Wenger awachimba mkwara Nasri, Clichy
- Jumatano, Mei, 25, 2011, 9:15
LONDON, Uingereza.
Meneja wa Arsenal mfaransa ARSENE Wenger amewakoromea nyota wake wanaogomea kusaini mikataba mipya, Samir Nasri na Gael Clichy kwamba hatokuwa na masihara katika hilo.
Nyota hao wamebakiza mwaka mmoja katika mikataba yao na kocha huyo wa Arsenal, Wenger anataka waamue mapema kuhusu kuongeza mikataba yao au waingizwe sokoni mwishoni mwa msimu huu.
“Tutamaliza tatizo hilo kwa haraka baada ya kumalizika kwa msimu,” alisema Wenger.
“Tunahitaji kufahamu mapema msimamo wao.”
Arsenal ilimpoteza kiungo Mathieu Flamini katika uhamisho huru mwaka 2008 baada ya kushindwa kuafikiana na nyota huyo wa Ufaransa.
Jambo hilo linamtisha Wenger na anadhani hali inaweza kujirudia.
Alisema: “Hatutaki yatokee kama yale yaliyokuwa kwa Flamini. Haturuhusu hilo kabisa. Tunataka kumaliza utata kabla ya msimu mpya kuanza.”

No comments:
Post a Comment