Thursday, March 8, 2012

MBWANA SAMATTA YUKO JUU ATIKISA NYAVU HUKO MBUJI-MAYI


Mbwana Samatta mfungaji wa goli pekee na la ushindi la TP Mazembe dhidi ya S.M Sanga Balende

MBWANA Samatta ameendelea kudhihirisha kuwa ni moto wa kuotea mbali katika kuzifumania nyavu, baada ya kuifungia timu TP Mazembe bao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya timu ya S.M Sanga Balende.
Mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (Super League) ilichezwa mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Kumbuji- Mayi, kilomita 1000 kutoka jiji la Lubumbashi.

Mbwana alifunga bao hilo dakika 48, kutokana na krosi ya Kilitcho Kasusula aliyeingia kipindi cha pili dakika ya 46 kuchukua nafasi ya Ngandu Kasongo.
Muda huo ndiyo aliingia Mtanzania mwingine, Thomas Ulimwengu kuchukua nafasi ya Yannick Tusilu.
Baada ya mchezo huo, rais wa klabu hiyo, Moise Katumbi aliwapongeza wachezaji wake kwa ushindi huo mgumu.
Haya ni mafanikio mengine kwa Samatta akiwa na TP Mazembe na ndiye anaongoza kwa ubora kwenye timu hiyo tangu msimu mpya wa ligi uanze.

Hivi karibuni, Kocha wa timu ya Taifa (Taifa Stars, Jan Poulsen alimtema nyota huyo chipukizi kwenye kikosi cha Stars kwa maelezo kwamba hajitumi anapoitwa kuchezea timu hiyo.

1 comment:

  1. Ingekuwa nchi za wanaopenda soka lao hawawezi kumuacha kocha ateue timu halafu aache wachezaji mahiri kama Samatta, tumewahi kusikia wachezaji kama Ronaldhinyo,Dunga,George weah na wengine wameleta mzozo kwa kutoitwa katika timu zao za Taifa..sasa sisi tunamuangalia tu huyu Poulsen na hana jipya katika timu yetu ya Taifa anazidi tu kutusokomeza shimoni katika viwango vya soka.

    ReplyDelete