NYOTA wa Ghana, Harrison Afful anaamini Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huu kati ya Esperance dhidi ya Wydad Casablanca itakuwa na uzuri wa aina yake. Beki huyo wa Esperance aliyeongoza ushindi wa jumla ya mabao 3-0 dhidi ya Al Hilal ya Sudan mwishoni mwa wiki, huku Wydad ikisonga mbele kwa fainali kwa ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Enyimba.
"Wydad ni timu nzuri. Wanatumia nguvu na akili na wanacheza soka nzuri kama tunavyofanya sisi," alisema Afful.
"Kwa hiyo itakuwa ni mechi nzuri ambayo kila moja atapenda kuitazama."
Esperance ambauo mwaka jana ilikosa ubingwa baada ya kufungwa na mabingwa wa DR Congo, TP Mazembe haijawahi kutwaa ubingwa huo wa Afrika tangu kuanzisha kwa Ligi ya Mabingwa kutoka kwenye mfumo wa Kombe la Washindi mwaka 1997.
Timu hiyo ya Tunisia imeshacheza na wabeba hao wa Morocco kwenye hatua ya makundi katika mashindano ya msimu huu.Mwezi Agosti wakiwa katika Kundi B mechi iliyofanyika Casablanca ilimalizika kwa sare 2-2, wakati ile ya marudiano jijini Tunis hawakufungana.
"Tumecheza mara mbili dhidi yao, hivyo kila moja anamjua vizuri mwenzake," alisema Afful. "Kwa kuzingatia malengo yetu ni umoja, tunaweza kufanya kile tunachotaka kuchukua ubingwa."
Wydad, imefuzu kwa fainali hizo kwa mara ya kwanza tangu ilipotwaa taji hilo mwaka 1992, watakuwa wenyeji wa mechi ya kwanza ya fainali itakayochezwa kati ya Novemba 04 au 06.
Mechi ya marudiano itafanyika wiki mbili baadaye nchini Tunisia. "Jambo zuri kwetu ni kuanza mechi ya kwanza nchini Morocco," alisema beki huyo wa Ghana.
Esperance iliyolazimika kucheza Jumamosi iliyopita bila ya mashabiki wake walipocheza dhidi ya Al Hilal kutokana na kufungiwa wa Shirikisho la Soka Afrika kufutia vurugu za mashabiki wake.
Hata hivyo, mashabiki hao wataruhusiwa kushudia fainali wakati Esperance watakapokuwa na ndoto ya kurudia kile walichokifanya mwaka 1994 ili waweze kufuzu kwa Kombe la Dunia la Klabu la Fifa.
"Kila moja Ulaya atazama Ligi ya Mabingwa Afrika na sisi wachezaji tunakitu tunachokipata kutoka katika mashindano haya," alifafanua Afful.
"Kucheza dhidi ya mabingwa wa Ulaya, Amerika Kusini katika Kombe la Dunia la Klabu ni kitu kizuri. Tunawatazama kila siku kwenye televisheni na kila wakati tunatama kucheza dhidi yao."
Kombe la Dunia la Klabu la Fifa mwaka 2011 linategemewa kufanyika nchini Japan kuanzia Desemba 08 hadi18.
No comments:
Post a Comment