Monday, July 6, 2015

CHILE BINGWA COPA AMERICA

Chile yanyakua kombe la Copa America baada ya kuichabanga Argentina kwenye mikwaju ya penati baada ya kushindwa kufungana ndani ya dakika 120. Chile ilipata penati 4 na Argentina moja tuuuu.

Wachezaji wa Chile wakishangilia ubingwa wa Copa America
null
Alexis Sanchez "SANchenga" akishangilia baada ya kutupia penati ya mwisho na ya ubingwa.

null
null
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa kwa wachezaji wa Argentina wakati Sanchez akipiga penati wa mwisho
null
Ushindi mtaaaaaamu hawa ni mashabiki wa Chile

null
Woyooooooooooooooooooooo    Vidal akishangilia ushindi

null
Wachezaji wa Argentina wakiongozwa na Messi kuvaa medali za ushindi wa pili huku wakilitazama kombe kwa "ugwadu"

 
Cheki mtanange huo hapa

Thursday, June 25, 2015

STARS MPYA YA MKWASA "MAFADHA WAPIGWA CHINI"

Kocha mkuu wa timu ya Taifa 'Taifa Stars' Charles Boniface Mkwasa (kushoto) akifafanua jambo leo wakati akitaja kikosi kipya tangu ateuliwe jana (kulia) kocha msaidizi Hemed Morocco
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ Charles Boniface Mkwasa (kushoto) akifafanua jambo leo wakati akitaja kikosi kipya tangu ateuliwe jana (kulia) kocha msaidizi Hemed Morocco


Kocha wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ Charles Boniface Mkwasa Jana ametangaza kikosi kipya cha timu hiyo ambacho kitaingia kambini hivi karibuni kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa marudiano wa kufuzu kucheza fainali za michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN) utakaopigwa kwenye uwanja wa Namboole, Kampala Uganda.
Mbali na kutangaza kikosi cha wachezaji 26, Mkwasa ametaja vipaombele vyake kwenye timu hiyo ambavyo amezingatia katika kuteua majina hayo. Amesema kitu pekee ambacho wameangalia ni uwezo wa mchezaji na nidhamu ndani na nje ya uwanja ili kuweza kujenga timu imara ambayo itakuwa na uwezo wa kupambana kwa kuwawakilisha watanzania.
Ametaja pia benchi la ufundi ambalo atashirikiana nalo katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu ya kuinoa Stars mpya, waliotajwa kwenye benchi la ufundi ni pamoja na kocha msaidizi Hemed Morocco, kocha wa makipa Peter Manyika, madaktari wa timu watakuwa wawili watatangazwa baada ya kuwasiliana na idara ya tiba, mtunza vifaa Hussein Sued ‘Gaga’ Mshauri wa timu Abdallah Kibadeni ‘King Kibadeni Mputa’, mratibu wa timu Alhaj Ahmed Idd Mgoyi na meneja wa timu ni Juma Mgunda.
Mkwasa pia ameomba ushirikiano kutoka kwenye vilabu vyote vya Tanzania na pindi watakapoliona benchi la ufundi la Stars kwenye vilabu vyao watoe ushirikiano kwani watakuwa wakitembelea vilabuni ili kufuatilia kwa karibu maendeleo ya wachezaji ili kuendelea kukiimarisha kikosi chao.
Ameishukuru kamati ya utendaji ya TFF kwa kumuamini na kumpa majukumu ya kuifundisha timu ya Taifa huku akikiri kuwa kazi hiyo siyo nyepesi kwasababu timu imeshapoteza mchezo wake wa nyumbani kwa idadi kubwa ya magoli lakini akakiri kuwa kwenye mpira chochote kinaweza kikatokea. Mbali na kuishukuru TFF, ameushukuru pia uongozi wa klabu yake ya Yanga kwa kumruhusu kwenda kuifundisha timu ya Taifa.
Lakini Mkwasa ameonya kuwa, wachezaji ambao wameitwa kwenye kikosi cha Taifa wanatakiwa kuendelea kufanya vizuri kwenye kikosi cha Stars na vilabu vyao. Mchezaji yeyote ambaye hatopata nafasi ya kucheza kwenye klabu yake hatoitwa kwenye kikosi cha Taifa hata kama anacheza nje ya nchi kama mchezaji nwa kulipwa.
Kikosi kipya cha Stars ni;
Mudathir Khamis (KMKM), Mwadini Ali (Azam FC) na Ally Mustafa ‘Barthez’ (Yanga). Mabeki ni Shomary Kapombe (Azam), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ (Simba SC), Mwinyi Hajji Mngwali (KMKM), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga SC), Kevin Yondan (Yanga SC), Hassan Isihaka (Simba SC), Aggrey Morris (Azam FC).
Viungo ni Jonas Mkude (Simba SC), Abdi Banda (Simba SC), Salum Telelea (Yanga SC), Frank Domayo (Azam FC), Simon Msuva (Yanga SC), Said Ndemla (Simba SC), John Bocco (Azam FC), Ramadhani Singano ‘Messi’ Simba SC na Deus Kaseke (Mbeya City). Washambuliaji ni Atupele Green (Kagera Sugar), Rashid Mandawa (Kagera Sugar), Ame Ali (Mtibwa Sugar), wakati wengine ambao wamewekwa akiba ni Juma Abdul wa Yanga SC, Mudathir Yahya wa Azam FC na Samuel Kamuntu wa JKT Ruvu.  Leo benchi la Ufundi la Stars litakutana na wachezaji wote walioteuliwa katika hoteli ya Tansoma, eneo la Gerezani, Dar es Salaam ili kuzungumza nao juu ya uzalendo na Mkwasa amesema Jumamosi timu itaenda kuweka kambi nje ya mji.
Mwisho, amewaomba wapenzi na mashabiki wa Stars wasahau yote yaliyopita kwasababu timu ipo mikononi mwao nao wanaamini watafanya vizuri. Amewaomba watanzania kuiunga mkono timu yao kama ilivyokuwa zamani na kuacha vitendo vya kuwadhihaki wachezaji ikiwa ni pamoja na kuwapiga mawe

Wojciech Szczesny wa Arsenal anamiliki mnyama mkali aina ya Tiger


Wojciech Szczesny wa Arsenal akijivinjari na Chui wake nyumbani kwake asubuhi ya leo

Wednesday, June 24, 2015

TAZAMA GOMA JIPYA LA CHAMELEONE-BWERERE


LIVERPOOL YANASA SAINI YA MBRAZIL FIRMINO


Firmino akiwa katika uzi wa Brazil


Firmino akiwa na uzi wa Hoffenheim

Klabu ya Liverpool imefanikiwa kumnasa Mbrazil Firmino aliekuwa akikipiga nchini Ujerumani na klabu ya Hoffenheim na kumsainisha mkataba wa ''Nyundo'' tano unaogharimu paundi za Uingereza Milioni 29 kuitumikia Liverpool.
Mkataba huo utakamilika sambamba na ukaguzi wa matibabu baada ya Firmino kurudi toka Chile ambako anaitumikia timu yake ya taifa ya Brazil katika michuano ya Copa Amerika.

Firmino akiwa ametikisa nyavu mara 47 katika mechi 151 alizokipiga na klabu ya Hoffenheim katika ligi ya Bundesliga nchini Ujerumani anakuwa mchezaji wa pili ghali katika klabu ya Liverpool baada ya Andy Caroll kunyakuliwa kwa kitita cha paundi za Uingereza milioni 35 mwaka 2011 akitokea Newcastle United.