Friday, June 17, 2011

ASHUSHWA KWENYE NDEGE KWA KUVAA MLEGEZO.

Marman

Kijana mmoja nchini Marekani ajulikanae kama Marman mwenye umri wa miaka 20 pichani juu alijikuta akiingia katika masahibu ya kushushwa kwenye ndege baada ya kugundulika amevaa suruali huku ameishusha mpaka chini ya matako hapa chini maarufu kama "mlegezo au kata K" na kuacha nguo ya ndani ikionekana bila tabu, wakati Wamarekani wao wanaita "Baggy Pants" kwa kiswahili maana yake ni suruali bombo.
"Siku ya jumatano muda wa saa tatu asubuhi polisi wa San Francisco walipokea simu kuwa nje ya geti la shirika la ndege la marekani kuna mtu amevaa hovyohovyo" alisema Sgt Michael Rodriguez. Wafanyakazi wa uwanja wa ndege walimuona kabla Marman hajapanda ndege 488,walipomuona amevaa suruali chini ya matako lakini juu ya magoti walimtaka kupandisha suruali yake lakini Marman alikaidi amri hiyo na kuendelea na safari ya kuingia ndani ya ndege,ndipo wafanyakazi hao walipoamua kupiga simu polisi na polisi walipofika uwanjani hapo walimkuta Marman ameshaingia ndani ya ndege na amekaa raha mustarehe. Askari walipomuamuru kushuka aliwajibu itanichukua dakika 15 mpaka 20 kushuka ndipo askari walipomkamata kwa kosa hilo,na kuachiwa siku ya alhamisi kwa dhamana ya dola 11,000 za kimarekani.
Mama wa Marman alipohojiwa alisema mwanae alikuwa na hali mbaya kihisia kwani alitoka kuhudhuria mazishi ya rafiki yake ambaye ni mwanafunzi mwenzake siku ya jumanne baada ya kuuwawa. Lakini wamarekani wengi wamejitokeza kulalamikia swala hilo na kusema lina uhusiano na ubaguzi wa rangi kwani Marman alivaa jinsi ambayo ilikuwa haimkeri mtu moja kwa moja.

No comments:

Post a Comment