Mmoja wa majeruhi akipata huduma ya kwanza
Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa Alain Juppe anatarajiwa kufanya ziara maalum nchini Uturuki, kujadili hatua dhidi ya mzozo unaoendelea nchini Syria.
Jumuiya ya nchi za kiarabu imeipa Syria siku tatu kumaliza tatizo hilo la sivyo itawekewa vikwazo vya kiuchumi.
Mmoja kati ya waandamanaji nchini Syria akiwa amebeba bango"Bashar acha mauaji"
Habari zinasema majeshi yaliyoasi yameendelea kulenga kambi za jeshi linalotii serikali.
Ni miezi minane ambapo waandamanaji wasiokuwa na silaha wamekuwa wakilengwa na wanajeshi watiifu kwa Rais Bashar Assad. Hali imebadilika na majeshi asi yameanza kukabiliana na mahasimu wao.Rais wa Syria Bashar Al-asaad
Duru kwamba majeshi yaliyoasi na chini ya mwavuli Jeshi Huru La Syria yameshambulia vituo kadhaa vya kijeshi mjini Damascus na kuwaua wanajeshi kadhaa wa serikali ya Syria bado hazijathibitishwa. Lakini ikiwa madai haya yana ukweli wowote, basi ni ishara kwamba huenda mzozo wa Syria umechukua mkondo hatari.
Jumuiya ya nchi za kiarabu imeonya kuiwekea Syria vikwazo vya kiuchumi ikiwa serikali ya Rais Assad haitakoma kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji na imetaka dhuluma hizo kukomeshwa siku tatu.
Maandamano nchini Syria kupinga utawala wa Bashar
Umati wa waandamanaji nchini Syria
Ututruki pia inatathmini kuiwekea Syria vikwazo. Tayari Marekani na jumuiya ya Ulaya zimeweka vikwazo, japo haijabainika athari za viwazo hivi ni ipi.
Jumuiya ya nchi za Magharibi na mataifa ya magharibi yameanza kutafakari mustakabali wa Syria bila uwongozi wa Bashar Al Asaad.
Waandamanaji nchini Syria
Hata hivyo pande zote ziko maakini kuzuia vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi hiyo. Hata hivyo ni vigumu kuafikia lengo hilo bila kuwepo ung'anganizi wa madaraka usipokuwa kwa mtutu wa bunduki.
No comments:
Post a Comment