Friday, May 25, 2012

CHADEMA IKO JUU, CHEZEA MNYIKA WEWE!


John Mnyika,Mbunge wa Ubungo(CHADEMA) aliyeshinda kesi ya uchaguzi.

Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Ubungo umeunguruma katika mahakama kuu kanda ya Dar es salaam na mbunge wa Jimbo la Ubungo John Mnyika (Chadema) amemshinda tena Hawa Ng'humbi (CCM) baada ya Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam kutoa hukumu kuwa ushindi wa Mbunge Mnyika uliofanyika Oktoba 31, 2010 ulikuwa wa halali.

Kesi hiyo namba 107 ya 2010, ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CCM, Hawa Ngh’umbi dhidi ya Mnyika ambaye ni mdaiwa wa pili katika kesi hiyo akitetewa na Wakili Edson Mbogoro.

Mdaiwa wa kwanza katika kesi hiyo iliyoko mbele ya Jaji Upendo Msuya ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na aliyekuwa Msimamizi wa Uchaguzi (RO) katika jimbo hilo, (aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni) ambao walikuwa wakitetewa na Wakili Mkuu wa Serikali (PSA), Justice Mulokozi.

Katika uchaguzi huo, uliofanyika Oktoba 31, 2010, Msimamizi wa Uchaguzi, Raphael Ndunguru alimtangaza Mnyika kuwa mshindi Novemba 2, 2010 baada ya kupata kura 66,742. Ngh’umbi alipata kura 50,544.

Hata hivyo, Ngh'umbi hakuridhishwa na matokeo hayo akaamua kufungua kesi Mahakama Kuu kuyapinga, akimtumia Wakili Issa Maige.

Katika hati yake ya madai na wakati akitoa ushahidi mahakamani, Ngh’umbi na mashahidi wake walidai kuwa kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu na kisheria katika ujumlishaji wa kura na utangazaji wa matokeo ambao umeathiri matokeo hayo.

No comments:

Post a Comment