Thursday, March 29, 2012

FABRICE MUAMBA "AFUFUKA" WACHEZAJI NA FAMILIA ZAO WAMIMINIKA HOSPITALINI KUMJULIA HALI


FABRICE MUAMBA

Habari kutoka London Uingereza zinasema kiungo wa Bolton, Fabrice Muamba ameweza kuamka kitandani na kuzungumza na wachezaji wenzake waliokwenda kumuona hospitali.


Reo Cooker,Pratley na Davies wakitoka Hospitalini kumtembelea Muamba

"Anatia moyo na hali yake inazidi kuimarika," ilisema taarifa ya pamoja ya klabu na hospitali.

Kocha wake, Owen Coyle alisema Muamba alikuwa akiangalia mechi za ligi za mwishoni mwa wiki ikiwemo timu yake ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Blackburn.


Defoe na mama yake (Sandra) na nyuma ni dada yake (Chonte) walipomtembelea Muamba Hospitalini

"Nilikuwa nasikia raha, nilikuwa sijisikii hata kulala wakati tunaongoza kwa mabao 2-0," alisema Muamba.

Kocha huyo alikuwa katika mipango ya mechi ya marejeo ya Kombe la FA na aliwashukuru mashabiki wa Tottenham Hotspur kwa msaada wao.


Benoit Assou-Ekotto akiwatilia saini mashabiki wake alipokwenda kumjulia hali Muamba hospitalini

Bolton inarudi kwenye Uwanja wa White Hart Lane kwa ajili ya mechi hiyo iliyovunjika baada ya mchezaji huyo kupatwa na shambulio la moyo na kuanguka uwanjani.

"Tutakuwa tukikuwaza, Fabrice." Wachezaji wa Bolton walisema walipomtembelea mwenzao ikiwa ni siku chache kabla ya kurudiana na Spurs.


Essien akizungumza na waandishi wa habari nje ya hospitali alipoenda kumtembelea Muamba

Wakati wanajiandaa kwenda kumtembelea mchezaji mwenzao, Zat Knight, David Wheater na Jussi Jasskelainen walikuwa wanashindwa hata kutoka hotelini kwenda London Chest Hospital.


Shaun Wright Philips na Ashley Cole nao walijumuika Hospitalini kumjulia hali Muamba

Wachezaji wa timu hiyo walikuwa wamevalia suti za michezo, na walipanda teksi kwenda hospitali kumwona.


Nahodha wa Bolton Davie na mkewe(Emma) na mtoto wao walipomtembelea Muamba

Bolton pia walirudia kuipongeza Tottenham hasa kitengo chake cha huduma pamoja na shabiki wa Spurs, Dk. Andrew Deaner.


Shabiki akiweka mdoli nje ya Chest Hospital jijini London alikokuwa akitibiwa Muamba.

Taarifa iliishukuru Tottenham waliokuwa wakimtakia kila la kheri Muamba, waliwashukuru London Ambulance Service na wale wote waliojitolea kutoka taasisi za moyo kumsaidia Muamba.

No comments:

Post a Comment