Friday, February 24, 2012

Man City kiboko,Inter Milan na Bayern Munich "Ndembendembe"


                       Man city 4-0 Porto

MABINGWA watetezi wa Europa Ligi, Porto wamevuliwa ubingwa huo baada ya kuchakazwa 4-0 na Manchester City na kuondolewa kwa jumla ya mabao 6-1 na vinara hao wa Ligi Kuu ya England juzi Jumatano.

Walifungwa 2-1 nyumbani hivyo timu hiyo ya Ureno ikawa na matumaini ya kurekebisha makosa ili iweze kusonga mbele kwa hatua ya 16 bora, lakini walipata pigo sekunde ya 19 kwenye Uwanja wa Etihad kwa bao la kuongoza la City lililofungwa na Sergio Aguero.

Katika usiku huo ambao kocha Roberto Mancini alisema mshambuliaji wake mtukutu Carlos Tevez amerejea baada ya kuwa nje kwa wiki kadhaa kufutia uamuzi wake wa kuomba radhi kwa kitendo cha kugomea kucheza, Aguero alionyesha kiwango cha juu na kuthibitisha kuwa City ina washambuliaji makini hata asipokuwepo Tevez.

Alitegeneza bao kwa mshambuliaji Edin Dzeko aliyeingia baada ya dakika ya 76 wakati City ilipoisambaratisha Porto.Pia bao la David Silva na David Pizarro yalikamilisha kalamu ya timu hiyo ya Mancini na kujikatia tiketi ya kufuzu kwa hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.

Porto walimaliza pungufu mchezo huo baada ya Rolando kuonyeshwa kadi ya njano ya pili kwa kumfokea mwamuzi akipiga bao alilolifunga Dzeko.

MARSEILLE, Inter Milan wamehadhibiwa kwa mbinu zao mbovu wakati Andre Ayew alipofunga kwa kichwa bao pekee na kuipa Olympique Marseille ushindi 1-0 kwenye mchezo huo wa kwanza wa Ligi ya Mabingw hatua ya 16 bora.

Ayew alifunga bao hilo akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Mathieu Valbuena katika dakika tatu za nyongeza na kuwaacha wachezaji wa Inter wakitikisa vichwa wasiamini kilichotokea.

Kocha wa Inter, Claudio Ranieri alimweka benchi mshambuliaji wa Argentina, Diego Milito, pamoja na kuwa huyo ndiye mchezaji pekee aliyeifungia timu hiyo katika michezo saba iliyopita, ukiwe ule aliofunga mabao nne walipotoka sare ya 4-4 na Palermo katika Serie A wiki tatu zilizopita.

Wesley Sneijder na Mauro Zarate hawakuwa kwenye kiwango kizuri dhidi ya Marseille, lakini Milito hakuingizwa na Ranieri alipotumia wachezaji wawili wa akiba kati ya watatu huku Giampaolo Pazzini pia alibaki benchi.

“Milito alikuwa na mafua wiki hii. Sikutaka kuhatarisha afya yake,” alisema Ranieri.Ranieri anaonekana anataka kujipanga kwa ajili ya mchezo wa marudiano utaofanyika nyumbani kwao San Siro hapo Machi 13.

BASEL, Timu ya Basel imepiga hatua moja kubwa katika Ligi ya Mabingwa baada ya kuidungua Bayern Munich kwa bao 1-0 na kujiweka vizuri kwenye harakati zake za kufuzu kwa robo fainali.

Mshambuliaji Valentin Stocker aliyeingia akitokea benchi alifunga bao hilo la ushindi kwa mabingwa hao wa Uswisi dakika ya 86 kwa shuti lililompita tobo kipa wa Bayern, Manuel Neuer.

Bayern walikosa mara mbili kwenye mchezo huo wakati mashuti ya Aleksandar Dragovic na Alexander Frei yalipogonga mwamba na kutoka, timu hiyo ya Uswisi ambayo mfumo wake wa kushambulia kwa kushtukiza ndio uliowamaliza Manchester United kwenye hatua ya makundi.

Hilo ni pigo jingine kwa Bayern ambao wamekuwa kwenye kiwango cha chini kwenye Bundesliga wakiwa nyuma kwa pointi nne kwa vinara Borussia Dortmund

No comments:

Post a Comment