Liverpool dakika za mwisho iliweza kupata mabao mawili ya haraka haraka na kupata ushindi wa kwanza kwenye uwanja wa Arsenal kwa miaka 11 iliyopita, hali ilnayozidi kumtia matatani meneja wa Arsenal, Arsene Wenger.
Arsenal - ikimchezesha Samir Nasri wakati huu mipango ya uhamisho wake kwenda Manchester City ikiwa imesita, iliweza kuwabana Liverpool hadi kiungo wao wa kutumainiwa Emmanuel Frimpong alipotolewa nje kwa kadi nyekundu zikiwa zimesalia dakika 20 kabla mchezo kumalizika.
Meneja wa Liverpool Kenny Dalglish haraka akamuingiza Luis Suarez na Raul Meireles uamuzi ulioonekana kuwa wa maana na wachezaji hao wawili walikuwemo katika mchakato wa kupatikana mabao hayo mawili.
Walishirikiana vizuri langoni mwa Arsenal hadi kijana chipukizi Ignasi Miquel, aliyechukua nafasi ya Laurent Koscielny aliyeumia, aliokoa mpira ambao ulimgonga Aaron Ramsey na kujaa wavuni na muda mfupi baadae Suarez alifunga bao la pili rahisi baada ya kupata pasi kutoka kwa Meireles katika sekunde za mwisho na kukamilisha ushindi wa kwanza wa Liverpool msimu huu.
Nayo klabu ya Newcastle iliendelea kufanya vizuri na kupata ushindi wa ugenini wa bao 1-0 dhidi ya Sunderland kwa bao lililofungwa na Ryan Taylor.
Wenyeji Sunderland walimiliki mpira kwa kiwango kikubwa kipindi cha kwanza, lakini Joey Barton wa Newcastle alikosa bao baada ya mpira wake wa kichwa alioupiga kumgonga Sebastian Larsson mkononi.
Stephane Sessegnon na Asamoah Gyan walikosa nafasi za kuipatia mabao Sunderland, wakati beki wao Phil Bardsley alitolewa nje kwa kadi ya pili ya manjano.
Ushindi huo wa Newcastle ina maana Newcastle imepoteza mechi moja tu kati katika michezo 13 iliyopita dhidi ya wapinzani wao hao wa jadi na ulikuwa ni ushindi wa kwanza kwa meneja Pardew tangu alipochukua hatamu za kuiongoza msimu uliopita.
Nayo Queens Park Rangers ama QPR wamefanikiwa kupata ushindi wao wa kwanza wa Ligi Kuu ya Soka ya England tangu mwaka 1996 baada ya mkongwe Tommy Smith kufunga bao lililoihakikishia ushindi huo wa kwanza wa ugenini dhidi ya Everton.
Eberton inayokabiliwa na matatizo ya fedha imekuwa ni mechi yao ya kwanza ya ligi kupoteza msimu huu.
Mabao yaliyofungwa na Gabriel Agbonlahor, Emile Heskey na Darren Bent yameipa ushindi Aston Villa katika mechi ya kwanza uwanja wa nyumbani wa Ligi kwa meneja Alex McLeish katika uwanja wa Villa Park.
Villa ilipata bao la kuongoza lililofungwa na Agbonlahor. Lilikuwa ni bao murua sana kwa mkwaju uliochongwa kwa ustadi na kujaa wavuni.
Heskey alifunga bao la pili kwa mkwaju wa chini chini kwa mkwaju wa yadi 20, lakini Morten Gamst Pedersen alifanikiwa kuifungia bao la kwanza Blackburn baada ya krosi ya Hoilett.
Lakini Bent aliihakikishia ushindi Aston Villa kwa bao la tatu rahisi baada ya mkwaju karibu na lango na kumpita mlinda mlango Paul Robinson.
Swansea City nayo ilifanikiwa kupata pointi ya kwanza katika kwanza Ligi Kuu ya England lakini mkwaju wa penalti waliopatiwa Wigan katika kipindi cha pili uliokolewa na mlinda mlango wa Swansea Michel Vorm na kuinyima ushindi Wigan.
Mlinda mlango huyo mpya aliyesajiliwa msimu huu, Vorm aliokoa mkwaju wa chini chini wa Ben Watson baada ya Jordi Gomez kuangushwa na Ashley Williams.
No comments:
Post a Comment