani baada ya kipenga cha mwisho. Kocha huyo kutoka Chile alifaidika na kichapo
cha Liverpool mikononi mwa Chelsea na hivyo alihitaji sare ya aina
yeyote kujihakikishia ushindi. Mancity iliititima West ham 2-0 na kutamatisha msururu wa mechi tano bila ya kushindwa . Pelligrini, atakumbukwa kwa kuirejesha kombe
Etihad baada ya Roberto Mancini kupigwa kalamu kwa kushindwa kutetea
taji msimu uliopita . Kocha huyo mwenye miaka 60 anajivunia mabao 102. Kwa upande wao Liverpool walisajili ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Newcastle United uwanjani Anfield. Mashabiki wa Man City wakishuhudia timu yao ikitwaa ubingwa wa EPL.
Samir Nasri akitupia kuihakikishia Man City ubingwa.
Nahodha wa Man City Vicent Kompany akinyanyua juuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu kombe la ligi kuu ya uingereza 2014-2015
Kocha wa Man City Manuel Pellegrini akiwa amebeba kombe la ligi kuu Uingereza 2014-2015 Wachezaji wa Man City wakiwa wamembeba kocha wao Pellegrini baada ya kunyakua kombe la ligi kuu ya UIngereza
Nyota wa Real Madrid ya Uhispania Cristiano Ronaldo
amevunja rekodi ya Lionel Messi ya ufungaji mabao mengi zaidi katika
ligi ya mabingwa barani Uropa alipoifungia timu yake mabao mawili na
kuisaidia
kuichapa Bayern Munich mabao 4-0 katika nusu fainali jana usiku.
Mreno huyo mwenye umri wa miaka , 29,alifunga bao lake la 15 na 16 msimu huu katika uwanja wa Allianz Arena.
Kufuatia ushindi huo Real Madrid ilifuzu kwa fainali ya mchuano huo kwa jumla ya mabao 5-0.
Ronaldo sasa amefunga mabao 16 katika mechi kumi
za ligi hiyo ya mabingwa Barani Ulaya mbili zaidi ya Lionel Messi wa
Barcelona .
Rekodi hiyo ya mabao 14 ilikuwa ikishikiliwa kwa
pamoja kati ya Messi (2011-12, Barcelona), Ruud van Nistelrooy
(2002-03, Manchester United) na Jose Altafini (1962-63, AC Milan).
Kwa jumla Ronaldo amefunga mabao 67 katika ligi
hiyo ya mabingwa barani ulaya sawa na Messi na ni mabao manne tu nyuma
ya rekodi ya idadio kubwa zaidi ya mabao yaliyofungwa na mchezaji wa
zamani wa Real na Schalke Raul.
Vigogo wa ligi kuu ya Uhispania Real Madrid, wamekuwa timu ya kwanza
kufuzu kwa fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya baada ya kuinyeshea
Mabingwa watetezi wa kombe hilo Bayern Munich ya Ujerumani kwa mabao
manne kwa nunge na hivyo kuibuka a ushindi mkubwa wa jumla ya mabao 5-0.
Sergio Ramos alifunga mabao mawili mapema katika kipindi cha kwanza cha mechi hiyo.
Ramos akitupia kambani goli la kwanza
Kabla ya nyota wa Ureno na mchezaji bora duniani Christiano Ronaldo
kuihakikishia Madrid fainali yao ya kwanza tangu mwaka wa 2002 na mkwaju
wa wa freekick.
Bao hilo lilikuwa lake la 16 katika ligi ya mabingwa barani Uropa.
Kwa Bayern, kichapo hicho kilikuwa ni kama wembe
wa kutu kwao kwani mwaka uliopita Wajerumani hao waliifunga Barcelona
7-0 katika hatua ya nusu fainali kabla ya kuilaza Borussia Dortmund na
kutwaa taji lao la tano barani ulaya.
Haijulikani kufikia sasa iwapo halmashauri
inayoingoza klabu hiyo itachukua hatua yeyote dhidi ya kocha wa klabu
hicho Pep Guardiola ambaye licha ya kuiongoza Barca kutwaa taji la
Bundesliga ameshindwa kutetea hadhi ya klabu hiyo katika mchuano huu wenye kitita kikubwa zaidi.
Nimeuaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Oyooooooo...Sergio Ramos akishangilia goli
Madrid sasa inasubiri kujua iwapo itachuana na
Chelsea ya Uingereza chini ya ukufunzi wake aliyekuwa kocha wao Jose
mourinho ama wapinzani wao wa mji wa Madrid , Athletico .
Mshambulizi wa Athletico Madrid Diego Costa
alisema anatumai Chelsea hawata regesha basi kwenye lango lao ilhali
watacheza mchezo yenye maarifa.
Timu hizo zilitoka sare tasa katika mkondo wa kwanza .
Arsenal ya Uingereza ilijiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa mchuano
wa ligi ya mabingwa mwakani baada ya kuinyuka Newcastle mabao matatu
kwa nunge katika mechi ya katikati ya juma iliyochezwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Emirate. Koscielny akitupia kambani bao la kwanza Giroud akimpongeza Koscielny baada ya kufunga goli la kwanza
Ushindi huo umeiacha Arsenal na jumla ya alama 73 nne zaidi ya wapinzani wao wa karibu Everton wenye alama 69. Laurent Koscielny ndiye aliweka niya ya 'the
Gunners' bayana alipofunga mkwaju wa Santi Cazorla kunako dakika ya 26
ya kipindi cha kwanza . Mesut Ozil naye akaongezea la pili kabla ya
kukamilika kipindi cha kwanza . Hata hivyo ni Olivier Giroud ndiye
aliyemhakikishia kocha Arsene Wenger alama tatu muhimu alipohitisha
kichapo hicho kwa bao la tatu kunako dakika ya 66 ya mechi hiyo. Aidha ilikuwa ni kichapo cha 6 mfululizo kwa timu ya Newcastle na kocha Alan Pardew . Hata hivyo mbivu na mbichi itabainika Manchester City itakapokwaruzana na Everton jumamosi ijayo. Timu nne za kwanza ndizo zinazoshiriki mchuano huo wenye kitita kikubwa zaidi barani. Arsenal ilikuwa imedorora kutoka nafasi ya kwanza na ilikuwa na hatari ya kukosa kushiriki ligi hiyo. Ozil akishangilia kutupia bao la pili
Most men ask: What do women want?
Contrary to popular belief, we aren't all that complicated. In fact,
most of my female counterparts just want to be loved by their partner.
That includes being respected, adored, supported, and appreciated. Not
so bad, is it?
Men, however, are said to be simple. But are they? Do men just want a
good meal, good sex, and a beer, or is there more than meets the eye? I
believe so. Here are five things single men are looking for in a woman
when dating 1. That natural chemistry
You heard me right; men want chemistry as much as women do.
They want to feel that "umph," that "it" factor that is often
indescribable. You don't have to look like a model. They just have to
feel that energy. You either got it as a couple or you don't. Oh, and
chemistry has little to do with sex.
2. A woman who is confident
Strut in with your head held high and men will notice. Every
man that I spoke with really appreciates a woman who is confident. They
love a woman who knows who she is and is comfortable in her own skin.
But don't confuse confidence with arrogance. Humility is best.
3. She's her authentic self
No matter who you are or what you do for a living, you must be
yourself. Men can tell when women are trying too hard. Men love women
who are genuine. Again, it shows that you are comfortable in your own
skin. And that's super sexy.
4. You can dress up and dress down
Men are visual creatures. Of course they want to find you
physically appealing. Put on a dress and look gorgeous. Put on jeans and
a pony tail and still look stunning? Yup. Men are looking for women who
can dress up and dress down. You don't have to put on the fake lashes
for bed. Let your hair down and show him you are a natural beauty.
5. Assertiveness is sexy. Society expects men to court women. And so do I. A man,
however, also enjoys a woman who treats him from time to time. He also
likes a woman who is assertive and tells him what she wants. Like one
man said to me, "I want a girl that can check me from time to time." In
other words, women should also wear the pants when needed. It truly is
about balancing the feminine and masculine within. Because a feminine
yet assertive woman is a sexy woman.
Chelsea vijana wa darajani Stanford, jijini London,
wamewanyamazisha vinara wa ligi kuu ya England, Liverpool baada ya
kuwachakaza mabao 2-0 katika uwanja wao wa Anfield.
Liverpool ikiwa imeuanza mchezo huo kwa kasi na
kwa dhamira ya kupata ushindi ilishuhudia jahazi lake likitota katika
dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza.
Ba akisujudu kuashiria kumtukuza muumba wake aliemuwezesha kutupia goli la kwanza
Jose Mourinho akishangilia ushindi
Alikuwa ni Demba Ba aliyeanza kupeleka kilio kwa majogoo wa Liverpool
pale alipounasa mpira kufuatia nahodha wa Liverpool Steven Gerrard
kuteleza na Ba kupata mwanya wa kumfunga kirahisi Mignolet.
Liverpool hawakukubali kusalimu amri kwa
wageni,kwani waliendelea kupeleka mashumbulizi ya hatari langoni mwa
wapinzani wao wakiishia kwa kosa kosa. Liverpool wanapigania ubingwa wa
ligi kuu ya England kwa mara ya kwanza katika miaka 24 iliyopita.
Steven Gerrald haamini kilichotokea
Joe Allen na Luis Suarez walizidisha mashambulizi katika lango la
Chelsea, kabla ya Willian aliyeingia kipindi cha pili kufunga bao la
pili kwa timu yake ya Chelsea baada ya Fernando Torres bila uchoyo akiwa
katika nafasi ya kufunga alimpasia Willian na kuwaachia kilio wenyeji
wao Liverpool.
Chelsea katika mchezo huo ilikuwa ikipewa nafasi
finyu ya kuibuka washindi. Lakini ni Jose Mourinho aliyeibuka na
kicheko, huku Brendan Rodgers akiugulia kipigo cha kwanza kwa timu yake
tangu kuanza kwa mwaka huu.
Kwa ushindi huo sasa, Chelsea inaachwa pointi
mbili nyuma ya Liverpool ambayo inaoongoza ikiwa na pointi 80, baada ya
michezo 36. Msimamo wa timu hizo ni Liverpool pointi 80, Chelsea 78,
Manchester City 74, itakuwa na pointi 77 iwapo itaifunga Crystal Palace
katika mchezo wao, huku Arsenal ikichukua nafasi ya nne ikiwa na pointi
70. Manchester City na Arsenal zimecheza mechi 35 kila moja huku
Liverpool na Chelsea zikiwa zimecheza mchezo mmoja zaidi.
Luis Suarez chini ya ulinzi mkali
Heka heka langoni mwa Chelsea
Mashabiki chipukizi wa Liverpool hawaamini wanachokiona uwanjani