Wednesday, November 2, 2011

TUZO ZA MWANANDINGA BORA WA DUNIA BARCELONA YATOA 8

Wayne Rooney ni mchezaji pekee wa Uingereza aliyeingia katika mchujo wa wachezaji watakaowania tuzo ya Fifa ya mwanakandanda bora wa mwaka ijulikanayo Ballon d'Or.

Barcelona imeingiza wachezaji wanane katika orodha ya mchujo huo, akiwemo Lionel Messi, ambaye ndiye mshindi wa tuzo hiyo kwa mizimu miwili iliyopita.
Nani (Man Utd), Luis Suarez (Liverpool) na Sergio Aguero (Man City) ni wachezaji wengine wanaocheza soka England waliomo katika mchujo huo.
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anaungana na Sir Alex Ferguson na meneja wa Chelsea Andre Villas-Boas katika orodha ya mameneja wanaowania tuzo kwa eneo lao la mameneja. Uamuzi utatolewa tarehe 9 mwezi wa Januari.
Rooney msimu wa ligi wa 2011 aliisaidia sana klabu yake ya Manchester United kuweka rekodi ya kunyakua taji la ligi la soka la England kwa mara ya 19 na kufika fainali ya Ligi ya Ubingwa wa Ulaya.
Mabingwa wa kandanda wa Ulaya klabu ya Barcelona imetawala orodha hiyo ya Fifa kwa kuingiza wachezaji wanane, ambapo Cesc Fabregas, aliyekuwemo kwa muda fulani katika kikosi cha Arsenal mwaka 2011, yumo katika orodha hiyo pamoja na Messi.
Real Madrid imeingiza wachezaji watano, akiwemo mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Cristiano Ronaldo na kiungo wa zamani wa Liverpool Xabi Alonso.
Orodha hiyo itachujwa tarehe 5 mwezi wa Desemba na kubakisha majina ya matatu kwa kila nyanja.
Wachezaji walioteuliwa kuwania tuzo ya Fifa na nchi zao katika mabano:



 Eric Abidal (Ufaransa),



Sergio Aguero (Argentina),



Karim Benzema (Ufaransa),


Iker Casillas (Hispania),


Cristiano Ronaldo (Ureno),

 
Dani Alves (Brazil),


Samuel Eto'o (Cameroon),


Cesc Fabregas (Hispania),


Diego Forlan (Uruguay),


Andres Iniesta (Hispania),


Lionel Messi (Argentina),

Thomas Muller (Ujerumani),


Nani (Ureno),


Neymar (Brazil),


Mesut Ozil (Ujerumani),


Gerard Pique (Hispania),


Wayne Rooney (England),


Bastian Schweinsteiger (Ujerumani),


Wesley Sneijder (Uholanzi),


Luis Suarez (Uruguay),


David Villa (Hispania),


Xabi Alonso (Hispania),


Xavi (Hispania).
Mameneja walioteuliwa kuwania tuzo hiyo na nchi pamoja na vilabu vyao:
Vicente Del Bosque (Hispania na timu ya taifa ya Hispania), Sir Alex Ferguson (Scotland/Manchester United), Rudi Garcia (Ufaransa/Lille), Pep Guardiola (Hispania/Barcelona), Jurgen Klopp (Ujerumani/Borussia Dortmund), Joachim Loew (Ujerumani na timu ya taifa ya Ujerumani), Jose Mourinho (Ureno/Real Madrid), Oscar Tabarez (Uruguay/Na timu ya taifa ya Ujerumani), Andre Villas-Boas (Ureno/Porto, Chelsea), Arsene Wenger (Ufaransa/Arsenal).

No comments:

Post a Comment