Wednesday, March 28, 2012
VICHUPI VYAPIGWA 'STOP' MASHINDANO YA OLIMPIKI 2012
Vichupi vilivyopigwa "stop"olimpiki
Wanawake sasa hawatohitajika kuvaa vichupi'bikini"katika mchezo wa volleyball ya ufukweni katika mashindano ya olimpiki yatakayofanyika katika jiji la London nchini Uingereza mwaka huu.
Utaratibu huo mpya umetangaza siku ya jumanne 27 March 2012 na kamati ya maandalizi ya Olimpiki ukisema kuwa katika mashindano ya Olimpiki ya kipindi cha kiangazi kwa upande wa mchezo wa Volleyball wanawake watatakiwa kuvaa kaptula fupi ama sketi fupi"vibwaya".
Tangu mashindano ya Olimpiki yalipoanzishwa mwaka 1996 huko Atlanta wanawake wamekuwa wakivaa vichupi"Bikini" na sasa hawatoruhusiwa tena kuvaa vichupi wanaruhusiwa kuvaa kaptlula ama sketi fupi pia "body suit".
Mabadiliko hayo yamefanyika ili kuweza kuenda sambamba na tamaduni za nchi mbalimbali zinazoshiriki michezo ya olimpiki. Kaptula ama sketi fupi zenye urefu wa nchi 1.18 juu ya magoti au bodysuit ndio mavazi yatakayoruhusiwa kwa mujibu wa utaratibu mpya wa kamati ya maandalizi ya olimpiki.
Kamati hiyo imesema utaratibu huu mpya utasaidia kushawishi nchi zenye tamaduni tofauti kukutana pamoja bila migongano.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment