Wednesday, June 24, 2015
LIVERPOOL YANASA SAINI YA MBRAZIL FIRMINO
Firmino akiwa katika uzi wa Brazil

Firmino akiwa na uzi wa Hoffenheim
Klabu ya Liverpool imefanikiwa kumnasa Mbrazil Firmino aliekuwa akikipiga nchini Ujerumani na klabu ya Hoffenheim na kumsainisha mkataba wa ''Nyundo'' tano unaogharimu paundi za Uingereza Milioni 29 kuitumikia Liverpool.
Mkataba huo utakamilika sambamba na ukaguzi wa matibabu baada ya Firmino kurudi toka Chile ambako anaitumikia timu yake ya taifa ya Brazil katika michuano ya Copa Amerika.
Firmino akiwa ametikisa nyavu mara 47 katika mechi 151 alizokipiga na klabu ya Hoffenheim katika ligi ya Bundesliga nchini Ujerumani anakuwa mchezaji wa pili ghali katika klabu ya Liverpool baada ya Andy Caroll kunyakuliwa kwa kitita cha paundi za Uingereza milioni 35 mwaka 2011 akitokea Newcastle United.
Tuesday, June 23, 2015
Thursday, June 11, 2015
MTOTO WA PELE ATUA SWANSEA
NDREW AYEW
Mshambuliaji wa Ghana Andre Ayew
amejiunga na kilabu ya Swansea kwa uhamisho wa bure na kuandikisha
mtakataba wa miaka minne na kilabu hiyo.
Ayew mwenye umri wa miaka
25,amekuwa katika kilabu ya Marseille tangu mwaka 2006 lakini mkataba
wake na kilabu hiyo ya Ligue 1 ulikamilika mwezi uliopita.Mchezaji huyo aliyetajwa kuwa mchezaji bora na BBC mwaka huu alifunga mabao 52 katika mechi 181 katika kilabu hiyo na amelichezea taifa lake mara 62.
''Nilihisi kwamba huu ndio wakati mwafaka kwangu'',alisema Ayew. Nilihisi hamu ya kucheza katika ligi ya Uingereza na kutaka kukuwa kama mchezaji na kwamba Swansea ndio suluhu kwangu kwa njia yoyote''.
"Uaminifu na hamu ya klabu hiyo ulinifanya kujihisi kwamba ni kweli wananitaka.Wameonyesha hilo kwa kila njia''.
Subscribe to:
Posts (Atom)