Hatimaye zile timu zilizokuwa zikiombewa madua ya kufa mtu zifike fainali ya michuano ya kombe la kagame yaani Simba na Yanga zote za Tanzania ambao ndio wenyeji wa michuano hiyo inayoshirikisha timu za ukanda wa Afrika mashariki na kati yametimia ambapo mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha dola za kimarekani 30,000 wa pili dola 20,000 na wa tatu dola 10,000 ambazo jumla yake ni dola za kimarekani zikiwa zimetolewa na Rais wa Rwanda Paul Kagame ingawaje katika mechi hiyo hatokuwepo na anategemea kuwakilishwa na waziri wa habari,vijana utamaduni na michezo wa Rwanda Protas Mitani,Kagame amekuwa akidhamini michuano hiyo tangu 2002.
Pazia la michuano ya kombe la kagame linatarajiwa kufungwa siku ya jumapili ya tarehe 10 julai 2011 kwa kuwakutanisha miamba ya soka la Tanzania Simba na Yanga baada ya ti mu hizo kufanikiwa kutinga fainali katika michuano hiyo kwa kuwaondosha baadhi ya vigogo vya soka katika ukanda huu wa Afrika kama vile El-Mereikh ya Sudan,APR ya Rwanda,Vital O ya Burundi na St George ya Ethiopia.
Kikosi cha Simba
Simba Sports Club walifanikiwa kutinga katika fainali hizo mbio zikiwa zimeanzia katika makundi na hatimae kutinga robo fainali, katika mechi ya robo fainali Simba ama Wekundu a msimbazi walikutana na Bunamwaya kutoka Uganda na kuiondosha kwa ushindi wa mabao 2-1 na kutinga nusu fainali,katika mechi ya nusu fainali Simba walikutana na miamba ya soka barani Afrika El-Mereikh ya Sudan na kufanikiwa kuwaondosha katika fainali hizo kwa changamoto ya mikwaju ya penati huku mlinda mlango Juma Kaseja akionesha uhodari wake kwa kupangua penati ya mwisho ambayo imewapeleka Wekundu hao mpaka fainali ya michuano hiyo ya Kagame na sasa uso kwa uso na watani wao wa jadi Dar Young Afrikans siku ya jumapili.
Kikosi cha Yanga
Yanga nao walipata kutika katika robo fainali ambapo mechi ya robo fainali walikutana na Timu ya Red Sea kutoka Eritrea na kuwaondosha kwa changamoto ya mikwaju ya penati,katika mechi ya nusu fainali ambayo imechezwa jana katika dimba kuu la Taifa ilishuhudiwa watoto wa Jangwani wakiitupa nje ya michuano hiyo timu ngumu ya St George kutoka Ethiopia pia kwa changamoto ya mikwaju ya maguu sita ama mikwaju ya penati. Sasa hofu miongoni mwa washabiki na wapenzi wa timu hizo imepanda kwa 100% ukizingatia katika michuano hii hakuna kujiandaa kutokana na ratiba kuwa mbanano ili kukamilisha michuano hiyo
No comments:
Post a Comment