Wayne Rooney alifunga bao lake la tisa msimu huu wa ligi kuu ya Premier ya England, na kuiwezesha Manchester United, ikicheza katika uwanja wa Old Trafford siku ya Jumapili, kuifunga Chelsea magoli 3-1.
Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya England aliweza kufunga bao la tatu, baada ya wenzake Chris Smalling kufunga bao la kichwa kufuatia mpira alioupata kutoka kwa Ashley Young, na Nani alikuwa pia amefunga la pili kutoka yadi 25.
Magoli yote mechi ya Man United na Chelsea
Torres akikosa goli la wazi
Wasiwasi wa pekee kwa Sir Alex Ferguson, meneja wa Man U, ilikuwa ni kumtizama Javier Hernandez akichehemea katika kipindi cha pili, kufuatia Ashley Cole kumpata mguu.
Kulikuwa na matumaini ya Torres kuhakikisha angalau mechi ilikwisha kwa Chelsea kufungwa magoli 3-2, lakini mguu wake ulithibitisha kabisa ulishindwa kutimiza wajibu wakati huu, kwani mpira ulielekea juu, huku lango likiwa wazi kabisa.
Katika mechi nyingine za Jumapili, mpira kweli hauna adabu, na usiwacheke wenzako kwa kufungwa.
Liverpool waliaibika kwa kufungwa na Tottenham katika uwanja wa White Hart Lane magoli 4-0.
Matukio na magoli yote Tottenham na Liverpool
Sunderland vs Stoke City
Majirani wa Man U, Man City, walishindwa kuwika katika uwanja wa Craven Cottage, kwani licha ya kuongoza kwa magoli 2-0, hatimaye mchezo ulimalizika kwa sare ya 2-2.
Fulham na Man City
Arsenal Hoi Bin Taaban
Blackburn imeweza kupata ushindi wake wa kwanza katika Ligi Kuu ya England msimu huu na kumpunguzia ugonjwa wa moyo meneja wao Steve Kean baada ya kuwa nyuma lakini wakafanikiwa kuilaza Arsenal mabao 4-3 katika uwabnja wa Ewood Park.
Gunners walikuwa ndio wa kwanza kupata bao lililofungwa na Gervinho kutoka umbali wa yadi 12 lakini Blackburn walisawazisha kwa bao rahisi lililowekwa wavuni na Yakubu.
Mikel Arteta akaifungia Arsenal bao la pili kwa mkwaju safi wa yadi 18 kabla Alex Song hajajifunga mwenyewe.
Matukio na magoli Arsenal na Blackburn
Yakubu tena akaipatia Blacburn bao la tatu na kufanya ubao wa matokeo usomeke 3-2, na muda mfupi baadae Laurent Koscielny akajifunga mwenyewe kabla ya dakika za mwisho Marouane Chamakh kuipatia Arsenal bao la kufutia machozi.Kabla ya mechi hiyo mashabiki wa Blackburn walifanya maandamano wakitaka meneja wao Kean atimuliwe.
Koscielny akijifunga
Song akijifunga katika mechi hiyo
Wiki nzima meneja huyo alikuwa akijigamba kwamba yeye ni meneja anayefaa kwa klabu hiyo ya Blackburn na matokeo ya mechi hiyo dhidi ya Arsenal yanaweza kumfariji na kumuweka mahali pazuri kulinda nafasi yake.
No comments:
Post a Comment