Man City ilipoilaza QPR
Man ilipoifunga Sunderland
Chelsea ikiivurumisha Blackburn bakora 1 kwa uchungu
Arsenal ikiilaza WBA 3-0
KLABU ya Manchester City imeendelea kujisafishia njia kuelekea kwenye ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya juzi kuilaza Queens Park Rangers mabao 3-2.Alikuwa Yaya Toure aliyeanza kufumania nyavu katika dakika ya 16 ikiwa ni sehemu ya ushindi huo ulioiacha Manchester United kwa pointi tano zaidi.
Manchester United iliyokuwa imeikaribia timu hiyo kwa pointi, lakini mabao ya Edin Dzeko na David Silva yalifutwa na Jay Bothroyd na Heidar Helguson, na lile la Toure alilofunga kwa kichwa akiunganisha mpira wa Alexsandr Kolarov na kuifanya timu hiyo kushinda mechi yake ya 10 mfululizo.
United ilimzawadia kocha wao Sir Alex Ferguson ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Sunderland. Ferguson alitimiza miaka 25 jana akiwa kocha wa timu hiyo.
Nayo Chelsea iliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Blackburn.
“Ilikuwa siku nzuri kwetu,” alisema Ferguson. “Nilikuwa nina wasiwasi timu isingeweza kufanya vizuri. Nilidhani bado timu ina 'mawenge' ya kufungwa. Wakati mwingine lazima uwe na wasiwasi huu, hali iliyokuwa nayo, lakini tumeshinda.”
Ushindi wa timu hiyo uliwezeshwa na beki wa timu hiyo, Wes Brown aliyejifunga akiwa katika harakati za kuokoa. Beki huyo aliyekuwa Man. United, alijiunga na timu hiyo mapema Julai.
Ferguson alikwenda katikati ya uwanja ni kama alikuwa akikagua gwaride la wachezaji wa United na Sunderland. Mashabiki 75,570 walimpigia makofi Ferguson huku bosi wa klabu hiyo, David Gill akitangaza kuwa jukwaa la upande wa kaskazini mwa uwanja litaitwa jina la kocha huyo.
“Sikutarajia hili,” Ferguson alisema. “Ni kama wamenishtukiza.”
Chelsea ilipata bao lake kupitia kwa Frank Lampard katika dakika ya 50 huku ikiisogelea United. Newcastle imeendeleza wimbi la ushindi kwa kuichapa 2-1 Everton. Arsenal nayo iliizamisha West Bromwich Albion mabao 3-0.
No comments:
Post a Comment